Kwa Mchezo mchafu unaosukwa, UKAWA wasishangae 2020 wakabakia na wabunge watatu (3)

Sijaona juhudi zozote za kitaalamu za Ukawa ku-declose mbinu zilizotumika kuwashinda. Leo Lowassa anasema, "yaliyopita si ndwele". Hovyo kabisa. Hivi tumeshindwa hata kutumia vijana wetu wa IT mfano kutambua nani alimpigia simu Jecha na mazungumzo yao? Mbona Kenya wameweza kumjua na kumdeclose mazungumzo ovu Kati ya Mkurugenzi wa Tume na Ikulu na kuweka hadharani tena kwa tv binafsi? Eti tuliibiwa kura kwa nini msianike wizi ulivyofanyika? Chadema kumejaa wasomi wajinga plus.
 
Mkuu
Achana na solution ya kwenda msituni hiyo siyo solution, labda useme maandamano nchi nzima nitakuelewa

Mkuu hiyo ya kuingia msituni sio poa kabisa lakini ukiangalia vyombo vya kusimamia huo uchaguzi wapinzani watakuwa wanapoteza muda wao tu. Huyu kiongozi wa sasa hajui wala haamini kushindwa kwa kura hata body language yake iko hivyo. Msituni kunaweza kugeuka kuwa njia sahihi japo hatarishi kwa usalama wa taifa letu.
 
Usione watu wako kimya ukadhani wameridhika. Kutesa kwa zamu wanasubiri muda uwadie ili wafanye maamuzi. Wanamezea tuu. kwa mwendo huu 2020 ccm out
 
CCM wamejipanga kuendelea kushika dola beyond 2020 hata kwa udhalimu. MaDC na maDED wote ni makada ambao si rahisi kwenda kinyume na mamlaka ya uteuzi. 2020 watatangaza ushindi wa CCM hata kwa kutumia udhalimu. Hata hiyo udhalimu una mwisho na siku zote ukweli na haki vitashinda hata kama ni kwa kuchelewa!
 
Sio hapa Nadhani unanielewa, Sio hapa! Akina Mbowe wanitafute na sio Najitia Kiburi hata na mimj nitawatafuta, Ila nilikuwa Disappointed kiasi wakati wa Uchaguzi 2015 walikuwa in their heads kiasi walikuwa wanaignore ushauri, basi nikajitosa kivyangu kupiga kampeni. Sio kwa Upenzi juu ya Lowassa as a person kwani niliamini Mabadiliko ya Kweli yasingeletwa na CCM. Hata wakati wa Kampeni simumshambulia Magu, Nilimpenda, au niseme sikumjua sawaswa ni baada ya Udictator wake ndio amenitoka kama kohozi, hulitafuti tena kulimeza!
Ushaona Fursa Unataka Kuitumia Kupata Pesa Ya Sikukuu Au Siyo ?
 
Usione watu wako kimya ukadhani wameridhika. Kutesa kwa zamu wanasubiri muda uwadie ili wafanye maamuzi. Wanamezea tuu. kwa mwendo huu 2020 ccm out
Mkuu ujue sio rahisi kabisa kuindoa ccm hasa pale juu
 
Ushaona Fursa Unataka Kuitumia Kupata Pesa Ya Sikukuu Au Siyo ?
Nope mimi nina mpunga wa kutosha, sema utakalo! Ni usiri wa solution yenyewe na sio kuwa nataka Kitu. Chadema hawana Uwezo wa Kuninunua mtu kama mimi my dear!
 
Nadani unaongea hvyo ukiwa huelewi hasaa hali kaskazini ilivyo.....chadema tumebaki kuongea na kulalamika hamna kazi wanayofanya mbunge yupo ndani mpaka sahv hamna lolote jipya linaloshikika mpaka leo pale mjini...
Kwaupande wa nasari atachaguliwa tu pale meru kwasababu ndo mmbunge pekee anaye fanya kazi inayoonekana naanapendwa sana....
Ni kama ilivyokuwa kwa kigoma na zito kabwe alihama naakashinda kwa kishindo...upinza ni wamejisahao kwa namna moja ama nyingine game limebadilika nawao wanatakiwa kubadilika kuendana na siasa ya sasa
Usilolijua usiku wa kiza. hivi Zito alishinda kawekwa?
 
Mkuu mleta mada mnamuonea sana bwana mdogo Nassari.
Kauli yake ya juzi wala haina tatizo...Ni kauli nzuri na ya kiungwana.Ndio maana hata wabunge wengine wa upinzani wanakiri kabisa kuwa hakuna mtu anaweza mpinga Rais JPM kwa yale mambo yanayoleta maendeleo kwa wote.Na hiki ndicho alichokisema Nassari...Utawezaje kumpinga mtu anayeleta maendeleo?Lkn sasa maendeleo na demokrasia/uhuru wa kujieleza yanaenda sambamba.Huo ndio msisitizo wa Josh Nassari.

Hilo suala la Wabunge wa UKAWA kurudi watatu bungeni...Mi naona kama watatu itakuwa wengi sana.Nafikiri 2020 Wabunge wa UKAWA wanaweza wasifike hata wawili tu wakuchaguliwa.Kwa sababu JPM ametengeneza "mpango kazi" wake matata sana.Hivi we unadhani Kayombo yule DED wa Ubungo ambaye ametokana na Shirikisho la Vyuo Vikuu-CCM anaweza kumtangaza Kubenea Ubungo na kuacha mbunge wa CCM?

Yaani kwa akili yako,hawa DED(ambao kisheria ndio Returning Officers) ambao kisheria ndio watangaza matokeo na kauli yao ndio hutangaza mshindi,watakubali kuwatangaza wabunge wa upinzani wakati na wao wote ni makada wa CCM??Sahau mkuu....2020 ni kishindo Kikuu!Kwa kuanzia na Lissu na Wabunge wote na madiwani wa Dsm....Jiji na Ikulu lazima iwe chini ya Chama
Mkuu mimi naelewa sana alichosema nasari.kwani kuna shida gani kusifu yale ya maendeleo kwa wananchi.

Shida kuna watu wanadhani kwamba ukiwa mpinzani lazima upinge kila jambo au kua ccm lazima ukubali kila kifanywacho na serikali.

Sent from my HUAWEI Y330-U11 using JamiiForums mobile app
 
mtoa post kama hawata kuelewa basi wasije kujilaum na kuanza kulialia kuwa wameibiwa kura il hal wametahazariwa mapema sana hata mwaka hauja isha,lkn pia kingunge pia kawapa ushaur mzr sana na wasipoufanyia kaz itakula kwao,upinzan weng wao n viongoz maslah kama akina nasary watu kama hawa sekunde 2 wako ccm bila kujua wamejengwa na kufahamika kuptia upinzan kama machal so wasipokuwa makn hawana chao 2020 kwan jamaa kasha panga safu ya ushnd ktk halmashaur zote,kunamambo upinzan umeingia woga,c mbowe yule wa zaman kukaa kimya kwa unyanyas huu,wote wamemwachia lisu na lema ambao kwa sasa yuko kwene kibano hapo hata msigwa amefyata mkia! kipnd cha kikwete hawakuwa hv wamekuwa wanamsha popo vjana walikuwa wanawaunga mko leo wako nyuma na vjana kuwaweka kama chambo haf bila msaada wowote!
 
Back
Top Bottom