Kwa mliokutana na haya wakati wa ku-apply kazi tukutane hapa

AlphaMale

JF-Expert Member
Oct 26, 2019
613
1,401
Yani waajiri sijui kwann wanafanya hivi, sijui ni unyanyasaji, roho mbaya au maringo, utakuta mtu umeapply kazi, unaambiwa uje kwenye interview saa tatu asubuhi au saa mbili asubuhi, kwa kuheshimu muda unafika hiyo hiyo saa mbili asubuhi, basi utakalishwa kwenye kiti kwa masaa hata matatu, wao wanataka uwahi ila wao hawaheshimu muda wako.
 
Ndio mambo yetu ya kiafrika hayo. Sharti kunyenyekea. Lakini hiyo yote ni choyo tu!!
 
Mbona mahakamani kwenye samansi wanasema uwahi saa 2 ahsubuhi lakini shauri linawezwa endeshwa saa 7 mchana,we jamaa inaonekana mlalamishi sana,hilo nalo ni jambo la kulalamika,ungepata sababu ya kucheleweshwa kutoka kwao angalau ndio ungekuja tuijadili
 
mbona hata mchepuko unauambia ufike lodge chumba na 13 saa7 mchana unakuja SAA 11 unakomea kimoja tu
 
Yani waajiri sijui kwann wanafanya hivi, sijui ni unyanyasaji, roho mbaya au maringo, utakuta mtu umeapply kazi, unaambiwa uje kwenye interview saa tatu asubuhi au saa mbili asubuhi, kwa kuheshimu muda unafika hiyo hiyo saa mbili asubuhi, basi utakalishwa kwenye kiti kwa masaa hata matatu, wao wanataka uwahi ila wao hawaheshimu muda wako.
Uende jeshini ndio utakoma.Kukalishwa pia Ni sehemu ya interview .Zinawekwa kamera kucheki uvumilivu zinarekodi kila kitu.Waweza kosa kazi hapo tu ulipokaa.
 
Yani waajiri sijui kwann wanafanya hivi, sijui ni unyanyasaji, roho mbaya au maringo, utakuta mtu umeapply kazi, unaambiwa uje kwenye interview saa tatu asubuhi au saa mbili asubuhi, kwa kuheshimu muda unafika hiyo hiyo saa mbili asubuhi, basi utakalishwa kwenye kiti kwa masaa hata matatu, wao wanataka uwahi ila wao hawaheshimu muda wako.
Interview wanaheshimu muda wao sio wa kwako.
 
Hiyo nayo ni sehemu ya interview, unalialia vitu vidogo kama hivyo kwenye kutafuta kazi
 
inategemea na taasisi kama hizi za serikalini muda wala sio kipaumbele.jitu linafika saa tatu hapo hapo linakwambia njaa inauma

nenda kwa kaburu uone Muda anavyoufanya lulu.
 
Yani waajiri sijui kwann wanafanya hivi, sijui ni unyanyasaji, roho mbaya au maringo, utakuta mtu umeapply kazi, unaambiwa uje kwenye interview saa tatu asubuhi au saa mbili asubuhi, kwa kuheshimu muda unafika hiyo hiyo saa mbili asubuhi, basi utakalishwa kwenye kiti kwa masaa hata matatu, wao wanataka uwahi ila wao hawaheshimu muda wako.
Wewe wamekuweka masaa matatu tu unalalamika!!
Nakumbuka niliitwa kwenye interview niliambiwa itaanza saa 3:00 asubuh basi kijana mimi na njaa zangu mida ya saa 1 asubuhi nimeshafika baada ya muda kidogo wenzangu nao wakafika tulikua takribani watu 12

Lakini cha kushangaza interview ilianza saa 9 alasiri
 
Back
Top Bottom