Francis12
JF-Expert Member
- Sep 30, 2016
- 7,533
- 22,278
KWANINI SERIKALI INAMTESA MAREHEMU? AMEWAKOSEA NINI?
Hali halisi ya mjini Moshi, kila mwananchi ameguswa na msiba na kila mmoja anajiandaa kwenda kumuaga marehemu Dkt Philemon Ndesamburo, lakini Serikali ya CCM inaliagiza jeshi la polisi kukwamisha shughuli hii kwa makusudi, yanatoka maelekezo ya ajabu ambayo yanaweza kuleta athari kubwa zaidi.
Umati wa watu ndiyo unaopelekea watu wapite kwenye njia Kuu, watu ni watulivu, ni wengi, lakini wanapanbiwa njia nyembamba kama kwamba huu sio msiba mkubwa, tena kwa vitisho na kuashiria uvunjifu wa amani, Jeshi la polisi kwanini msiwe mnajiongeza kitaaluma kuliko kufuata maagizo ya viongozi wa kisiasa wanaowachonganisha na wananchi?
Watanzania watakumbuka, alipokufa Mohamed All (bondia wa zamani) mwili wake ulizungushwa maeneo yote ya mji na watu walijaa barabarani wakiusubiri wamuage, mwili ulikuwa u azungushwa kwaajili hiyo, sasa kwa mzee Ndesa mwili kutolewa hospital kupelekwa uwanjani kuagwa mnawakatalia wananchi, mna nia gani? Mbona mnaifanya Tanzania kuwa sio mahala salama pa kuishi?
Nani asiyetambua uzito wa msiba, hata mkawazuia watu kwenda pamoja kumuaga marehemu, mnasema hayo ni maandamano? Mbona maeneo mengi nchini kwasababu ya imani zetu tofauti, lakini kwa sisi tunaotumia kuubeba mwili wa marehemu kwenda nao mpaka makaburini na hutumia njia Kuu na wananchi huwa watulivu kwasababu wanafahamu uzito wa msiba?
Kwa msiba wa mzee Ndesa, Moshi imefiwa, serikali walipaswa wawaache wananchi wamuage kwa amani na Uhuru, hakika haya mambo yatakuja kusababisha watu walipane visasi mtu kwa mtu, maana sio kwa manyanyaso haya.. zipo nchi zilikuwa tulivu kuliko Tanzania lakini hivi sasa historia imegeuka, Tanzania sie ni akina Nani yashindikane hayo?