Kwa Mchezo mchafu unaosukwa, UKAWA wasishangae 2020 wakabakia na wabunge watatu (3)

TL. Marandu

JF-Expert Member
Jul 12, 2015
3,627
2,000
Kwa jinsi Mazingira yanavyokwenda, na Mchezo mchafu sana Unaosukwa na Magufuli na CCM, hali sio nzuri kabisa kwa UKAWA 2020.

Kuna wanaoshauri UKAWA wasusie Uchaguzi 2020 Kama hakuna katiba mpya na tume mpya ya Uchaguzi, hilo likitokea CCM wataona ninsherehe, Kadhalika bado UKAWA wakishiriki Uchaguzi bado kwa CCM ni sherehe!

Mtego mkubwa uliopo ni kuwa Wabunge wengi Siasa ubunge kwao ni sehemu ya ajira. Hata tume na katiba ikiwa mbovu kiasi gani, Ili mradi kuna uwezekano wa wao kushinda ubunge, ukiwakataza kugombea Ubunge watakimbilia CCM wapo wachache majasiri, lakini wasaliti kama Joshua Nasari watakimbilia CCM kwa Speed ya supper sonic.

Pia huo ni mtego mbaya sana kwani tumeona CCM ni kama mafisi wasiojali kula kiungo cha mnyama ambaye bado anatembea au nyama ya mzoga ambao umeoza kiasi cha kutoa usaha! kugomea uchaguzi kwao itakuwa ni sherehe na njia ya mkato ya kuiua CHADEMA. Na kwa CHADEMA kushiriki Uchaguzi Kutakuwa ni Mhururi wa Kuwasafishia CCM ushindi haramu wa urais ambao sina shaka watajitangazia hata kama kura za Urais watapata tano. Mfano halisi ni Zanzibar. Hata hivyo kama CHADEMA hawako tayari kufanya mambo kadhaa muhimu, ninaona ni bora washiriki uchaguzi hivyo hivyo. Lakini pia hofu mbaya zaidi ni kuwa Rais Magufuli kwa kukataza mikutano na akaona no body pushed away hard enough, msishangae bila aibu 2020 akalazimisha wagombea wa CCM watangazwe washindi majimbo ya upinzani hata kama mpizani ameshinda kwa asilimia 98 na yule wa CCM asilimia 2.

If a man will swim with crocodiles and they do nothing, he will be used of it! CCM na Rais Magufuli wameget away na uhuni mwingi, kunyanganya Komputer za UKAWA 2015 kimya, kufuta matokeo ya Zanzibar, kimya, kukataza mikutano ya vyama kimya, kumsindikiza na Polisi Lipumba kuvunja Ofisi za CUF, kimya. Tutashuhudia vituko 2020. Ni kwamba CCM uchaguzi mkuu hauna maana tena! Wao wameshaona wanaweza kufanya uhuni wowote kimacho macho na wasifanywe kitu na mtu yeyote.

I just want to warn Chadema/Ukawa this issue is no longer a laughing matter anymore, something deliberate and precise has to be done fast!

Mimi nina suluhisho la uhuni huu, bila shuruti CCM wenyewe wataomba iwepo Katiba mpya na Tume mpya ya uchaguzi, nitawatafuta UKAWA- CHADEMA only once, wakipuuza thats it. Baada ya hapo wanitafute wao au 2020 wabakie na Wabunge watatu (3)

Kuna wanaosema Ati wataaminije Kama CCM hawajanituma. Ni bora nife kuliko Kutumwa na yeyote hasa ikiwa ni CCM, Mimi ni Natural Leader ambaye sijawahi, siwahi wala sitawahi Kujipaka Mkorogo Kisiasa, As far as I am concerned what U see is what you get!
 
TL. Marandu

JF-Expert Member
Jul 12, 2015
3,627
2,000
Tupe suluhisho tafadhali.
Sio hapa Nadhani unanielewa, Sio hapa! Akina Mbowe wanitafute na sio Najitia Kiburi hata na mimj nitawatafuta, Ila nilikuwa Disappointed kiasi wakati wa Uchaguzi 2015 walikuwa in their heads kiasi walikuwa wanaignore ushauri, basi nikajitosa kivyangu kupiga kampeni. Sio kwa Upenzi juu ya Lowassa as a person kwani niliamini Mabadiliko ya Kweli yasingeletwa na CCM. Hata wakati wa Kampeni simumshambulia Magu, Nilimpenda, au niseme sikumjua sawaswa ni baada ya Udictator wake ndio amenitoka kama kohozi, hulitafuti tena kulimeza!
 
