Nkoyi Pasikali,Wanabodi,
Declaration of Interest
Naomba ku declare interest kuwa mimi sina chama, namfahamu Lissu na kumkubali sana tuu, pia na sympathize yeye kwa kilichompata, ila ninachofanya hapa ni being objective. Pia nafahamu fika kinachotokea kila ukifanya ukosoaji wa Chadema au viongozi wao wanaowaabudia, hivyo wale wa kutukana, be free to do so, the truth will always be the truth and will stand up to the end.
Hili ni bandiko la swali, "Kwa Mliomsikia Tundu Lissu Kwenye Hard Talk, Jee Unadhani Atarejea Nchini?. Mimi kwa upande wangu, I seriously doubt kama atarejea, na ikitokea kweli akarejea, then Tundu Lissu atakuwa ni shujaa mwenye ushujaa mkubwa kuliko hata ushujaa wa Nelson Mandela!.
Nimesema hivyo kwa sababu nimemsiliza kwa makini Tundu Lissu. him being a Lawyer, kwa yale aliyoyasema, kwa tuhuma alizoshusha bila ushahidi, I seriously doubt if Tundu Lissu will ever return home during this era, na ikitokea kweli akarejea, then Tundu Lissu atakuwa ni shujaa kuliko Nelson Mandela, kwa sababu Mandela alirejea kuendeleza mapambano bila kujua nini kitampata, na alipofungwa jela na kusurvive hadi kuja kuja kuwa rais wa SA, hakujua, lakini Lissu, being a lawyer, anajua kabisa huwezi kutuhumu na kutaja majina ya watu bila ushahidi, hivyo ukirejea nchini, anajua fika akikanyaga tuu ardhi ya Bongo, atapokelewa na nani, na anajua atafikia wapi, and kwa situation hii tulionayo sasa, with vitu kama polonium 210, I doubt kama he will be so lucky kama Mandela.
Hivyo huu ni wito kwa watu wa karibu na Lissu, mshauri tuu aendelee na matibabu, hata mwili ukipona kabisa, aendelee tuu na matibabu ya kisaikolojia, ila aandike barua kwa Spika kuelezea kuwa bado anaendelea na matibabu, na kabla hajarejea, atumie international fora, kujihakikia akirejea, hata pokelewa na wale mimi ninaodhania ndio watampokea na hata fikia kule mimi ninakodhania atafikia.
Waliomshambulia Lissu ni watu wasiojulikana, hivyo nilishauri humu
Tuacheni Ramli Chonganishi: Tusihukumu, Tusije Tukahukumiwa!. "Karma Ndio Pekee Hutoa Hukumu ya Haki Hapa Duniani!. - JamiiForums
Pia nikawatambulisha aina mbili za wasiojulikana
Shambulio la Lissu: Wajue Wasiojulikana Watakaojulikana na 'Wasiojulikana' Ambao Kamwe, Hawatajulikana!. - JamiiForums
Nikauliza
WanaJF, Je tuisaidie Serikali yetu inaposhindwa au tusubiri ishindwe, tuibeze na kuizomea kuwa haiwezi? - JamiiForums
Mwisho nikasema waandishi wenye uwezo wa IJ, wanaweza kumsaidia Kamanda Siro kuwabaini wasiojulikana hawa, na mimi ni miongoni mwa waandishi wa IJ,
Serious Media inaweza kuwabaini "wasiojulikana" Deo Masakilija - JamiiForums
My Take.
The Hard Talk kwa Lissu was a waste, Chadema inabidi ianzishe kitengo cha International Politics kuwafunda makada wa Chadema, wakipata international foras, waseme nini in terms of International politics. That was a great opportunity kwa Lissu kuongea as a president in waiting na sio kuongea kama mwana harakati mwanzo mwisho. Hakupaswa kutoa tuhuma zisizo na ushahidi, pia hakupaswa kuponda mwanzo mwisho as if Magufuli is all that evil, and is doing nothing good for this country.
Kwa upande wa lingua, kiukweli Lissu ana flow, kwenye top 5 wetu, mtu pekee mwenye uwezo wa kuflow kivile ni Mama Samia, na labda Majaliwa, tukishuka chini zaidi kwa mawaziri, MFA na January they are good. Kwa upinzani, ikitokea mtu kama Zitto akakaribishwa Hard Talk kiukweli mtaona the difference, nawashauri Wapinzani the man to bank on ni Zitto, kwa sababu Lissu kaharibu, unless awe kaharibu makusudi ili akirejea apokelewe kule so that they can make big noises!.
