Kwa Mhe. Waziri Mkuu Mizengo Pinda: Kitenisi kingine hicho, pangua! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kwa Mhe. Waziri Mkuu Mizengo Pinda: Kitenisi kingine hicho, pangua!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by so who, Jun 18, 2012.

 1. so who

  so who Member

  #1
  Jun 18, 2012
  Joined: Oct 28, 2011
  Messages: 73
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  LEO BUNGENI NIMEONA KITENISI KINGINE KIMEELEKEZWA KWENYE OFISI YA WAZIRI MKUU NAMNUKUU MHESHIMIWA ZITTO KABWE (mb) WAZIRI KIVULI JE HAPA HII OFISI YA WAZIRI MKUU ITATUELEZA NINI KWENYE NCHI AMBAYO INAFUATA MFUMO WA FEDHA WA IFRS NA IPSAS KWA KITENNISI HIKI TUNAOMBAMAELEZO YA KINA MHESHIMIWA MTOTO WA MKUU LIMA LASIVYO KAULI YAKO YA KWAMBA UNAANZA SAFISHA SERIKSLI NA KASHFA UTAKUWA ULIKUWA UNATUPIGA MAGIRINI TU
  NAMNUKUU;

  Hitimisho
  Fedha za Rada Mheshimiwa Spika,
  Wakati Kamati za Bunge zilipokaa kujadili taarifa ya Serikali kuhusu Mfumo wa Mapato na Matumizi, Waziri wa Fedha na Uchumi alitoa Taarifa kuhusu Fedha za Rada zilizorejeshwa, jumla ya shilingi 72.3 bilioni ambazo zilipokelewa tarehe 26 Machi, 2012. Kwa mshtuko wa Wabunge, Waziri aliiambia Kamati kuwa mchakato wa manunuzi ya vitabu na madawati kwa kutumia fedha hizi ulikuwa umeanza chini ya Ofisi ya Waziri Mkuu TAMISEMI. Fedha hizi hazijawahi kupitishwa na Bunge lako tukufu.
  Kitendo cha Serikali kuzitumia kabla ya kupitishwa na Bunge ni kuvunja sheria za Fedha kuhusiana na masuala ya Bajeti. Wakati Waziri akiwasilisha Hotuba yake hakugusia kabisa suala la fedha zilizorejeshwa kutokana na Ununuzi wa Rada! Mheshimiwa Spika, Kambi ya upinzani inataka maelezo ya Serikali juu ya Fedha hizi na utaratibu wa kuzitumia.
  Kambi inataka kufahamu vigezo vilivyotumika kuteua mikoa ya Mwanza, Morogoro na Dar es Salaam kutumia fedha hizi. Kambi pia inapenda kufahamu Deni lililochukuliwa kununua Rada hii iliyoleta kashfa kubwa sana hapa nchini limefikia kiasi gani kulilipa na tukililipa tutakuwa tumelipa kiasi gani kwa ujumla.
   
 2. A

  Alfred Ngowi Member

  #2
  Jun 18, 2012
  Joined: Jan 8, 2012
  Messages: 50
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Sasa kila kitu bungeni akiwa anajibu waziri mkuu mawaziri wengine wanakazi gani?? Hio ni kazi ya waziri wa fedha ndugu. Ndio maana suala la madeni ya nje na kila kitu anahusika yeye. Waziri mkuu huja kuongeza tu kama kuna ulazima. Au la, subiri PM's question and answers time. Sijui kama unania ya kujibiwa na PM unadhani atakujibu hapa.
   
 3. t

  tpmazembe JF-Expert Member

  #3
  Jun 18, 2012
  Joined: Jan 5, 2012
  Messages: 2,474
  Likes Received: 39
  Trophy Points: 145
  kwa maelezo yao ni kuwa hizi pesa haziko tena hazina chini ya waziri wa fedha ,bali zilipokelewa zikapelekwa moja kwa moja TAMISEMI kwa waziri mkuu,ambaye wizara ya tamisemi na tawala za mikoa iko chini yake.NI SAWA KABISA KUULIZWA WAZIRI MKUU,
   
 4. A

  Alfred Ngowi Member

  #4
  Jun 18, 2012
  Joined: Jan 8, 2012
  Messages: 50
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  sasa ndugu tamisemi kuna waziri, na manaibu mawaziri wawili. Wote hao hawatoshi??? Bado afanye pm?? Ni sawa kweli? Tanzania itafika tunako taka iende kweli?? Kazi ya hao wote nini??? Kupanda vx na ac?? Namna hii mtamchosha pm na hataweza kufanya mambo ya maana kabisa kabisa. Kama ndivyo basi msubiri pm's q and a time maana ni wazi hawezi kuwajibu hapa.
   
 5. simtami

  simtami Member

  #5
  Jun 18, 2012
  Joined: Aug 22, 2011
  Messages: 28
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  wale ni mawaziri wa nchi ofisi ya waziri mkuu wanajibu kwa niaba ya waziri mkuu tu lakini swali linaelekezwa kwa WAZIRI MKUU ungejua hata raisi anaposhauriana na waziri mkuu uteuzi wa mawaziri huwa anamwonyesha wizara ambazo zitakuwa katika ofisi yake apendekeze nani atafanya nae kazi kwenye wizara zitakazokuwa ndani ya ofisi ya waziri mkuu hawa vile vile kwenye baraza la mawaziri linalokutana na RAISI ni waziri mkuu tu ndiye aneingia huko hawa jamaa wakimuuliza waziri mkuu ni sawa kabisa kwani hawa ni kama manaibu wake tu !
   
 6. simtami

  simtami Member

  #6
  Jun 18, 2012
  Joined: Aug 22, 2011
  Messages: 28
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Sasa kila kitu bungeni akiwa anajibu waziri mkuu mawaziri wengine wanakazi gani?? Hio ni kazi ya waziri wa fedha ndugu. Ndio maana suala la madeni ya nje na kila kitu anahusika yeye. Waziri mkuu huja kuongeza tu kama kuna ulazima. Au la, subiri PM's question and answers time. Sijui kama unania ya kujibiwa na PM unadhani atakujibu hapa.

  ofisi ya waziri mkuu
  iwe waziri wa nchi tamisemi au waziri wa nchi uratibu wa bunge majibu yao yanawakilisha waziri mkuu sawa tuombe majibu
   
 7. R

  RMA JF-Expert Member

  #7
  Jun 18, 2012
  Joined: Oct 10, 2010
  Messages: 409
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Waziri mkuu ndiye msimamizi wa shughuli za serikali bungeni!
   
 8. franksarry

  franksarry JF-Expert Member

  #8
  Jun 18, 2012
  Joined: Nov 9, 2009
  Messages: 1,107
  Likes Received: 229
  Trophy Points: 160

  Bana mwana JFs Ngowi, tusiwe wasemaji wa Hon PM...!, ni muhimu sana kwa PM kulijibu hilo swali, kwa kuwa Govt imepanga kuzitumia hiyo fedha ya Rada nje ya Utaratibu wa Matumizi ya Fedha za Govt.
   
 9. Pendael laizer

  Pendael laizer JF-Expert Member

  #9
  Jun 18, 2012
  Joined: Jan 14, 2012
  Messages: 961
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Sasa hizo billions of money ndio tuseme huyu mtoto wa mkulima amezitafuna manake haiwezekani akazielekeza katika matumizi kabla ya kupitishwa na bunge la jamhuri. CCM NI UWOZO MTUPU. TUPA KULE 2015 NA KUWASHTAKI HAWA MAFSADI WOTE.
   
Loading...