Kwa mshahara huu wa 185,000 Rhino cement haizingatii vigezo vya kima cha chini cha mshahara

Kambilingo

New Member
Jul 15, 2016
2
1
Jamani hivi kwa kupitia mikataba kama hii, serikali ina nia njema na watanzania sisi masikini kama ilivyolenga kuwasaidia watanzania hawa? ni kweli kima cha chini cha mshahara kwa mfanyakazi ndio hiki?

Kiwanda kikubwa kama hiki cha cement chenye matawi nchi zaidi ya tano Afrika ni kweli hakiguswi na maisha ya mtanzania hadi kinawalipa hivi?

Waziri mkuu wao aliyekuja juzi kujiosha na uwekezaji na akakaribishwa kwa ngoma na mizinga ya jeshi amekuja kusaini vitu kama hivi?

Tafadhali rais tusaidie maana waliopita wote wamepita kando ndani ya kiwanda hiki.

Hatutoki namna hii.
 

Attachments

  • MKATABA (1).pdf
    1.4 MB · Views: 161
Huu ni unyonyaji wa hali ya juu ukilinganisha na aina ya kazi yenyewe, serikali iangalie kwa jicho la tatu uwekezaji wa aina hii.

Sikatai kwamba tatizo la ajira nchini ni kubwa lakini, kutumia kama kigezo cha kuwanyonya watanzania, hili halikubaliki hata kidogo.

Mamlaka husika walifutilie.
 
Mkuu hata mm nilipitia hapo mwaka juzi na wala sishangai maana kama safety manager alikuwa analipwa laki 2 na ni graduate,usifanye mchezo na hao wahindi tena huyo aloweka saini hapo anaitwa girish kumar alikuwa ndo plant manager rhino cement ya mkuranga kahamishiwa huko
 
Dah... Kwani Umelazimishwa bana?? Mbona ishu nyingine rahisi tu...Acha usisaini Kama mdogo...
 
Back
Top Bottom