Kwa mhe. Rostam: Ahadi kwa familia ya danny mwakiteleko itekelezwe | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kwa mhe. Rostam: Ahadi kwa familia ya danny mwakiteleko itekelezwe

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by jongoo, Jul 29, 2011.

 1. j

  jongoo Member

  #1
  Jul 29, 2011
  Joined: Feb 10, 2010
  Messages: 17
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Wakati wa msiba wa Mwandishi Mwandamizi wa New Habari 2006 Ltd ilisikiaka ahadi iliyotolewa na mmiliki wa kampuni hiyo Mh. Rostam Aziz kwamba ataendelea kumlipa mke wa marehemu mshahara wa Danny kwa miaka mitano na pili atasomesha watoto wa Marehemu mpaka kufikia chuo Kikuu. Vyombo mbali mbali vya habari pia viliripoti jambo hili ambalo kama likitekelezwa ni zuri sana. Danny nilipata kufanya nae kazi kampuni mbili tofauti za habari alikuwa mwadilifu sana na nasikia hata kwa Rostam pia alikuwa nmwadilifu hivyo hastahili kuenziwa na ahadi hewa.

  WASIWASI wangu ni kwamba isije ikawa ni ahadi ya kisiasa na kutaka kujipatia umaarufu tu kama taasisi na watu wengine walivyokwisha kufanya. Wengi wamekuwa wakiingia mtini baada ya muda mfupi tu.

  Nasema nina WASIWASI kutokana na maelezo niliyoyapata kutoka kwa wafanyakazi wa kampuni hiyo ya magazeti walioshikwa na butwaa kwa ahidi hiyo kubwa.

  WASIWASI huo unajengeka katika mazingira yafuatayo:
  • Wafanyakazi hao wa New Habari hawajalipwa mishahara ya tangu mwezi Juni mpaka sasa huku wengi wakiwa na malimbikizo ya nyuma (naamini Danny pia kazikwa akidai)
  • Wafanyakazi waliofukuzwa au kuacha kazi kutolipwa stahili zao kwa muda mrefu sasa
  • Kama kampuni kuwa katika msukosuko wa kiuchumi.
  Hayo hapo juu Mhe. Rostam alishaahidi kuyafanyia kazi si mara mora moja lakini ahadi hizo zimekuwa hewa.

  Mwezi July unaisha jumapili, je Mke wa Danny akienda jumatatu tarehe moja anapewa hela

  Mhe. Rostam Aziz katika hili kusiwe na usanii. Kwa maeklezo toka kwa wafanyakazi pale msibani mshahara wa Danny kwa miaka mitano si chini ya 100M. Pia ikumbukwe ahadi ilitolewa hadharani hivyo hata ndugu waliofikiria kumsaidia mjane huyu wataacha kufanya hivyo akijua kuna hela inapatikana New Habari na watoto wanasomeshwa. Isifike mahali mjane huyu akifika tu ofisi za Mtanzania anakimbiwa na kuanza kuzungushwa.

  USHAURI:

  1. Ahadi alizotoa ziwekwe katika maandishi ili badiliko lolote la uongozi lisiathiri tamko
  2. Tanzania Editors Forum ambayo Danny alikuwa mwanachama hai mfuatilie kuhakikisha linatekelezwe kinyume cha hapo muujulishe umma kupitia vyombo vyenu.
  3. Maandishi yatakayowekwa yaeleze bayana kama fedha hizo atakuwa akitoa mfukoni mwake au kupitia New HABARI 2006 Ltd.
  Kama ahadi hii itatekelezeka mpaka mwisho Mhe. Rostam atakuwa mfano wa kuigwa.
   
 2. b

  buguruni Member

  #2
  Jul 29, 2011
  Joined: Feb 5, 2010
  Messages: 22
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  BINAFSI nasubiri kuona matokeo coz nasikia madeni kampuni inadaiwa ni mengiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiii na hajalipa. Kama movie vile!
   
 3. S

  Shangazi JF-Expert Member

  #3
  Aug 1, 2011
  Joined: Mar 24, 2009
  Messages: 307
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Naafikiana na wewe Jongoo.

  Hii inanikumbusha ahadi alizopewaga shangazi yangu kama hizo na baadae zikageuka kuwa hadithi na zimeishia hewani. I hope RA hataleta siasa.


  Aweke utalatibu ambao hata kama yuko abroad huku utekelezaji unaenderea smoothly.

   
 4. s

  sikiolakufa JF-Expert Member

  #4
  Aug 2, 2011
  Joined: Feb 1, 2010
  Messages: 411
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  ni kweli mama wa watu amepata pigo kubwa sana maishani....iwapo watamzungusha kwenye ahadi hiyo watakuwa wanafanya dhambi kubwa......
   
 5. Nyambala

  Nyambala JF-Expert Member

  #5
  Aug 2, 2011
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 4,470
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Rostam anahusikaje kwenye hiyo ahadi? Just curious..... Maana isije ikawa ahadi ilitolewa na kampuni/uongozi wa kampuni ambayo kesho ikifa au ikiuzwa inakuwa habari si habari!
   
 6. R

  Rubuye123 JF-Expert Member

  #6
  Aug 2, 2011
  Joined: Dec 18, 2009
  Messages: 1,443
  Likes Received: 472
  Trophy Points: 180
  R.A sio 'muheshimiwa' tena!
   
Loading...