Kwa mtaji huu hakuna maendeleo, zaidi ni maumivu tu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kwa mtaji huu hakuna maendeleo, zaidi ni maumivu tu

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by gollocko, Apr 24, 2012.

 1. gollocko

  gollocko JF-Expert Member

  #1
  Apr 24, 2012
  Joined: Dec 20, 2011
  Messages: 2,830
  Likes Received: 1,544
  Trophy Points: 280
  Natumai mu wazima na mnaendelea kulisukuma gurudumu la maendeleo la nchi yetu ambalo kwa mtazamo wangu linaenda kinyumenyume na wala hakuna matumaini ya kuligeuza na kulipeleka mbele.Kilichonifanya nijitokezeleo ni hali halisi ya nchi yetu inavyoendelea hivi sasa kuwa halijojo hasa katika utendaji wa serikali, kwa mtazamo wangu kwa serikali hii iliyopo madarakani ni vigumu sana kupiga hatua yoyote ya maendeleo hata tushushiwe magunia trilioni ya pesa au dhahabu.

  Utendaji wa baraza la mawaziri
  Baraza hili la awamu ya nne ndo ambalo limetia fora kwa madudu mengi ambapo kila wizara kuna ubadhilifu mkubwa wa mali za umma ulio waziwazi, usimamiaji wa mawaziri hawa ni kama haupo.
  Waziri mkuu yeye yupoyupo tu hajui amsimamie nani na amwache nani kilichopo ni bore liende siku ikipita kimya kwake ndio nafuu.
  Hili limethibitishwa na tuhuma ambazo mawaziri na manaibu wao kutofautiana hadharani huku ikionekana mawaziri hawana kabisa mamlaka kamili ya kuzisimamia wizara zao.
  Kwa mfano;Waziri wa uchukuzi Omari Nundu na Naibu wake Athumani mfutakamba kutunishiana misuli kama wote ni mawaziri kamili. Nundu akimtuhumu naibu wake kusafiri bila kibali chake naye Mfutakamba akijitetea kupata kibali toka ofisi ya waziri mkuu huku akijua waziri wake yupo.

  Hii ina maanisha kuwa katika serikali hii manaibu waziri, makatibu wakuu na makamishina kila mmoja aweza jifanyia maamuzi mwenyewe na kuwaruka mabosi wake na baadae kupata Baraka za waziri mkuu au raisi mwenyewe nab ado mambo yakaenda watakavyo. Waziri mkuu mwenyewe hana nguvu yoyote ya kuwaajibisha mawaziri hata kama wamekosea, hivyo kila mtu ndani ya serikali anendesha kaidara kake atakavyo ilimradi anapatana na raisi au waziri mkuu. Mifano iko mingi hebu tujikumbushe matukia ya Zakhia Megji na Daudi Balali, Mwantumu Mahiza na Blandina Nyoni na sasa Cyril Chami na Lazaro Nyarandu.
  Bunge

  Wabunge siku zote wamekuwa wakilalamika kuwa serikali haishughurikii mapendekezo yake na mara zote imeonyesha zarau kwa wabunge, lakini tujiulize dharau hii inatoka wapi? Kwa ujumla dharau ya serikali dhidi ya bunge husababishwa na wabunge wenyewe, kwani wenyewe wabunge hushindwa kuchua maamuzi na kushikilia misimamo yao na kubaki wakibwabwaja tuuu bila hata ya mafanikio. Kwa mfano wabunge hasa wa CCM ambao ndio walio wengi kuna vipindi walikuwa wanabwatuka utadhani mwisho wa dunia umefika lakini wakiitwa kwnye vikao vyao vya chama hutoka wamenywea utadhani vifaranga vya kuku vilivyonyeshewa, hebu tujikumbushe sakata la Jairo,Ngeleja na Mgao wa umeme na hili la sasa la ubadhirifu serikalini achana na la Richmond ambalo Lowassa kama sio hasira zake angekuwa bado yupo ofisini mpaka leo.

  Mara zote wabunge wanapobwabwaja serikali huja na mipango ya kuwalainisha, kuwapumbaza na wao kama mazuzu vile hukubali na kubaki kimya halafu baadae wakiona mipango haitekelezeki wanaanza kulalama. Kwa mtazamo wangu watanzania tusiwe tunadanganyika kirahisi mara tuonapo wabunge wamekuwa wakali kama pilipil pale bungeni na kuanza kuwamwagia sifa kuwa bunge limekuwa zuri, wengi wao hutaka vyeo au kujionyesha kwamba wanauchungu na nchii lakini ni bure tu.(Hapa nawazungumzia zaidi wale wa chama tawala maana ndio wenye tabia hii).

  Mwisho nahitimisha kwa serikali hii na bunge hili, hakuna maendeleo yatakayokuja tutabaki hivi hivi mpaka tutakapoamka na kubadilisha serikali yote kuanza upya. Pili tuache tabia ya kuwasifu wabunge kila wabwabwajapo mjengoni tusubiri maamuzi yao ya mwisho ndipo tuwape sifa zao. Jiulize katika hoja ya Zitto ya kutokuwa na imani na waziri mkuu wako wapi wale ambao walipata sifa kwa ubwabwajaji na kusema mbele ya maslahi ya taifa wao hawana undugu na mtu? Ole Sendeka,January Makamba,Anna Kilango,Godfrey Zambi n.k
  kumbukeni maneno bila vitendo hatuendi popote!

  Nawasilisha;
   
 2. BASHADA

  BASHADA JF-Expert Member

  #2
  Apr 24, 2012
  Joined: Jul 13, 2011
  Messages: 487
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 35
  Siwezi kusoma thread iliyoandikwa kwa maandishi madogo kiasi hiki na yamebananishwa. Mleta mada jifunze kupangilia maandishi yavutie wasomaji, bila hivyo ni magumashi tuu,..
   
Loading...