Kwa mtaji huu hata jeshi likichukua nchi hamna kitu

President Elect

JF-Expert Member
Aug 9, 2011
693
212
Baadhi ya wananchi wamekuwa wakituma maoni yao kwenye radio mbalimbali' wakisema bora jeshi lichukue nchi.

Hata hivyo kutokana na maafisa kadhaa wa ngazi za juu jeshini kuhusishwa na kashfa nzito za ubadhirifu, ni wazi kwamba wazo hilo si muafaka hata kidogo.

Utawala wa kijeshi unaweza kuipeleka nchi yetu kubaya zaidi, kinyume na matarajio ya wale wenye matamanio kama hayo.

Dhana ya utawala bora na demokrasia ya kweli, kwa kufuata misingi ya sheria bila ubaguzi, ndio njia sahihi zaidi ya kututoa hapa tulipo.
 
Back
Top Bottom