Kwa mh. mbunge wa Ilemela

Koryo2

JF-Expert Member
Nov 28, 2016
2,056
2,515
Mhe. Mbunge wetu mpendwa unakumbuka kuwa tulikuchagua kwa kishindo ili baadaye upeleke matatizo yetu yafanyiwe kazi na kutuletea maendeleo. Mimi nijikite kwenye tatizo la barabara ya kutoka Buswelu Makao Makuu ya Wilaya mpaka barabara ya lami ya kwenda Musoma. Kutokana na Makao Makuu ya Wilaya ya Ilemela kuwa Buswelu sasa hivi magari yanayopita kwenye barabara hiyo ni takriban magari 1500 kwa siku. Mhe. zifuatazo ni adha tunayopata sisi wananchi tunaoishi kando kando ya barabara hii:-
  • Vumbi inayotimuliwa na magari yanayopita kwenye barabara hiyo kwa masaa 24.
  • Magonjwa yanayosababishwa na vumbi inayotimuliwa hasa ya kikohozi hasa watoto wetu.
  • Kelele inayosabbishwa na magari takriban 1500 yanayopita kila siku kwenye barabara hii.
  • Uchafu wa kila siku kwenye nyumba zetu, vyombo vyetu, nguo zetu, mashuka yetu nk.
  • Wenye biashara wanaoishi kando kando ya barabara hii kukimbiwa na wateja kutokana na vumbi zito linalotumuliwa na magari na hasa wenye nyumba za kulaza wageni.
  • Gharama kubwa ya maji tunayotumia kumwagilia maji ili kupunguza vumbi inayotimuliwa.
  • Hatari wanayopata watoto wetu wanaosoma kwenye shule zilizopo kando kando ya barabara hii kwa kugongwa na magari mfano shule ya msingi ya Gedeli.
Kutokana na sababu niizozieleza hapo tulikuomba barabara hii itengenezwe kwa kiwango cha lami lakini hadi leo hatuoni dalili yeyote ya kuanza kazi katika barabara hii. Ukumbuke Ubunge ni miaka mitano sisi bado tunakuamini lakini usije ukatulaumu pale tutakaposema HAPANA kama utakuja kutuomba tena Ubunge. Hapa tunakuombea uwe sasa Waziri Kamili lakini tunakuomba barabara hii itengenezwe kwa kiwango cha lami.

Naomba kuwasilisha.
 
nakweli hilo barabara linavumbi haswa tena usiombe ukapita na pikipiki vumbi litakalokuingia machoni utajuta kupita!
 
Jamani mbona hill vumbi lipo miaka yote na hamsemi? Na jinsi wakazi wa hapo mlivyoibana Barbara ndio hatari kabisa, Mimi nawashauri muuze hizo nyumba au pangisheni maana mapafu yenu baada ya miaka kumi hayana kazi.
 
Back
Top Bottom