Kwa moto huu wa Magufuli, CHADEMA kama kampuni ya Samsung, Lowassa Samsung galaxy note 7

Halafu mambo ya msingi hawayaoni wamebaki kubwabwaja yasiyo na maana.
Uchumi umenyauka kama mchicha usio pata maji wao sawa, mikopo ya wanafunzi ni mgogoro mkubwa unanyemelea taifa wao hawaelewi, ajira za Vijana hakuna wala mpango wa kuwawezesha haupo yanaona poa tuu, mkulu anasema kafurahi madereva wa malori wanakosa kazi eti alikuwa na ugomvi nao yenyewe yanachekelea tuu.
Kweli ile tafiti ya watu wanne ingefanyika pale Lumumba matokeo yangekuwa tofauti. Kila penye wanne wawili ni mataahira
Una huruma sana kuhusu hayo matokeo. Haufai kufanya utafiti maeneo ya Lumumba wewe. Sio kwa michango na posti zao humu!
 
Kampuni ya Simu za Mkononi ya Samsung yenye makao yake makuu katika mji wa SAMSUNG nchini Korea kusini ilijizolea sifa sana kwa utengenezaji wa simu nzuri sana na kufikia hatua hata ya kuua soko la Makampuni kama ya Motorola, Nokia na Apple.

Hivi karibuni Kampuni hiyo ilijinasibu kuwa tolea lake jipya la simu aina ya SAMSUNG GALAXY NOTE 7 kuwa aina hiyo ya simu ilikuwa salama licha ya kulalamikiwa mara kadhaa kuwa ilikuwa na matatizo.
Lakini simu hiyo inadaiwa kushika moto ikiwa mikononi mwa abiria ambaye alikuwa kwenye shirika la ndege la Southwest Airlines nchini Marekani, hiyo ikiwa ni mara pili kwa aina hiyo ya simu kulipuka kwa moto.
Kufuatia Matukio hayo mawili, Kamapuni ya SamSung Wamekiri kuwa simu hiyo ina matatizo ya Betri na tayari wameshaiondoa sokoni.

CHADEMA(KAMPUNI YA SAMSUNG) wenye sifa ya kutengeneza wagombea urais kutoka nje ya CHAMA hususan kutoka CCM, walipata umaarufu sana walipompata Dk. Wilbroad Slaa ambaye kwa kweli alitoa ushindani mkali kabla na baada ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2010.
Aidha walijinasibu sana na mgombea wao mwingine kutoka CCM, EDWARD LOWASSA(SAMSUNG GALAXY NOTE 7) kuwa ni chaguo sahihi licha kulalamikiwa(kama ambavyo sumsung galaxy note 7 ilivyolalamikiwa) kuwa hana sifa ya kuwa rais hasa ukizingatia mazingira ambayo nchi ilikuwa nayo ya Rushwa, Ufisadi, Uzembe Kazini, Watumishi hewa n.k, malalamiko yaliyotokana na ukweli kwamba LOWASSA(SamSung Galaxy note 7) ni mmoja wa watu waliolifikisha taifa katika mazingira hayo.

MOTO wa rais Dk. John Pombe Magufuli kushughulikia Ufisadi, rushwa, Uzembe katika ofisi za Umma, Watumishi hewa n.k hakika LOWASSA ndani ya CHADEMA ni sawa na SamSung Galaxy Notem7. CHADEMA wamekosa dira kwa sababu hoja yao ya kupiga vita Ufisadi imekwisha. Hoja ya UFISADI imekwisha kwa sababu ya mambo mawili, mosi ni kukiri kwao kuwa Rais anashughulika na ilani yao ambalo ni jambo jema kukiri kuwa kilio chao cha siku nyingi sasa rais anakishughulia lakini PILI na amabalo ni muhimu ni kiendelea kwao kumkumbatia mtu ambaye walitembea nchi nzima kutangana tena wakisema wana USHAHIDI wa UFISADI wake, LOWASSA(SAMSUNG GALAXY NOTE 7). Mbaya kabisa(narudia ! Mbaya kabisa) wakiamini NDIYE tegemeo lao kwenye uchaguzi wa 2020. WASUBIRI SAMSUNG GALAXY NOTE 7 kulipuka kabla ya 2020.
hahahahahaha @TatamaMadiba umeua kabisa. Lowasa ni betri ndani ya SamSung Galaxy Note 7 (chadema) hivyo ilisharipuka 2015 na sasa itaripuka tena 2020, hahah chama mfu kweli ni sawa na bure
 
Hata mkiambiwa na mtu kama mzee Mwinyi kuwa nchi inaenda kama gari bovu mnabisha kwani mnaishi Tanzania kweli wenzetu?
 
Back
Top Bottom