Kwa mnaotaka kuoa / kuolewa 2017 michango ya harusi mtanunia watu wengi sana.. michango watu hatutoi

MKATA KIU

JF-Expert Member
Nov 22, 2010
3,191
7,320
habari wadau..

ni vizuri tukakumbushana wapendwa wetu hasa wenye jukumu la kuoa au kuolewa karibuni kwamba wajipange wenyewe vizuri..

watu michango hatuna ya kuwachangia..

magufuli amebana na anazidi kubana kila siku bora jana..

maana kumekuwa na tabia mtu usipomchangia harusi yake anakununia kama ugomvi... sasa mwaka 2017 mtanunia wengi sana maana hali tete
 
Naunga Mkono hoja kwa kweli harusi zinatughalimu sana na mara nyingi zinafanyika Mikoa ya mbali wala hatushiriki huko. Wastage of Money...Tutaonana wabaya jamani...............
 
Usipotoa ww watoa wengine lkn jua usiposhiriki shughuli ya mtu na yeye pia ata kua mzito kwako afu hata kama umeshaoa kuna watoto wako uko haya mambo hayaishagi
Unakua unajiekea social capital mwenyw
 
sio kama sitaki kushiriki.. ila nitashiriki kwa aina nyingine zaidi ya michango...

nipo tayari kutoa mchango wa mawazo Ila sio wa kifedha maana hali mbaya..




Usipotoa ww watoa wengine lkn jua usiposhiriki shughuli ya mtu na yeye pia ata kua mzito kwako afu hata kama umeshaoa kuna watoto wako uko haya mambo hayaishagi
Unakua unajiekea social capital mwenyw
 
Harusi saizi ni janga.Kuna mmoja kaja kulalama eti sijampa hata ya kuandaa kadi.Wakati anaandaa hakunijulisha.
 
ishu sio kuchanga, ishu ni kulipa fadhila, kama ulishaoa au kuolewa means ulichangiwa, sasa unakwepaje? kama upo single ni rahisi kukwepa, ila siku ikifika zamu yako utajua kachumbari ni mboga
 
Hii mambo ya kuchangiana wakati wa kuoa na kuolewa mimi inaniboa sana.

Namshukuru Mungu kwamba binafsi wakati naoa niliandaa kila kitu mwenyewe na nikaalika watu na sherehe ilipigwa kanisani kiingilio bureeeeeeeee! Aise nakuhakikishia hata mil 2 ni kubwa kwa chakula maana watu walikula na kusaza. Hii ndio maana ya sherehe yangu
 
Nadhani one of my new year ni kupunguza michango ya harusi. Kutochangia kabisa haitowezekana.
 
Back
Top Bottom