Kwa miswada hii Mitatu ya madini na maliasili, Prof. Palamagamba Kabudi umetisha!

Rais Magufuli ninakupongeza wewe na wale wote waliokushauri ili kumteua Prof. Kabudi katika nafasi ya Waziri wa Katiba na Sheria.

Prof. Kabudi na timu yake ya wanasheria wameanza kutoa matunda yao mema kwa taifa kupitia kazi zao kama zilivyobainika kwenye miswada hii.

Kwa miswada hii iliyopelekwa bungeni ili kujadiliwa na kuwa sheria haina maneno mengi lakini yaliyopo yamejaa umuhimu mkubwa kisheria kwa maslahi ya taifa, sina shaka kwa kiwango kikubwa taifa litakuwa limeingia katika ukurasa mpya katika safari ya kulinda maliasili zake ili zinufaishe taifa kwa kizazi hiki na kijacho.

Kama Rais Magufuli alivyosema, ‘’tulichelewa lakini kama taifa tumeamua kufika’’ na kwa miswada hii ninatumaini tutafika.

Yaliyopo katika miswada hii ya sheria ni pamoja na;

>>Bunge kupitia mikataba yote ya maliasili za nchi kuangalia maslahi ya Watanzania na baada ya kubaini masharti hasi katika mikataba hiyo Bunge linaweza kuitaka Serikali kufanya majadiliano upya na upande wa pili wa mkataba ili kuondoa masharti hayo.

>>Kuweka utaratibu wa bunge kufanya mapitio na maridhiano ya mikataba.

>>Kufanya mapitio madaraka ya Waziri na Kamishna wa madini.

>>Kuimarisha mifumo ya uthibiti na uwajibikaji katika sekta ya madini na petrol.

>>Kupanua wigo wa ukusanyaji wa mapato kwenye sekta ya madini na petrol.

Kwa wale wanataka kuisoma hiyo miswada Gonga hapa;
LINK>>Miswada ya marekebisho ya sheria za maliasili

Hizi ni baadhi ya contents zilizoko kwenye miswada.
View attachment 532776
View attachment 532777
Ulimpongeza lkn leo spika analia na mikataba.
 
unga Mkono Hoja.
Miswada hii ikipita hivi hivi ilivyo, na kama itakuwa applicable retro respectively kwa mikataba tayari iliyopo, then Tanzania tutakuwa tumevunja mikataba yote ya uwekezaji kwenue maliasili zetu, hakuna cha IICD wala MIGA, mambo yote ni Sheria za Tanzania!, huu ndio uzalendo, huu ndio uanamume, na kama hawataki, wafungashe, wakwende zao
Hii retro-respecective itawezekana?
 
Hii retro-respecective itawezekana?
Kitakachofanyika ni re negotiations na kukubali kuivunja mikataba iliyopo amicably na kuingia mikataba mipya kwa sheria mpya. Accacia wameishakubali, hivyo itavunjwa na kuundwa kampuni mpya kwa sheria mpya.

P
 
kweli JF ukiandika kitu uwe makini sana yaani watu hadi kupongeza walipongeza na kuna mdau alimtolea uvivu tundu lisu leo nahisi na yeye analia kama mzee wa Parliament
 
Kitakachofanyika ni re negotiations na kukubali kuivunja mikataba iliyopo amicably na kuingia mikataba mipya kwa sheria mpya. Accacia wameishakubali, hivyo itavunjwa na kuundwa kampuni mpya kwa sheria mpya.

P
Welcome again I hope uko na afya njema wengine tukadhani umejiteka au ulikuwa maganzo ukivuna mahindi.
 
Back
Top Bottom