Kwa miswada hii Mitatu ya madini na maliasili, Prof. Palamagamba Kabudi umetisha!

Wapinzani waache kupinga kila kitu...ni muda muafaka wa kuweka inputs....hatuwezi kusubiri


!
!
Hii mikataba wanajua zaidi [HASHTAG]#sisiem[/HASHTAG]. Wanajua walichokifanya huko nyuma. Unataka tumaini walizingua kwa bahati mbaya? No, makusudically
 
Lissu ni mzuri katika kelele za kisiasa lakini kwenye masuala ya kisheria hana huo uwezo unaosema.

Kesi ya Zitto kufukuzwa CHADEMA aligonga mwamba.

Kesi ya kikatiba ya Mbowe kuitwa na Mkuu wa Mkoa na Kamanda wa Polisi katika kituo cha polisi amegonga mwamba.

Kesi ya kufanya mikutano ya kisiasa bila kibali cha polisi amegonga mwamba.

Hata kesi ya kina Bulaya na Mdee kuhusu adhabu walizopewa bungeni atagonga mwamba.

Kumbuka huu mswada umeandikwa na watu ambao hawana maslahi binafsi.

Miswada ya nyuma ilikuwa inaletwa huku ikiwa na hidden sinister motives

Kwa chuki na wivu huu lazima kuna kitu kibaya alishawahi kukufanyia huyu jamaa. Maana katika kila post yako hasira zako na jitihada za ku-undermine uwezo na michango ya akina Lissu and the likes huwa uko dhahiri.
In a nutshell, kwa mtu mwenye fikra na mawazo huru hawezi hata siku moja kukuchukulia serious...
It is the just the old same routine Lumumba asshole! That's all!
 
Inawezekana ikawa mizuri sana tatizo wanaojadili wanaielewa?

Kwanza lugha yenyewe ni ya malkia na wapo waheshimiwa wale waliohesabu vyumba 7 pekee na wengine wakabahatisha mpaka vile 4 ingawaje matokeo hayana tofauti na Daudi.

Pili, muda uliowekwa kuijadili unaonekana kuwa ni mdogo, katika sheria kila sentensi ina maana yake, tafsiri yake. Je kwa muda huo wataweza kuijadili kwa mapana yake.

Tatu, kuna hoja ya ubinafsi wa kivyama na huu ndio uliotugharimu mpaka leo, ni wabunge hawa hawa wa chama kile kile waliopitisha sheria za ajabu na waliruka na kushangilia, leo wanaletewa kitu kingine wataruka na kushangilia, hata kesho wakipelekewa mwingine wataruka na kushangilia. Wanatakiwa wapeane elimu ndani ya Bunge, waweke maslahi ya taifa kwanza halafu chama baadae.

Pamoja na hayo yote, tutakua hatujafanya kitu kama bado tutaendelea na katiba hii ya kifalme. Mfalme anapokosea hakuna wa kumgusa hata kama enzi yake imepita. Jambo la msingi tunapaswa kulipigania watanzania wote ni KATIBA MPYA hii ndiyo itakata mzizi wa fitina na kuleta heshima ya kiti.

Tunahitaji viongozi na sio watawala.
 
Wana Simba tutulie. Tulikuwa tunafikiri tunapambana na Yanga kwenye usajili kumbe tulikuwa tunapambana na Sirikali na mugulu muchemba. Tatizo Niyonzima. Aveva na Kaburu Mungu atawapigania.
 
Miswada ya kingleza.... wachangiaji ndo akina KKK. hao hao ndo walipitisha hiyo miswada ya kupeleka makinikia nje tena kwa hati za dharura....... tutegemee jipya kweli??
 
Lissu ni mzuri katika kelele za kisiasa lakini kwenye masuala ya kisheria hana huo uwezo unaosema.

Kesi ya Zitto kufukuzwa CHADEMA aligonga mwamba.

Kesi ya kikatiba ya Mbowe kuitwa na Mkuu wa Mkoa na Kamanda wa Polisi katika kituo cha polisi amegonga mwamba.

Kesi ya kufanya mikutano ya kisiasa bila kibali cha polisi amegonga mwamba.

Hata kesi ya kina Bulaya na Mdee kuhusu adhabu walizopewa bungeni atagonga mwamba.

Kumbuka huu mswada umeandikwa na watu ambao hawana maslahi binafsi.

Miswada ya nyuma ilikuwa inaletwa huku ikiwa na hidden sinister motives
Zitto bwana huwa unamchukia Sana lissu pole Sana
 
Lugha iliyotumika niya malikia

Jamani kigezo cha KKK katika siasa kiboreshwe maana wengine hapo wasioweza kunyamaza ndio watachangia kwa kukejeli,kutukana na kuzomea.

Niwakati wa meza kupigwa tena hasa na wale wasiokua na uelewa wa mambo hayo mazito
 
Kuna mswada wa Medical, Dental and Allied Healthscience

Mswada huu umelenga katika ku 'regulate' shughuli za wataalam wa afya

Nimeupenda kwasababu allied health science ni sehemu muhimu ya watoa huduma
Kwa bahati mbaya kwavile hawana usajili na hakuna mechanism ya kuwa regulate huduma zimetolewa na watu tu wa mitaani.

Mtu kasoma kozi ya siku 7 ya Red cross anaitwa Allied Health sciences

Pamoja na hayo mswada umelenga kulinda masilahi ya wataalam, kuzuia wanaotoka kusikojulikana kuja kufanya kazi za afya nchini kama Wataalam, na hapa ni Madaktari

Tatizo katika mswada ni pale unapotaja 'Tanzania mainland tu'

Ningependa wabunge wajadili nafasi ya Zanzibar.

