Kwa mtaji huu stars hashindi hata mechi moja

kwa nn wasingeandika jina la mchezaji na makonda hapo anafanya nn?.
Mkuu hapo mbona hamna shida hata kidogo au thinking capacity ndiyo tatizo. Kilichozinduliwa ni jezi mpya hilo jina Magufuli hapo nyuma limewakilisha jina la mchezaji yaani wangeweka jina lolote kuwakilisha majina ya wachezaji siyo kwamba jezi zote zitakuwa na jina la Magufuli. Mfano kipa wetu ni Aishi manula jezi yake litakuwa na jina la Aishi manula lakini litaandikwa kwa mfumo huo wa hilo jezi lililoshikiliwa hapo . Kwa maneno machache hiyo ni SAMPLE tu wangeandika hata jina la MAKONDA AU MAALIM SEIF haingemaanisha ni hivyo kwa jezi zote. Si kila jambo la kupinga hata kama hujaelewa bwana mkubwa kuuliza ni muhimu. Halafu usidhani jezi ziko 23 tu ziko nyingi na hata wewe unaweza ukawana original jezi yenye jina lako.
 
RC Makonda anataka sana kuwa Mbunge katika moja ya Jimbo la Mkoa wa Dar es Salaam na hasa hasa la Kawe lakini pia RC Makonda ameshaaminishwa kuwa anakuja kuwa Rais wa Tanzania hivyo tayari ameshasoma Saikolojia ya Watanzania hasa kwa wana Dar es Salaam kuwa wanapenda Mpira na tayari ameshamuweza Rais wa TFF Karia hivyo Karia anatumika Kufanikisha lengo lake hilo ambalo kwa mtazamo wangu tayari naona kama vile RC Makonda ameshalifanikisha. Ipo Siku hata Ofisi za TFF zote zitahamia hapo Ilala Boma zilipo Ofisi za Mkuu wa Mkoa Makonda na Timu ya Taifa itachaguliwa na Makonda pia.
Labda awe raisi wa vicoba
 
Write your reply...Sipati picha nikiifikiria siku kwanza ambayo Makonda aliingia Dar ...sijui alikua na dhamira gani moyoni
 
Write your reply...Sipati picha nikiifikiria siku kwanza ambayo Makonda aliingia Dar ...sijui alikua na dhamira gani moyoni
Hapo sasa! Labda alijipanga kazi yeyote hata kuwa "house girl" inatosha.
kwinyara___ByIaUpZA8Tq___.jpeg
 
watu mnapenda kuhoji vitu vidogovidogo visivyo na mashiko............hivi kwani wewe huwezi kununua jezi ukaandika jina lako?mbona ni mambo ya kawaida tu acha uzwazwa
 
watu mnapenda kuhoji vitu vidogovidogo visivyo na mashiko............hivi kwani wewe huwezi kununua jezi ukaandika jina lako?mbona ni mambo ya kawaida tu acha uzwazwa
Huna akili, ndio maana kwako unaona ni jambo dogo tuu.
Lakini ungeshughulisha akili yako hata kidogo ungeona mantiki ya hoja
 
Nimeikimbuka filamu ya "One down two to go" ya Fred Williamson, Jim Brown na Jim Kelly.Ila kwetu imegeuka.
Afcon ambayo Stars wanashiriki baada ya miaka 39 kupita imetuonyesha jinsi CCM walivyo igawa nchi na kupoteza hadhi kwa kukosa uzalendo.
Wakati Angola walipopata nafasi kushiriki mashindano ya World cup South Africa, nakumbuka hata waasi wa Unita waliweka silaha chini muda wote wa mashindano ili kuonyesha dunia kuwa ANGOLA KWANZA mengine baadae.
Lakini oneni Stars baada ya kuifunga Uganda na Polepole kuita ushindi ule kuwa ni wa CCM sijui ununua ndege, sgr na Stiglers gouge watu walivyo poteza mapenzi na timu yao.
Wapo waliofikia kushangilia ushindi wa Senegal kwa vile tuu wanaichukia CCM.
Mbona Kenya hakuna anayeisema vibaya Harambee stars? Uganda nk?
Hiki liwe somo kuu kwa CCM kuwa kuwagawa wananchi ni jambo baya na la hatari, jee ingekuwa tunapigana vita nini kingetokea?
Vita ya Kagera tulishinda kwa vile tulikuwa wamoja na watu walichangia hadi kuku, wakati Uganda kulikuwa na mgawanyiko na waliokuwa wanapinga maovu ya Amin ndio walitusaidia kumchapa.
CCM iache tabia za kutugawa wananchi, Magu ajue na Chakubanga waelewe wanalipoteza taifa kwa kujenga chuki.
 
9 Reactions
Reply
Back
Top Bottom