Kwa mfanyao utafiti: Hivi 'Population diversity' ni nini hasa inapokuja jamii ya watu? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kwa mfanyao utafiti: Hivi 'Population diversity' ni nini hasa inapokuja jamii ya watu?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mzee Mwanakijiji, Apr 15, 2012.

 1. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #1
  Apr 15, 2012
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  Hili neno nimekutana nalo katika nyaraka fulani fulani za serikali na kwa kweli halijatafsiriwa vizuri. Nimekutana nalo pia katika mambo ya wanyama, na ikolojia. Lakini linapotumika kuhusu jamii au kundi fulani la watu linamaanisha nini hasa? Najua wapo ambao wamefanya tafiti mbalimbali na labda nao huwa wanaangalia hiki kitu kinachoitwa "population diversity' kuna mtu anaweza kutuelezea maana yake ni mifano yake kwa nchi kama ya kwetu?
   
 2. N

  NasDaz JF-Expert Member

  #2
  Apr 15, 2012
  Joined: May 6, 2009
  Messages: 11,308
  Likes Received: 1,653
  Trophy Points: 280
  Nami nasubiri kwa hamu, maana ake huwa nakutana nalosana hili neno mahali.....nazani majibu yatachelewa kwavile kwa hivi sasa wadau watakuwa kwa ulabu!
   
 3. Kobello

  Kobello JF-Expert Member

  #3
  Apr 15, 2012
  Joined: Feb 20, 2011
  Messages: 5,689
  Likes Received: 656
  Trophy Points: 280
  Google.... oops! sorry!
   
 4. FortJeasus

  FortJeasus JF-Expert Member

  #4
  Apr 16, 2012
  Joined: Jan 19, 2012
  Messages: 568
  Likes Received: 61
  Trophy Points: 45
  Population ni idadi ama kundi la viumbe hai wenye sifa zinazofanana wanaopatikana na /au kuishi katika eneo moja la kijiografia wakichangia resources mbalimbali kama vile maji, hewa na mwanga.Unaweza kuwa na population ya binadamu,(human population) , miti ya aina fulani (plant population), na kundi la nyoka (snake population)na kadhalika.
  Dhana ya Population Diversity kama itumikavyo katika taaluma ya Biography na katika eneo lake dogo la Biodiversity,humaanisha uwepo wa viumbe hai zaidi ya moja,wenye sifa na tabia tofauti,wanaopatikana katika eneo fulani la kijiografia.Unapokuwa na population ya simba ,nyati, ng'ombe,miti na binadamu katika eneo moja la kijiografia, hiyo kiikolojia tunaiita Population Diversity.
  Katika taaluma ya sosholojia ama anthropolojia,maana ya msingi inabaki kama ilivyoonyeshwa hapo juu:kwamba ni hali ya kuwa na mchanganyiko wa watu wa makabila mbalimbali,(different races and tribes),asili mbalimbali,(different origins) na rangi mbalimbali (divergent colour),na hata dini tofauti(different beliefs).
  Taifa la Marekani ,kwa mfano, lina population diversity ama diversed population kwa kuwa kuna watu wa makabila,asili,na rangi na dini mbalimbali.
  Tanzania nayo,kwa kiasi fulani, ina population diversity ingawa sio kwa kiwango cha Marekani.
   
 5. jponcian

  jponcian Member

  #5
  Apr 16, 2012
  Joined: Oct 2, 2011
  Messages: 67
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 15
  Mkuu unaweza kuongeza pia genetic diversity ya human population kwa mantiki kuwa unaweza ukawa na kundi la watu wa kabila moja au hata familia moja lakini bado wakatofautiana kwenye genetic makeup i.e. wafupi, wanene, weusi tii, maji ya kunde, n.k. Kwa ujumla dhana ya human population diversity inatumika ku-describe the varying nature of human population in terms of their physiognomy, race, ethnicity, genetic make-up, etc.
   
 6. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #6
  Apr 16, 2012
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  Ndio maana wengine huwa wanafeli hivi hivi! Mtu kaulizwa swali la historia anakuja na maelezo ya Bongo Flava!
   
Loading...