Kwa mbali nimeanza kuuelewa ulinzi mkali wa Rais...

Kweli ulinzi mkali kabisa unahitajika, aongeze zaidi ulinzi, kuanzia, hasa katika safari zake zote, hata ktk ndege zake aongeze ulinzi kote yaani, sbb kumbe maadui zake ni watu wakubwa wastaafu walioshika madaraka makubwa.. Kupambana na maadui kama hawa kweli unahitaji kutumia njia zote kushinda. Naunga mkono hoja aongeze ulinzi mkali kabisa
 
Kweli ulinzi mkali kabisa unahitajika, aongeze zaidi ulinzi, kuanzia, hasa katika safari zake zote, hata ktk ndege zake aongeze ulinzi kote yaani, sbb kumbe maadui zake ni watu wakubwa wastaafu walioshika madaraka makubwa.. Kupambana na mafisadi kweli unahitaji kutumia njia zote kushinda. Naunga mkono hoja aongeze ulinzi mkali kabisa
Leo wastaafu wamekua mafisadi, kazi ipo!!
 
Kama Mambo ndani yako hivi Tena kwa watu wa karibu...kwa hawa tu tunaowajua..itakuwa vipi kwa Wale wengine tusiowajua?
Babu unaona mbali sana.

This post is thinking outside the bottle.

Inaonyesha kumbe incumbet ameishi na hatari jirani mno, lakini sisi tukawa tunajihoji kuwa huo ulinzi wa nini? Mungu aweke ulinzi zaidi kwake na kwetu pia
 
Nahisi Raisi alikuwa anatamani aongee mengi kutujulisha watanzania jinsi watu wanavyoitaka roho yake lakini alikuwa anashindwa.

Ndio ujue zile kelele za Mange na wenzie kuwa walinzi wanatoka nchi jirani zilikuwa zinatoka kwa watu wa karibu yake walioshindwa kumdhuru.

Ili ufanikiwe kumdhuru lazima uwe na mamluki ndani ya walinzi wake.
 
Hakuna lolote, yani kusiwe na ushindani wa kisiasa? Watu kutaka tu kugombea 2020 nayo inaonekana ni sababu ya mtu kujiongezea ulinzi? Watu wasikosoee?

Basi hakuna haja ya demokrasia. Hivi JK alivyokuwa anakosolewa na hata kutaka kupokonywa kiti ndani ya chama na Edo naye angesema aongezewe ulinzi.

Tusidanganyane, tusitafute kichaka cha kijifichia. Tumekwama kama Taifa, mtu kaharibu mambo wazalendo wanaona sasa inatosha hali hii haiwezi kwenda miaka 10. Kujenga ni kazi ngumu na ya muda mrefu kubomoa ni kazi kidogo sana.

Biashara vilio, kilimo huko ni vilio, uchumi hoi, watumishi hoi, mwaka wa tano huu tunazungumzia Stigler na SG ambao mpaka tukope ndio tujisogezee . Nini cha kujivunia kama Taifa?
 
Back
Top Bottom