Kwa mkoa wa Morogoro Wilaya gani nzuri kwa kilimo na ufugaji?

MWAMUNU

JF-Expert Member
Dec 17, 2011
856
494
Habari za mda huu wana jamvi,

Naomba msaada kwenye tuta.Kuna rafiki yangu ni Mwalimu yupo wilayani Newala katika mkoa wa Mtwara.

Kutokana na sababu zilizo nje ya uwezo wake anatakiwa kuhama kikazi, na katika Mikoa aliyoichagua kuhamia ni mkoa wa Morogoro.

Jamaa yangu anaomba kujua kwa Morogoro ahamie wilaya gani ndo nzuri, maana anataka nje ya kazi yake ya ualimu pia ajihusishe na masuala ya ufugaji na kilimo biashara.

Natanguliza shukrani, pia povu ruksa!
 
Na hasa ukizingatia mimi sinaga mambo ya wivu,haya hebu tiririka basi !!
 
Aende Moro vijijini huko mkuyuni...etc..akalime mpunga na wasukuma na ufuta..usije mjini...walimu wengi wa mjini esp wa secondary wameleralx hatari😛😛! Kukopa na wao wao nakukopa😛😛!( Msinipopoe huo ndo ukweli...
Walimu wa shule za msingi wengi ni wachakarikaji balaa Ila secondary sijui wanajikuta matawii
 
Aende Moro vijijini huko mkuyuni...etc..akalime mpunga na wasukuma na ufuta..usije mjini...walimu wengi wa mjini esp wa secondary wameleralx hatari! Kukopa na wao wao nakukopa!( Msinipopoe huo ndo ukweli...
Walimu wa shule za msingi wengi ni wachakarikaji balaa Ila secondary sijui wanajikuta matawii
Asante kwa mawazo, noted !!
 
Umeongea kitu kikubwa sana! Kwa upande wangu i have already learnt from my past mistakes through pains and depressions,am no longer me!
Ni kweli now days ni watu wachache sana unaeza mshirikisha mipango yako asikuangushe
Haya karibu na wewe uchangie uzi.
 
Changamoto ya kujiandaa nayo huko ni wafugaji tu hasa wamasai.

BTW:Kwa nini wilaya ya Ulanga haizungumziwi sana hata kwenye media tofauti na wilaya zingine zote za Morogoro?

Hakuna fursa za kilimo huko kama kwingine au?
 
Vipi kuhusu huduma zingine za kijamii kama maji umeme afya
nk??

Sent from my Infinix X650 using JamiiForums mobile app
Zahanati ipo, umeme upo kwenye suala la maji sina hakika nalo sana kutokana na muda niliokaa pale niliishi lodge maji nilipoyahitaji nilipata sasa sina hakika sana, Ila ni makao mapya ya wilaya kwa hiyo vitu vingi vipo kwenye hatua za kuendelea nadhani umenielewa mkuu.
 
Unataka umeme shambani wa nini ?
Unataka maji mashambani kwanini usichimbe kisima tu ?

Afya nakusupport
Nadhani hujanielewa , mshikaji wangu ni teachear so sehemu atayo hamia kwa vyovyote lazima kuwe na huduma za kijamii. Ikimbukwe yeye ni mtumishi wa serikali so masuala ya kilimo ni ziada tuu.

Sent from my Infinix X650 using JamiiForums mobile app
 
Huku hakufai huku
Kwa ushauri wangu aende ifakara Kuna sehemu panaitwa mbingu pale hawezi jutia maisha Bei chee misosi yA kutosha pia mashamba na ufugaji inalipa Kuna njia ya treni na barabara kwaio biashara inaend po a kabisa wanalima mpunga ,cocoa na mazao yote
Nilimshauri hivyo kutokana na rafiki zangu waliowekeza huko kwenye kilimo na wamefanikiwa, hata mbingu ni sehemu nzuri pia.
 
Changamoto ya kujiandaa nayo huko ni wafugaji tu hasa wamasai.

BTW:Kwa nini wilaya ya Ulanga haizungumziwi sana hata kwenye media tofauti na wilaya zingine zote za Morogoro?

Hakuna fursa za kilimo huko kama kwingine au?
Ulanga kuzuri sana, ila mbali na barabara mbaya kuna adha ya usafiri, na ukiachana na hayo yote, wafugaji wa huko ni wasumbufu mno!

Hata Kilombero sugar wanakoma na hao wafugaji.

Everyday is Saturday............................. :cool:
 
Back
Top Bottom