Kwa Mbunge wangu Mnyika - Lisemee Tatizo Hili | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kwa Mbunge wangu Mnyika - Lisemee Tatizo Hili

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Tiba, Jun 24, 2012.

 1. Tiba

  Tiba JF-Expert Member

  #1
  Jun 24, 2012
  Joined: Jul 15, 2008
  Messages: 4,511
  Likes Received: 95
  Trophy Points: 145
  Mbunge wangu Mnyika,

  Naomba nitangulie kujitambulisha kwamba mimi ni mmoja wa wapiga kura wako, na ninafurahi kwamba kura yangu haikupotea bure. Mimi ni mkazi wa jimbo la Ubungo katika eneo linaloitwa Malamba Mawili, kule Mbezi. Miaka zaidi ya minne iliyopita, wakati Lowassa akiwa Waziri mkuu, ulianzishwa mradi wa maji na huu mradi ulikuwa ukisimamiwa na wachina.

  Wote tulio kuwa tunahitaji maji tuliandikisha majina yetu, vipimo vilichukuliwa, tuliambiwa kiasi cha kulipa kama gharama ya kutandika mabomba na kuuunganishiwa maji. Tulioweza tulilipa na mabomba yalifungwa mpaka kwenye nyumba zetu pamoja na mita za maji. Sehemu zilizohusika ni mitaa ya kwa Osama, Bulicheka Recreation Centre, Msikitini na pale Makuti.

  Kwa ujumla tulifurahi sana kwamba sasa tutaondokana na tatizo la maji kabisa, tatizo ambalo limekuwepo miaka nenda rudi. Cha ajabu mpaka leo, hatujawahi kuona hata tone moja la maji lilitoka. DAWASCO wanatuletea bill ingawaje hizo bili hazidai chochote.

  Kwa kuwa bunge linaendelea sasa, naomba ufuatilie kujua ni kwanini pesa zetu na serikali pia zilitumika vibaya kwa kutandika mabomba ya maji ambayo leo ni karibu miaka 5 bado hayatoi maji!!! Kwa nini pesa hii haikutumika kufanya shughuli nyingine za maendeleo badala ya kuzizika tu? Tulipolipia gharama za kuunganishiwa maji, si kwamba tulikuwa tuna pesa zisizo na kazi, la asha. Tulifanya hivyo kwa kujua kwamba hilo tatizo la maji sasa ingekuwa ni historia. Kwa sasa tunanunua lita 1,000 za maji kwa kati ya Tshs. 10,000 na Tshs. 15,000 kulingana na msimu.

  Nimefurahi kuona kwamba kwenye taarifa yako kwa umma kuhusu suala la kutolewa nje ya bunge, umegusia suala la kuongeza uwezo wa mtambo wa Ruvu na ujenzi wa Bwawa ambavyo vikifanyika uenda tatizo la maji kwa maeneo yetu ikawa historia.

  Nimeamua kutumia njia hii kukufikishia ujumbe kwa kuwa sikujua ni vipi ningeweza kukutana na wewe na siku ulipofanya mikutano kule kwetu bahati mbaya mimi sikuwepo. Lakini pia najua wewe ni mwanachama wa JF hivyo nina imani ujumbe huu utakufikia.

  Tafadhali tuisadie kumaliza tatizo la maji kwenye eneo letu.

  Tiba
   
 2. Kimbunga

  Kimbunga Platinum Member

  #2
  Jun 24, 2012
  Joined: Oct 4, 2007
  Messages: 13,012
  Likes Received: 1,817
  Trophy Points: 280
  Mabomba ya wachina ni kilio kwa wananchi wa kimara. Kuna sehemu mambomba yapo ardhini lakini hakuna maji. Kuna mengine yanatoa maji kwa zamu ila maji hayafiki majumbani unayakuta yamelowesha barabara. Sijui zile bajaj za DAWASCO zinafanya kazi gani? Halafu eti DAWASA wanajenga miundombinu halafu DAWASCO wanasambaza. Mimi sijaona ufanisi wowote hapa.
   
 3. Tiba

  Tiba JF-Expert Member

  #3
  Jun 25, 2012
  Joined: Jul 15, 2008
  Messages: 4,511
  Likes Received: 95
  Trophy Points: 145
  Mkuu nashukuru kwamba na wewe umeliona hilo. Nasikitikia hiyo pesa iliyotumika sijui ilikuwa ya serikali au ya wafadhili lakini kwa ujumla haya ni matumizi mabaya sana ya resources. Mnyika amuulize waziri wa maji ni lini tutarajie maji kupatikana katika maeneo yetu.

