Kwa mfumo huu wa TRA wengi tutafunga Biashara

Kosa ni waziri was fedha na mkubwa wake hawajawahi kufanya biashara
 
Habari wadau;
Ni hivi;Nilitembelewa na wakaguzi wa TRA ofisini kwangu.Walipofika walianza kuniuliza maswali mengi na nikawapa nyaraka zote walizotaka na kwa mujibu wa Taarifa zangu kodi yangu nilishalipa yaani sikuwa na deni.

Basi baada ya kuona niko safi wakaanza kuniuliza maswali ya kipuuzi.Moja wapo ilikuwa niwaonyeshe risiti ninazowapa wateja wanaponunua nikawapa wakajumlisha sana kisha wakasema mbona kodi unayolipa ni ndogo kuliko mapato yako?

Nikawatazama kwa jicho la dharau kisha nikiwauliza kivipi?Wakanipa maelezo mazuri sana.Nikiwaambia hivi kodi inatozwa kwenye faida au kwenye mapato wakasema kwenye faida basi nikawaulizambona hamjauliza taarifa za matumizi?Wakasema tupatie basi nikawapatia.

Katika matumizi ikaonekana kwa faida ninayopata basi hata kodi ninayolipa nikubwa hivi inabidi nipunguze kiwango cha kodi kwani kwa faida niliyopata ni kama vile tunagawana robo kwa 75.Yaani mimi nabaki na 25 wao wanakula 75% ya faida yangu.

Walipoona hivo wakaanza kukagua risiti zangu za matumizi,kwa kuwa mimi ni mjasiriamali na biashara yangu ni ya kuuza chakula kwa hiyo kiasi kikubwa cha manunuzi yangu hayana risiti kwa hiyo tulianza kubishana sana na hawa watu wakaweka kofuli kwenye ofisi yangu wakitaka niende TRA ofisini kwao.

Kiukweli kutokana na biashara kuwa ngumu na kwa kuwa kodi yangu inaisha mwisho wa mwezi wa pili niliwaambia sawa na walipomaliza kufunga usiku nimeita fundi welding nimevunja lile kofuli lao nimebeba materials zangu zote,kisha nimeenda polisi kufungua kesi kuwa nimevamiwa na majambazi wameiba kila kitu.na niko hapa TRA na RB yangu ya kuibiwa nawaona wanavojichnaganya tu kunitishia huku wakifikiri mimi sielewi ninachofanya.Yaani mfungie masufuria yanu,bakuli,majiko nakadhalika kwa sababu tu mnataka kunikamua.

Kakamueni wake zenu na kama mmechafukwa mnifunge basi ila kodi silipi tena huko ninakoenda naenda kufungua biashara bila kulipa kodi.Huu wizi wizi sitaki tena kufanyiwa nimechoka
Ulipaswa uende kwanza ukawasikilize ,ukiijua sheria ya kodi hapo ungewatoa knock out kabisaaa
 
Duuh aseee hii hali hata mimi inanikera sana yaaan kodi kubwaa kwa biashara ndogo tu na viongozi wetu ndo wapo mstari wa mbele kituambia tujiajiri alafu mambo yenyewe ndo haya yaan ni kero, kero.....
 
Niko mbion kufunga duka la vifaa vya ujenz, mwez 4 huu linasoma -ve tuu..ni use*nge mtup..hyo mashine ya efd ni changamoto,wanavyoidai utafkir walinikopesha..nmegoma,siinunui na nafunga biashara mwez ujao..au mwez huu,si ndo wanavotaka hiv wote turud kolomije..
 
jamaa walivyonichosha wameniambia nimlipie na mwenye Frem kodi alafu mimi nikamdai hiyo hela.
 
Kwamba TRA wamekua wakichukua 75% ya faida na wewe 25% ni uongo wa kishamba.

TRA wanaendelea kushinda kwa sababu tunajisndwa kuwapinga kwa hoja za kitaalam.
 
Huu ukenge huu, ndio unaharibu nchi!! Mie upande wa bodi ya mikopo labda waje na RPG wanilipue, silipi ng'ooo. Eti wameniewekea na faini, he he heeee! Wanifuate huku kwenye biashara yangu ya mchanga!!
Ivi hili deni bado wanatudai kumbe! Mie haaaaaaata sijawahi kupata hata maumivu ya kichwa kukumbuka hii insue napiga zangu mishe taratibu napata pesa ya kula! Baba alikuwa analipa kodi ilikuwa haki wanipe pesa ya kusomea chuo!
 
Kwakweli hali ni mbaya, huku kahama wateja wamelala mbele, maduka yamefubaa, mafrem yamegeuka magheto.

Munapovamia maduka nakuanza kutisha watu huko vijijini tafasiri ni mbaya na watu hawaji tena kununua bidhaa.

Kila mtaa unamtendaji wa mtaa kwanini msiwatumie kuratibu kodi? Serikali iajiri afisa biashara wa kata huyo awe pia wakala wa kodi, badala ya kujifanya mabaunsa wa kiganda mnapiga watu hadi kufa
 
Pale mwendakulima mama mmoja kashuswa kwenye bus eti anakilo nyingi bus litazidi mizani, huko ndo tumefika.
 
mimi nikienda dukan namwambia mwenye duka kabisa aandike bei ndogo.

Yani kama ni kitu cha laki moja namwambia aandike elfu ishirini.

Namkwamisha Magu kama yeye anavyonikwamisha
 
Kigongo ferry pantoni haifanyikazi masaa 24, ikifika saa mbili hakuna tena magari yanayovuka, tumebakiza kukusanya kodi kwenye mahindi na maharage.
 
Sasa wewe unakataa kwa sababu unajua au unakataa kwa sababu una wenge?Kama huelewi we nenda kakaange maandazi ule

Wewe umefanya biashara ambayo unawalipa TRA 75% ya faida yako, mwenye mawenge ni wewe! Eti huna rekodi za bei ya unga wa maandazi yako. Mali bila daftari!
 
Hiyo mashine ni kwaajili ya wateja wanaofanya mauzo/mtaji kuanzia 14M.
Wewe mbona mauzo yako ni kawaida tu?
Sasahivi wanalazimisha tu....kama una mauzo ya elfu 15 unalazimishwa kuchukua efd... Efd yenyewe inauzwa laki 7....efd wakati biashara Imeporomoka
 
Niko mbion kufunga duka la vifaa vya ujenz, mwez 4 huu linasoma -ve tuu..ni use*nge mtup..hyo mashine ya efd ni changamoto,wanavyoidai utafkir walinikopesha..nmegoma,siinunui na nafunga biashara mwez ujao..au mwez huu,si ndo wanavotaka hiv wote turud kolomije..
Game la biashara ya vifaa vya ujenzi imekuwa tight sana....competition nayo imekuwa kali sana competition in price and distribution plus gvt ya sasa na other cost no profit ....nimefunga hiyo biashara
 
jamaa walivyonichosha wameniambia nimlipie na mwenye Frem kodi alafu mimi nikamdai hiyo hela.
Unalipa Withholding tax huku mwenye nyumba amelipa kodi ya jengo hawezi kukurudishia
 
26 Reactions
Reply
Back
Top Bottom