Paskali
Rejea za Ushauri wangu kwa Tundu Lissu na Chadema
Swali la Morality: Je ni lazima kuusema kila ukweli unaousikia au tutangulize mbele maslahi ya Taifa? - JamiiForums
Mhe. Tundu Lissu, Please Acha Kumsulubu Spika Wetu!, Unammaliza Kabisa Hadi Ameshindwa Kazi!. - JamiiForums
CHADEMA Chama cha Ajabu Sana!.Kwenda Mahakamani Kwa Non Issue, Serious Issue ya Katiba ni UKUTA!. - JamiiForums
Hoja ya Udikteta wa Magufuli: Tundu Lissu isn't Right. Haupingwi kwa kupaza sauti kupiga tu Kelele! - JamiiForums
Vurugu za Bungeni: Mhe.Tundu Lissu, Anastahili Adhabu Kali?!. Ni Mtundu Toka Shule!. - JamiiForums
Ushauri kwa CHADEMA: Japo ni Haki, lakini chondechonde Msiandamane. Mwenye Nguvu Mpishe! - JamiiForums
Katiba: CHADEMA mlikosea! Kubalini yaishe, Tusonge mbele! - JamiiForums
Nakubaliana na wewe kwa kutokubaliana kutokana na hoja zako.
Yes, kwa mtizamo wako nakubaliana na wewe 100% kuwa umeanalys na kuja na hayo majibu kutokana na hiyo interview.
Mimi nitakuwa na maoni kama ifuatavyo,
1. Lissu ni opposition, hata kama asingekuwa ameshambuliwa isingewezekana apate platform halafu aanze kusifia chama tawala, hata siku moja halitawezekana na kamwe HAIWEZEKANI. Ntakupa na mfano kabisa, Mh Mwita Waitara alikuwa opposition majuzi nafikiri ulikuwa ukisikia alichokuwa akiongea those days, kwa sasa yuko "Njia kuu" unamsikia miziki anayoimba. Hata mkuu wa kaya, ulishawahi kumsikia akisifia upande wa pili? Rais wa jiji la bongo huwa unamsikia? So kwa hapo nakukatalia maana hata wewe huwezi kwenda kwa msichana(Enzi zako) na ukamsifia jamaa anaefukuzia the same msichana unamfukuzia.
2. Lissu ni Lawyer personally sina doubt kuwa anachokiongea hana ushahidi nacho. Kuna mwanasheria mmoja alituhumiwa sana hapa Tanzania,kelele zikapigwa sana na yeye akiwa kimyaaaa, alivyochoka na nyongo kumjaa aliongea sentensi moja tu " I'm not such a fool to sign without cover" mpaka leo hajawahi hata kuitwa kwenye ile mahakama kubwa ilianzishwa kwa lengo la kuwaswekelea mbali MAFISADI.... Palikali wa ngw'iswe, ogopa sana hawa jamaa waliosoma somo linaitwa Law halafu wakapasi mitihani kwenye shule yao inaitwa "Law School". Kama wewe ni mwalimu kama mimi,yakupasa kufikilia mara mbili mbili ili kumrushia kombora, matokeo yake utakuwa kama raisi wa jiji,alijikuta anarusha makombora ya kujishambulia mwenyewe na familia yake.
3. Tukiacha uana siasa,harakati na hicho ulichokisema u "president in waiting" , Lisu ni binadamu wa kawaida kama mimi na wewe, anaumia,anakasirika na anafurahi pia. Kitendo alichofanyiwa na hao watesi wake (Ambao hawajulikani) hakimfurahisha na kamwe hatakisahau maishani mwake, hakika anapopata nafasi ya kuongea na watu lazima atatoa kila alichonacho moyoni kwa maana ya dunia ielewe ni nini kilitokea(Kitu ambacho naamini hata wewe Pasikali ungefanya). Ubinadamu hawezi kumtoka vile tu sababu anahisi anweza kugombea uraisi. Lisu si malaika, bado ni mwanadamu wa kawaida hivyo alichokifanya ni ktimiliza uanadamu.
4. Nahitimisha kwa kukuambia, huo ushahidi mimi na wewe hatujui lakini je,wajua kuwa Lisu hajui au anaujua kilichotokea siku hiyo?
Naamini mimi na wewe hatuwezi kulijibu hilo bali yeye mwenyewe anauwezo nalo na kwa mantiki hiyo,mimi na wewe hatuwezi kuwa mahakimu wa kuhukumu kesi ya Lisu kuwa kaongea vitu pasipo ushahidi.
Namala ng'wichane ong'wa Mayala.