Kwa Mpenzi Wako - Je, unajali/ulijali ni wangapi aliwahi kutembea nao kabla yako? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kwa Mpenzi Wako - Je, unajali/ulijali ni wangapi aliwahi kutembea nao kabla yako?

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Steve Dii, Oct 23, 2008.

 1. Steve Dii

  Steve Dii JF-Expert Member

  #1
  Oct 23, 2008
  Joined: Jun 25, 2007
  Messages: 6,416
  Likes Received: 67
  Trophy Points: 145
  "Pale" aliponiuliza, miye niliona vibaya kutomjibu, na nilimjibu kwa namna yangu. Nilizidisha idadi ya wale niliowahi tembea nao mara mbili ili kumwona kama atavumilia na kuhimili kishindo cha hiyo idadi. Maskini; na alihimili, alivumilia. Miye sikutaka kumuuliza, ila "yeye" mwenyewe akasema, "mbona simuulizi?" Nami nikaitikia wito, nikamuuliza. Idadi aliyonitajia ilinipagaisha. Ilikuwa mara mbili ya ile niliyo izidisha mara mbili mimi.-- dot-- dot-- dot, Mwisho.

  Moral of the story: Does it really matter how many men/women your sexual partner has ever slept with?!
   
 2. Yona F. Maro

  Yona F. Maro R I P

  #2
  Oct 23, 2008
  Joined: Nov 2, 2006
  Messages: 4,237
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 0
  Naona kama unampenzi take her or him kama alivyo hapo alivyo kwa muda huo kama unataka ajirekebishe ongea nae ila ukisema uanze kufuatilia maisha yake haswa ya kimahusiano unaweza lia siku moja kwa sababu unaweza kumhukumu kutokana na historia yake -- na maanisha utaanza kumfuatilia kujua hili na lile unapoteza muda wako kwa mambo hayo wakati u need to make ur life better in a wonderfull world
   
 3. S

  Sabri-bachani Member

  #3
  Oct 23, 2008
  Joined: Apr 3, 2008
  Messages: 96
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Khee. Usinchekshe. Hazina makombo hizo
   
 4. Steve Dii

  Steve Dii JF-Expert Member

  #4
  Oct 23, 2008
  Joined: Jun 25, 2007
  Messages: 6,416
  Likes Received: 67
  Trophy Points: 145
  Ahsante kwa ushauri Shy. Hata hivo kuna swali naomba kuongezea... je, kama mpenzi wako alikuwa anajishughulisha na biashara ya ngono kabla ya kuwa na wewe, kujua si itakuwa bora, au?!
   
 5. Yona F. Maro

  Yona F. Maro R I P

  #5
  Oct 23, 2008
  Joined: Nov 2, 2006
  Messages: 4,237
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 0
  Kama alikuwa na biashara hiyo ni vizuri akuambie ili ujue jinsi ya kukabiliana nayo siku za baadaye usije ukaambiwa na watu baadaye ikaja kuwa ishu si unajua siku hizi dunia invyoweka watu karibu zaidi -- yaani ni ngumu sana kuficha makucha na mambo mengine yako
   
 6. Steve Dii

  Steve Dii JF-Expert Member

  #6
  Oct 23, 2008
  Joined: Jun 25, 2007
  Messages: 6,416
  Likes Received: 67
  Trophy Points: 145
  ...ila hubakia na reputation tu...
   
 7. Yona F. Maro

  Yona F. Maro R I P

  #7
  Oct 23, 2008
  Joined: Nov 2, 2006
  Messages: 4,237
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 0
  Msichana ambaye niliachana nae mwaka huu niligombana nae siku moja then ndugu yake mmoja akaja kuniambia ukweli kuhusu dada huyo kwamba alikuwa anajiuza wakati akiwa chuo ili aweze kupata chochote wakati huo jamaa ambaye alikuwa nae hakuwa na uwezo wowote kwahiyo nae alitegemea huyo dada ajiuze ili aweze kupata chochote

  tulivyogombana ndio akaniambia ukweli huo --- kumbe zamani ningejua hii hata nisinge hangaika nae unaona nimekaa nae miaka 2 hivi so thats how it ended

  na aliniambia hata kwangu alikuwa anajiuza
   
 8. Yona F. Maro

  Yona F. Maro R I P

  #8
  Oct 23, 2008
  Joined: Nov 2, 2006
  Messages: 4,237
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 0
  Ahsante naima kwa kunipa courage , ushauri na msaada mwingine kuhusu suala hili angalau nimeweza kupambana nalo na kujifunza ya walimwengu
   
 9. Steve Dii

  Steve Dii JF-Expert Member

  #9
  Oct 23, 2008
  Joined: Jun 25, 2007
  Messages: 6,416
  Likes Received: 67
  Trophy Points: 145
  ...duuuuh!! Pole sana Shy, ingelikuwa bora kweli kama ungelijua mapema.
   
 10. Buswelu

  Buswelu JF-Expert Member

  #10
  Oct 23, 2008
  Joined: Aug 16, 2007
  Messages: 1,989
  Likes Received: 42
  Trophy Points: 145
  Waliokuwa wanajiuza bar maid na wengine wengi...huwa wanatulia sana wakiolewa...kwani wengi wao wanafanya kazi hizo kwa influence ya kukosa pesa na maisha magumu....except ambao wanafanya bila kuja,kuwa na makundi mabaya etc.

