Kwa mbiu hizi Kweli CCM ina wenyewe

meeku

JF-Expert Member
Jan 24, 2012
570
170
Najaribu kufuatilia milolongo ya maamuzi ya chama tawala kujisafisha lakini wapi. Yawezekana katika milolongo hiyo na mikakati kama siyo mipango kazi isiyo na malengo lakini inapobuniwa basi sisi wananchi huwa mioyo inainuka tukidhani hapa ndiyo sulusho.

  1. Tulianza na vita ya walanguzi na unyonyaji: Enzi hizo za mwaalimu. Lengo tukaambiwa madaraka yanarudishwa kwa wananchi. hadi leo naona bado hayaji tu. Na marehemu baba yangu alikuwa muumini mkubwa lakini ndo kwanza kajifia bila kuona hayo madaraka yakiruudi. Hapa tulimwona sterling Marehemu sokoine akija na mbinu za kunyonga na kukamata walanguzi. Wapi, tumeshasahau. Enzi hizo RTD kila baada na kabla ya taarifa ya habari kulikuwa na kauli "Acha kuiba mali za uma, weweee" Chezea ccm wewee.
  2. ufagio wa chuma: Hapa Sterling akiwa mzee mwinyi alitengeneza kabisa ufagio wa chuma. Watu tukawa na mategemeo kama hawa mafisadi wameshindwa kung'oka kwa fagio wa chelewa basi huu wa chuma lazima wango'ke tuu. Mzee mwinyi kama anapitia JF tunaomba atuambie ule ufagio uko wapi? Au waliupiga mnada. Mbona hatujaambiwa? au ulipiga kutu tuandae wa steal au fagio la kopa?
  3. Mkapa sikumbuki yeye alikuwa na kauli gani? ila pengine uzee nao unanikuta kusahau?

Stearling JK. hapa zipo movie nyingi:


  1. Majina ya wauza unga yapo na nitayaweka hadharani muda wowote: Kwa tafakari yangu hapa alikuwa anamaanisha unga wa sembe na ndiyo maana imeshindikana kutaja majina kwani mashine za kusaga kila siku zinaongezeka na hata maagenti wa kuuza unga wanaongezeka. Mzee anasubiri kuwaorodhesha wote atutajie.
  2. Kuvua gamba: magamba yenyewe wengine wamesema limeishia kiunoni labda tupeleke shoka. Du!! hii kali. Siku ya kuanza hii operation niliamini basi kama binadamu nasi tunaweza kuvua gamba kama nyoka basi TZ itakuwa pepo kwa wote tutakuwa nyoka wapya. Mashaka yangu ni kuwa wapo waliovua magamba yao; sasa hawa watakuwa wamevua na sumu iliyoko midomoni mwao au ndo kwanza sumu inaongezeka? Starling tuambie ili kama sumu imezidi basi tuwavalishe waliovua magamba yao.
  3. Kilimo kwanza: Mimi siyo mkulima lakini naona hapa kuna jambo. Ni kilimo kwanza au unga kwanza? kwa sababu tangu tuanzishe hiyo mbiu hadi leo ndo wateja wa unga wamezidi.
  4. Tumethubutu tumeweza tunasonga mbele??????: Mwanangu aliniuliza "baba tulithubutu nini????" Naombeni jibu nimpatie mwanangu"
  5. Mawaziri Mzigo: Sijui huu mzigo alifunga nani na unapelekwa wapi? Hii ndo latest siingle ya wazee wa CCM? Swali huu mzigo anatarajiwa kuubeba nani na aupeleke wapi? Na je Mbona kuna dalili kuwa huo mzigo uttaendelea kuozea ulipo? Sehemu kubwa ya hizi mbiu imelenga watu kuwajibika na pengine kutoa fursa ya kujisahihisha. Mbona sioni hata mamoja anayewajibika kwa hizi mbiu au ni ubunifu tu wa kutunga mbiu??? NA WENYE CHAMA NAO WANA MBIU MOJA TU "HANG'OKI MTU HAPA" wadau yawezekanaa kuna niliyosahau, nikumbusheni kwani nataka kufanya collection ya the best of CCM.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom