Kwa mbali naona wananchi wanafagilia serikali inayoongozwa na Chadema kuanzia 2015

TEMILUGODA

JF-Expert Member
Feb 11, 2012
1,389
285
Salaam kwenu wanabodi! Ni haki yangu naitumia kuweka hapa kwenu great thinkers fikra niionayo juu ya Tanzania baada ya 2015. Binafsi kwa mamlaka ya ujuzi niliopata kwenye falsafa za Karl Max katika uchambuzi wa jamii nafarijika ninapoiona jamii yangu ya Tanzania ikifagilia serikali yao itakayo ongozwa na CHADEMA kuanzia mwaka 2015.

Kwanza kwa kupata tumaini jipya la serikali mpya.Pili kwa kupata mawazo mapya ya watawala.Tatu kwa kupata mbinu mpya za kiuchumi.Nne kwa kupata imani mpya ya mfumo wa uzalishaji mali kwa jamii ya Tanzania. Tano kwa kupata mfumo mpya wa uwajibikaji kwa raia,uongozi na watawala wa nchi.

Sita kwa kupata mbinu mpya za kugawa pato la taifa kwa wananchi.Saba kwa kupata mfumo mpya wa kugawa ajira kwa watanzania. Nane kwa kupata mbinu mpya za matumizi ya maliasili za Tanzania.Tisa kupata fursa ya kujitegemea kama taifa huru lililojikomboa kutoka kwa ukoloni wa ndani.

Kumi na mwisho ni kupata serikali inayotetea haki na usawa wa raia wake kwa kuelimisha umma juu ya kupata haki za msingi. MIMI NIKIWA MBUNGE WA KALENGA KUPITIA CHADEMA 2015 nafarijika sana kuona wananchi wanajituma na kuwajibika katika kazi na majukumu ya kuzalisha mali kama ilivyokuwa miaka ya 1990-1988.

NAWAPONGEZA VIONGOZI WA CDM NA WANANCHI WOTE KWA UJUMLA KTK KUJILETEA MAENDELEO KWA USTAWI WA JAMII YA MTZ.
 
lazima kwanza tujipange vilivyo. kuchukua nchi si kitu cha lelemama. Majeuzi yanihitaji maandalizi ya kutosha
 
Hakuna cha maandalizi ya kutosha wala nini, tuaingia ikulu j kwanza, na kuanza mabadaliko haraka ya ujenzi wa mfumo mpya wa kisiasa na uchumu unaowapa watazania walio wengi mamlaka kubwa ya kufanya maamuzi mazito ya namna ya kutumia rasilimali zao kukuza uchumi wao kwa faida yao na watoto wao. ACHA UPPUZI WA KUJIPANGA KABLA, ACHA WOGA YES WE CAN.
 
Back
Top Bottom