Huko kuna vyuo na kwavile sisi ni ''JM'' Wznz watavuka na vyeti pengine kutoka katika vyuo visivyokuwepo na kudai ni sehemu ya JMT

Ningependekeza Wznz wanaosoma vyuo ZNZ na kwavile wana bodi zao kama ilivyo Uganda na Kenya, wakija Mainland Tanzania wapewe hadhi ya 'foreign' kama vyuo vina viwango, au wasitambuliwe kabisa kama wamesoma vyuo visivyo na viwango

Hili litasaidia kulinda afya za 'Mainland Tanzania' kwa kupitia mgongo JMT

Mswada umelenga 'mainland Tanzania' siasa za Muungano ziwekwe kando.
Tunalinda afya za Mainland kwanza
 
Miongoni Mwa Janga la Taifa hili Ni pale Watu wenye Akili Wanaposhindwa kuzitumia na Kuamua kumkabidhi Mtu azitumie

ZIDUM FIKRA ZA TUNDU..................

Bado enzi za mwalim hazijesha ktk vichwa vya Wabongo
Shida yetu ni kushangilia mawazo ya mtu mmoja. Tusubiri hiyi miswada ipite kwa dharura halafu tuone matokeo yake, tukishindwa tuwe wapole tu Tanzania inaendeshwa bila usukani
 
Naunga Mkono Hoja.
Miswada hii ikipita hivi hivi ilivyo, na kama itakuwa applicable retro respectively kwa mikataba tayari iliyopo, then Tanzania tutakuwa tumevunja mikataba yote ya uwekezaji kwenue maliasili zetu, hakuna cha IICD wala MIGA, mambo yote ni Sheria za Tanzania!, huu ndio uzalendo, huu ndio uanamume, na kama hawataki, wafungashe, wakwende zao!.

Paskali

...huwa nakuelewa sana maandishi yako!
 
Hiyo lugha iliyotumika kwenye hiyo Miswada Sipati Picha kwa Musukuma na Lusinde Kama watatoboa

Tatizo kubwa la hii MISWADA ni migumu kutafisirika kwa Kiswahili na hivyo ikiwa kwenye vyombo vya sheria inatafisiriwa kwa namna ambapo kiinglish kinamaanisha hapo ndipo shughuli ipo.Wakisema 'Original Document" maana yake wanaenda kwenye ile ya KIINGLISH.Sasa tofauti ya neno moja kila kitu pinduliwa.

Sasa wenzangu na mie tuliyoishia darasa la 'KKK' tu tunaishia kupiga makofi hatutaki kujadili wala kuweka hadharani ili watanzania wengine waijadili kuona manufaa yake.Mwisho wa siku itapewa SPika akiamua.Hahahhahahahah
 
Miswaada inaletwa kwa hati ya dharula ili ijadiliwe faster......., au wabunge wapitishe kama ilivyo? Tuombe mungu iwe mizuri.
Kina msigwa ndo waijadili? Alafu jaribu kuelewa kinachokusudiwa ni ili kuwapa hao wabunge nguvu waliokuwa wanaitaka!!
 
Binafsi sijaona kipya, bali naona kiza kilichojificha.

Kwa nini hiyo miswaada isiwe straight kwa maana ya kusema kabisa, 50/50 ya mrahaba unapokuja kuchimba madini yetu, pia tukaambiwa kabisa na adhabu ya moja kwa moja kwa mtu atakayelitia hasara taifa kwenye mikataba..

Mbona muswaada haujasema effect ya huo muswaada utakuwaje kwa wale wanaochimba kabla ya sheria mpya??,,

Ukumbuke pia hata waliotengeneza sheria zilizopita ni wasomi waliobobea tena wengine ni wa havard, bunge hili hili ndio lilisema ndiooo na mambo yakaenda hovyo, vipi tunauhakika gani na weledi wa hili bunge katika kujadili hii miswaada??.

Bado tunamahitaji mengi kwenye sheria zetu na katiba yetu ili kufikia malengo, zimamoto haiwezi kutatua matatizo ya kisheria na katiba...
 
CCM ni wakuangaliwa kwa makini la sivyo unaweza ukapelekwa Chaka hakuna kitu wanachokiandaa wakaacha kukisifia,baadae utaanza kuwasikia kuwa tumeibiwa kwa kupitia kitu kilekile walichokiandaa wenyewe na ambacho walitahadharishwa kuwa hakifai
 
Aise.Salute kwako Mheshimiwa Rais.Tatizo kubwa limekuwa ni kwenye hizo Arbitral Tribunals ambazo Lissu amekuwa akirejea mara kwa mara.Kama tukiweza kudhibiti choice of laws kwa foreigners itatusaidia sana.Tatizo kubwa je,uwezo wa mahakakam zetu uko vizuri?,jE,tuna wabobezi katika maeneo haya?
 
Naunga Mkono Hoja.
Miswada hii ikipita hivi hivi ilivyo, na kama itakuwa applicable retro respectively kwa mikataba tayari iliyopo, then Tanzania tutakuwa tumevunja mikataba yote ya uwekezaji kwenue maliasili zetu, hakuna cha IICD wala MIGA, mambo yote ni Sheria za Tanzania!, huu ndio uzalendo, huu ndio uanamume, na kama hawataki, wafungashe, wakwende zao!.

Paskali
"Miswada hii ikipita hivi hivi ilivyo"......Wala hakuna haja ya kujadiliwa! Hiki ndicho unachomaanisha, mkuu?
 
Back
Top Bottom