  Nina mshikaji wangu..mke aliye nae alikwa bar maid early 90's kwenye bar jirani wakati nikiwa kid.Kwa sasa ni mama mwenye watoto watatu katulia,wenye afya akili na kimwili..wanasoma pazuri...bwana ni engineer wa kutegemewa...

  Harafu advantage ya hao wakiamua kutuliwa wanatulia kweli....so ni choice yako ukiona anakufaaa kamata weka ndani.....
   
 11. Yona F. Maro

  Yona F. Maro R I P

  #11
  Oct 23, 2008
  Joined: Nov 2, 2006
  Messages: 4,237
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 0
  buswelu lakini this is information age utakubali mwanamke wako ambaye alikuwa anajiuza aje kusababisha uangushwe katika mambo fulani huko mbeleni sifa yake mbaya ije kuwa ndio chachu ya kuondoa vitumbua vyako ??
   
 12. Steve Dii

  Steve Dii JF-Expert Member

  #12
  Oct 23, 2008
  Joined: Jun 25, 2007
  Messages: 6,416
  Likes Received: 67
  Trophy Points: 145
  Shy, perception matters siyo?!
   
 13. Yona F. Maro

  Yona F. Maro R I P

  #13
  Oct 23, 2008
  Joined: Nov 2, 2006
  Messages: 4,237
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 0
  yes kweli kabisa -- mimi naangalia huko mbeleni itakuwaje jamii itakuchukuliaje kama ukiamua kusahau ya historia , mfano mzuri tunaona wakina palin wanavyoteswa na vijimambo vya vya enzi hizo
   
 14. Mbu

  Mbu JF-Expert Member

  #14
  Oct 23, 2008
  Joined: Jan 11, 2007
  Messages: 12,729
  Likes Received: 187
  Trophy Points: 160
  ...SteveD, 'ukimchungua sana kuku haliki!', ...ni bora mnapoamua kuishi pamoja basi mfungue tu ukurasa mpya, mambo ya kuangalia aliyevunja mlango nani mnhhh... wengine roho zetu tukipaliwa tu zinatoka, yataka moyo!
   
 15. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #15
  Oct 23, 2008
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,572
  Likes Received: 82,101
  Trophy Points: 280
  Mla mla leo, mla jana kala nini? :). Ukimpekuapekua sana kuku utashindwa kumla :)
  Mtaanza kuuliza na yule jamaa mlikuwa mnafanya style gani? Chuma mboga au mbwa kachoka? Halafu ukishaambiwa unaingia mitini kwa sababu zile njemba nyingine zilishaingia uwanjani kwa style zote hizo :) Inafaa mtafute bikira ;)
   
 16. Buswelu

  Buswelu JF-Expert Member

  #16
  Oct 23, 2008
  Joined: Aug 16, 2007
  Messages: 1,989
  Likes Received: 42
  Trophy Points: 145
  Ha haha hivi bado wapo kweli duniani..?bubu kasema kweli.....uffss.(l)
   
 17. M

  Mama JF-Expert Member

  #17
  Oct 23, 2008
  Joined: Mar 24, 2008
  Messages: 2,858
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 0

  wapo lakini ni underage! rika lenu ni wa kubahatisha au hakuna. Vipi wawepo ilhali mnataka kutest kwanza kabla hajachukua kitu kizima kizima?
   
 18. Buswelu

  Buswelu JF-Expert Member

  #18
  Oct 23, 2008
  Joined: Aug 16, 2007
  Messages: 1,989
  Likes Received: 42
  Trophy Points: 145
  Ha ha ha mama.....trust me or not nimekutana nae akiwa bikra mwaka wa pili chuo kikuu...namqoute "leo tarehe .... nimekupa mwili wangu..ukiwa hujaguswa...ili uniamini" uffs....siku naamini...ila leo mtu akiniambia..kuwa kakutana na wa hivyo ukubwani naamini...ila usiniulize ni vipi niliweza tofautisha ya kichina na kweli...kwa kuwa na za kichina zipo.

  Unaweza pata penzi feki la kichina.

  Good night
   
 19. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #19
  Oct 23, 2008
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,572
  Likes Received: 82,101
  Trophy Points: 280
  Bado wako lakini inabidi uende kwa mganga kuwapata ;). Juzi nilimuona mzungu (mmarekani) kisura kweli kweli alikuwa anauza ya kwake to the highest bidder. Sikufuatilia kujua nani aliinunua kwa bei mbaya :)
   
 20. Domo Kaya

  Domo Kaya JF-Expert Member

  #20
  Oct 23, 2008
  Joined: May 29, 2007
  Messages: 530
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Mimi Sijali ili mradi hafanyi hivyo akiwa na mimi, tulivyoanza mahusiano tulichora mstari, ya nyuma yabaki kuwa ya nyuma na yambele ndio haswa ninayoyaangalia.

  " Aliyekula mwaka jana kala mwaka jana, na anayekula mwaka huu ndio mlaji"

  Na waswahili wanasema ukimchunguza sana bata hutamla. hivyo basi jali nini mpenzi wako anafanya sasa hivi tangu alivyokuwa na wewe na kuendelea.
   
Loading...