  Tiba
   
 4. N

  Njoka Ereguu JF-Expert Member

  #4
  Jun 25, 2012
  Joined: Apr 7, 2012
  Messages: 822
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 35
  Kuna haja ya kukagua nyumba za wafanyakazi wa DAWASCO kubaini kama katika nyumba zao maji yanatoka ili kuwabana vizuri. Haiwezekani miradi mikubwa kama huo wa kimara ambao umegarimu bill.of money hadi leo hakuna maji yanatoka, DAWASCO wana kila sababu ya kutueleza kinachoendelea kwa sabau huedna ikawa ni usaliti wao ili kujineemesha katika biashara ya maji.
   
 5. Nduka

  Nduka JF-Expert Member

  #5
  Jun 25, 2012
  Joined: Dec 3, 2008
  Messages: 8,479
  Likes Received: 761
  Trophy Points: 280
  Mnyika litolee tamko hili mbunge wa matamko.
   
 6. Tiba

  Tiba JF-Expert Member

  #6
  Jun 25, 2012
  Joined: Jul 15, 2008
  Messages: 4,511
  Likes Received: 95
  Trophy Points: 145
  Wewe usilete utani kwenye mambo ya msingi. Hapa tunazungumzia pesa za umma zilizotumika kutengeneza miundo mbinu halafu maji hakuna.

  Magamba at work!!!!!

  Tiba
   
 7. Tiba

  Tiba JF-Expert Member

  #7
  Jun 25, 2012
  Joined: Jul 15, 2008
  Messages: 4,511
  Likes Received: 95
  Trophy Points: 145
  Ni kweli mkuu ili nalo linawezekana.

  Tiba
   
 8. zomba

  zomba JF-Expert Member

  #8
  Jun 25, 2012
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 17,081
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 0
  Miradi mikubwa miwili ya maji kwa jiji la Dar, ipo katia hatua tofauti, kuna mradi wa Ruvu chini na kuna mradi wa Kimbiji, yote imeanza na ipo kwenye hatua tofauti. Halihitaji kusemewa na mtu kwani bila hiyo miradi kukamilika hata useme nini, jibu litarudi pale pale. Labda uulize hiyo miradi imefikia wapi na inategemwa kwisha lini, Jibu: Mmoja wa Ruvu unategemea kumalizika mwaka 2013 na ule wa Kimbiji mwaka 2015. Hii itatatua upatikanaji wa maji Dar.
   
 9. Tiba

  Tiba JF-Expert Member

  #9
  Jun 25, 2012
  Joined: Jul 15, 2008
  Messages: 4,511
  Likes Received: 95
  Trophy Points: 145
  Asante kwa taarifa hii lakini ningependa mimi binafsi na wakazi wenzangu wa maeneo tajwa tupate majibu kutoka kwa wahusika. Sasa ni mwaka wa 5 tangu hayo mabomba yafungwe lakini maji hamna. Napenda majibu yaingie kwenye record za bunge ili kesho na keshokutwa tuwe na reference. Hizo ahadi za kukamilisha miradi ya Ruvu na Kimbiji imekuwa kama ni nyimbo sasa!!!!

  Tiba
   
 10. Ruge Opinion

  Ruge Opinion JF-Expert Member

  #10
  Jun 25, 2012
  Joined: Mar 22, 2006
  Messages: 1,696
  Likes Received: 306
  Trophy Points: 180
  Kwetu Makuburi habari ni hiyo hiyo. Baada ya Wachina kumaliza kazi, kwanza maji yalitoka vizuri, baadae pressure ikapungua na ukaanza mgao tukawa tunapata siku mbili kwa wiki, sasa hayatoki kabisa. Badala yake kuna kampuni kubwa ina malori makubwa (bowsers) yanaleta maji na kupaki External na sehemu zingine kwenye barabar ya Mabibo jeshini na kutulangua maji. Huu unaonekana kama ni mpango mahususi kati ya wenye kampuni na DAWASCO na labda serikali za mitaa. Labda wenye kampuni ni watu wa DAWASCO wenyewe. Jina la kampuni limenitoka ningeliweka hapa ili wenye taarifa waweze kutujuza nani wamiliki wake.
   
Loading...