TL. Marandu

JF-Expert Member
Jul 12, 2015
3,627
2,000
Nasari akihamia CCM watu watachague hata mbunge kutoka vyama vidogo vidogo kuliko kumchagua mgombea wa CCM.
Watanzania wengi ni Ushabiki ujue! Hawatafakari kwa kina, Utashangaa watamchagua tu, But the hell I don,t care for that Dogo!
 
barafu

JF-Expert Member
Apr 28, 2013
6,680
2,000
Mkuu mleta mada mnamuonea sana bwana mdogo Nassari.
Kauli yake ya juzi wala haina tatizo...Ni kauli nzuri na ya kiungwana.Ndio maana hata wabunge wengine wa upinzani wanakiri kabisa kuwa hakuna mtu anaweza mpinga Rais JPM kwa yale mambo yanayoleta maendeleo kwa wote.Na hiki ndicho alichokisema Nassari...Utawezaje kumpinga mtu anayeleta maendeleo?Lkn sasa maendeleo na demokrasia/uhuru wa kujieleza yanaenda sambamba.Huo ndio msisitizo wa Josh Nassari.

Hilo suala la Wabunge wa UKAWA kurudi watatu bungeni...Mi naona kama watatu itakuwa wengi sana.Nafikiri 2020 Wabunge wa UKAWA wanaweza wasifike hata wawili tu wakuchaguliwa.Kwa sababu JPM ametengeneza "mpango kazi" wake matata sana.Hivi we unadhani Kayombo yule DED wa Ubungo ambaye ametokana na Shirikisho la Vyuo Vikuu-CCM anaweza kumtangaza Kubenea Ubungo na kuacha mbunge wa CCM?

Yaani kwa akili yako,hawa DED(ambao kisheria ndio Returning Officers) ambao kisheria ndio watangaza matokeo na kauli yao ndio hutangaza mshindi,watakubali kuwatangaza wabunge wa upinzani wakati na wao wote ni makada wa CCM??Sahau mkuu....2020 ni kishindo Kikuu!Kwa kuanzia na Lissu na Wabunge wote na madiwani wa Dsm....Jiji na Ikulu lazima iwe chini ya Chama
 
Jaribu kupiga Picha Mbowe awaombe Wabunge wa Chadema waugomee uchaguzi wa 2020 halafu nipe list ya watakaokubaliana naye na Kubakia Chadema, nami nitakuonyesha Nassari Katika list mojawapo.
 
TL. Marandu

JF-Expert Member
Jul 12, 2015
3,627
2,000
Achana na solution ya kwenda msituni hiyo siyo solution, labda useme maandamano nchi nzima nitakuelewa
Nope hiyo watawaua, Ukuta walishindwa ndio iwe msituni? Huko siko, Na hapo ndio Kiburi cha CCM wanajua wa Kuweza hilo hayupo, Na mimi pia nadhani anayewaza hilo ni Mwenda wazimu. My Br.Do not try to read my mind! Kuna mengi ya Kuchangia hapa hilo la Solution yangu niachie mimi na Ukawa, Kama una Mawazo au solution nyingine, waweza Kuchangia. Na solution yangu sio main discussions hapa!
 
Sep 27, 2015
17
45
Nasari akihamia CCM watu watachague hata mbunge kutoka vyama vidogo vidogo kuliko kumchagua mgombea wa CCM.
Nadani unaongea hvyo ukiwa huelewi hasaa hali kaskazini ilivyo.....chadema tumebaki kuongea na kulalamika hamna kazi wanayofanya mbunge yupo ndani mpaka sahv hamna lolote jipya linaloshikika mpaka leo pale mjini...
Kwaupande wa nasari atachaguliwa tu pale meru kwasababu ndo mmbunge pekee anaye fanya kazi inayoonekana naanapendwa sana....
Ni kama ilivyokuwa kwa kigoma na zito kabwe alihama naakashinda kwa kishindo...upinza ni wamejisahao kwa namna moja ama nyingine game limebadilika nawao wanatakiwa kubadilika kuendana na siasa ya sasa
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom