Kwa miaka 61, chama chenye maarifa mengi (CCM), kimeshindwa kutatua tatizo la maji na umeme!

Salary Slip

JF-Expert Member
Apr 3, 2012
46,888
143,985
Sisemi mengi.

Hivi inakuingia akilini kuwa CCM ni chama chenye maarifa mengi kama kwa miaka 61 sasa watanzania wanakabiliwa na shida ya maji na umeme wakati nchi imezungukwa na mito, maziwa na hata bahari?

Yaani watu walioshindwa kutumia maji ya maziwa (mfano ziwa victoria) katika kupambana na tatizo la maji kwa miaka 61 ndio wana maarifa mengi?

Watu ambao kwa miaka 61 wanaongelea megawatts wakati nchi ina vyanzo vingi tu vya nishati ya umeme ndio wana maarifa mengi?!

Watu ambao kwa miaka karibu 30 sasa wameshindwa kupambana na upinzani kwa hoja ndio wana maarifa mengi?!

Watu ambao nchi ina misitu ya kila aina ila watoto wanakaa chini kwa kukosa madawati ndio nchi inayoongozwa na chama chenye maarifa mengi?

Nchi inayoongozwa na chama chenye maarifa mengi kwa miaka 61 sasa bado kinaanda Bajeti inayotegemea huruma ya wahisani?!

Anyway, yako mengi ila huenda maarifa anayoongelea ni yale ya kuiba kura na kuvuruga chaguzi zetu.

kikwete.PNG
 
Kikwete amewadanganya wenzake, halafu hayo maarifa ni ya wizi wa kishamba wa kura unaovuja hata kabla haujatendeka?
 
Umeme?!

Mbona umeenda mbali sana...

Hata changamoto ya vyoo kwenye mashule wameshindwa kuimaliza...

Hata changamoto ya madawati wameshindwa kuimaliza...

Usikute huko vijijini wakati mwingine Walimu wanakosa hata chaki...
 
2 Reactions
Reply
Back
Top Bottom