Kwa mnaoenda baa baada ya kupata kinywaji jitahidi kurudi nyumbani

Dr Kingu

Senior Member
Jun 13, 2011
154
43
Habari zenu wana jf. Katika hali isiyo ya kawaida baba mmoja amejikuta anasota wodini masaa 36 hapa hospitali ya mkoa morogoro akiwa na majeraha yasiyoshonwa na hana dawa. Mtu huyu ambaye alikuwa na mazoea ya kwenda baa kunya na kulala baa hata siku mbili alipata mkasa huu juzi baada ya kutokea vurugu kt baa na yeye kupigwa na kuporwa simu yake. Wasamalia wema wakamleta hapa hospitali akiwa hana hela wala ndugu hawana taarifa. Kwa vile jamaa ana mazoea ya kulala baa mke, watoto na ndugu hawakumtafuta. kama mnavyojua hospitali haina dawa na nyuzi za kushonea jamaa akaandikiwa dawa na vifaa vya kushoea majeraha akapewa karatasi akanunue, na yeye hana hela. Daktari karudi kwake mara tatu ila amshone majeraha na yeye akawa hana vifaa. Baada ya kuulizia ndugu zake wako wapi akajibu hawajafika hospitali na hawana taarifa. Kisha akajieleza kuwa ana mazoea ya kulala baa hivyo ndugu wanajua yupo baa akaomba wasamalia wema wamsaidie vifaa na dawa. Uzuri kuna chakula cha hospitali kilikuwa kinamsaidia hasijedondoka kwa njaa. Hivyo kwa wale waliozoea kulala baa ni vizuri warudi nyumbani baada ya kunywa wasije pata tatizo ndugu hawamtafuti wanajua ni tabia yake.
 

KALYOVATIPI

JF-Expert Member
Aug 11, 2011
1,414
196
we dokta kingu si una duka la madawa pale buguruni msaidie kama upo tayari anika namba yako ya m pesa wakuu tukusaidie kwani si cutgut au suture na tinture,?
 

Kisima

JF-Expert Member
Oct 8, 2010
3,856
3,652
Habari zenu wana jf. Katika hali isiyo ya kawaida baba mmoja amejikuta anasota wodini masaa 36 hapa hospitali ya mkoa morogoro akiwa na majeraha yasiyoshonwa na hana dawa. Mtu huyu ambaye alikuwa na mazoea ya kwenda baa KUNYA na kulala baa hata siku mbili alipata mkasa huu juzi baada ya kutokea vurugu kt baa na yeye kupigwa na kuporwa simu yake. Wasamalia wema wakamleta hapa hospitali akiwa hana hela wala ndugu hawana taarifa. Kwa vile jamaa ana mazoea ya kulala baa mke, watoto na ndugu hawakumtafuta. kama mnavyojua hospitali haina dawa na nyuzi za kushonea jamaa akaandikiwa dawa na vifaa vya kushoea majeraha akapewa karatasi akanunue, na yeye hana hela. Daktari karudi kwake mara tatu ila amshone majeraha na yeye akawa hana vifaa. Baada ya kuulizia ndugu zake wako wapi akajibu hawajafika hospitali na hawana taarifa. Kisha akajieleza kuwa ana mazoea ya kulala baa hivyo ndugu wanajua yupo baa akaomba wasamalia wema wamsaidie vifaa na dawa. Uzuri kuna chakula cha hospitali kilikuwa kinamsaidia hasijedondoka kwa njaa. Hivyo kwa wale waliozoea kulala baa ni vizuri warudi nyumbani baada ya kunywa wasije pata tatizo ndugu hawamtafuti wanajua ni tabia yake.

Ulichoandika hakieleweki kiuharisia!
Umesema jamaa alikuwa ANAKUNYA na kulala baa inamaana ndo makazi yake hayo! So cha msingi walitakiwa wamrudshe bar ndo kwake huko.
 
0 Reactions
Reply
Top Bottom