Kwa mazingira yalivyo; je, sanduku la kura liendelee kuwa suluhisho la kupata voongozi?

JET SALLI

JF-Expert Member
Dec 1, 2014
1,991
1,194
Ndugu zangu Great Thinkers hebu tujiulize haya yanayotokea na uhalali wake. Na sasa tufike mahali tuseme sote tena tukiwa na akili timamu kabisa pasipo shaka na pasipo ushabiki wowote kwamba sanduku la kura ndio suluhisho la kupata viongozi ambao wananchi wanawataka kwa ridhaa yao ili waweze kusimamia maendeleo wanayoyataka.

Tunakumbuka Rais mstaafu Jakaya Mrisho kikwete alianzisha mchakato wa katiba mpya naamini hakuwa mjinga kuna vitu aliviona ambavyo Mtawala wa sasa na waandamizi wake hawavioni, mimi na wewe hatujui kama hawavioni kwa sababu ya upeo wao mdogo au mkubwa katak kufikiri.

HV katika hali kama hii tutasema tunawadanganya wachache au tunawadanganya wengi na hasa ktk hiki kinachoendelea kuhusu uchaguzi.

Hivi katika mateso ya miaka mitano ndio CCM inashinda 100% je tunamdanganya nani?Kabla ya kuanza zoezi la UCHAGUZI tumekwenda kwenye nyumba za ibada Kumuomba MUNGU lkn baada ya kutoka humo tunarudi tunamfanyia dhihaka kwa kuendeleza WIZI na dharau kwake na kwa watu wake.

Ndugu zangu kuna kulipia wala tusijidanganye MUNGU anaona na naamini hapendezwi kwa sababu ni MTAKATIFU. KUMBE TUJUE ATA WAADHIBU WOTE WAFANYAO matendo hayo. TULINUSURU TAIFA.
 
Sidhani hata kidogo kama sandaku la kura litaitoa ccm.

Kiuhalisia imeshatoka madarakani ila imeshikilia kinguvu. Basi ni nguvu tu zinatakiwa kuitoa.

Tatizo ni je mimi na wewe tupo tayari!!?

Mungu tupe nguvu kama ulizo wajalia wana wa Israel kuichukua Yeriko. Amen
 
kituo nilicho piga kula jana asubuhi nimeshuhudia mawakala wa CDM na ACT wakipigwa virungu vya hatari , kosa hawana barua za utambulisho na wamekuja kufanya fujo, mwishowe ma CCM yakachakachua kula zetu adi basi
 
Ndugu zangu Great thinkers hebu tujiulize haya yanayotokea na uhalali wake.Na sasa tufike mahali tuseme sote tena tukiwa na akili timamu kabisa pasipo shaka na pasipo ushabiki wowote kwamba sanduku la kura ndio suluhisho la kupata viongozi ambao wananchi wanawataka kwa ridhaa yao ili waweze kusimamia maendeleo wanayoyataka.

Tunakumbuka Rais mstaafu Jakaya Mrisho kikwete alianzisha mchakato wa katiba mpya naamini hakuwa mjinga kuna vitu aliviona ambavyo Mtawala wa sasa na waandamizi wake hawavioni,mm na ww hatujui kama hawavioni kwa sababu ya upeo wao mdogo au mkubwa ktk kufikiri.HV katika hali kama hii tutasema tunawadanganya wachache au tunawadanganya wengi na hasa ktk hiki kinachoendelea kuhusu uchaguzi .

HV KTK MATESO YA MIAKA MITANO NDIO CCM INASHINDA 100% je tunamdanganya nani?Kabla ya kuanza zoezi la UCHAGUZI tumekwenda kwenye nyumba za ibada Kumuomba MUNGU lkn baada ya kutoka humo tunarudi tunamfanyia dhihaka kwa kuendeleza WIZI na dharau kwake na kwa watu wake.Ndugu zangu kuna kulipia wala tusijidanganye MUNGU anaona na naamini hapendezwi kwa sababu ni MTAKATIFU.KUMBE TUJUE ATA WAADHIBU WOTE WAFANYAO matendo hayo.TULINUSURU TAIFA.
Bila kuwa na tume huru ya uchaguzi na katiba ya mwananchi NI UPUUZI MTUPU KUAMINI KATIKA SANDUKU LA KURA
 

Sanduku la kura halina umuhimu tena katika mazingira kama haya tuliyoyaona hamna kitu.


Ni rahisi kushangilia na kusema ccm imeshinda na kuwagaragaza wapinzani vibaya sana.

Pia ni rahisi kwa wachambuzi wa mambo ya siasa kusema hapa nchini "upinzani bado sana na haukujipanga" ila unabaki kujiuliza, katika mazingira kama haya unategemea upinzani ujipange vipi ili kuwe na haki.


Safari bado ndefu.
 
USIFURAHIE KAMWE KWAMBA CCM IMESHINDA 100% UNAJIDANGANYA MCHANA KWEUPE.UTAWALA WA NAMNA HIYO HAUJAWAHI KUWA MZURI KWA AFRICA.WALapumbavu hawawezi kuelewa.Baba wa Taifa aliwahi kusema mpumbavu ni sawa na MTU mfupi ambae huwezi kumrefusha na ukilazimisha kumrefusha utamuua.Nchi imeshachanika vipande vipande wajinga wanaweza kuelewaelewa hv ila usitarajie wapumbavu wataelewa mambo haya sio rahisi ksbisa .
 
KUONGOZA NCHI KUNATAKA AKILI,HEKIMA ,BUSARA NA HURUMA AWAMU YA TANO ILIYAKOSA HAYA YOTE NDIO MAANA WATU WAMESHUHUDIA MATESO MAKUBWA.Tunakoelekea kuna Giza Amini usiamini.Usipotenda HAKI kuna gharama zake ambazo zinaweza kuwa ndogo au kubwa zitakazoacha vidonda vya kudumu kwa watu wote bila kubagua.
 
Demokrasia imenajisiwa kwa kiwango kikubwa sana...
Huwa nalichukia sana neno Demokrasia

Hakuna Demokrasia Dunia
Demokrasia ni uchafu na uvundo

Tukiendelea kuamini neno hili,tutaishia pabaya kama walivyoishia wenzetu
 
Ukifikiria vizuri unagundua kuwa ccm haiwezi toka madarakani kwa mfumo tulip nao.
Msajili anateuliwa na mwenyekiti wa ccm.
Mwenyekiti wa tume anateuliwa na mwenyekiti wa ccm
Wakurugenzi ambao ndio watendaji wa tume, wanateuliwa na mwenyekiti wa ccm
Wasimamizi wa uchaguzi ambao ndio huteua wagombea huteuliwa na mwenyekiti wa ccm
Wasimamia sheria (IGP) anateuliwa na mwenyekiti wa ccm.
Watafsiri sheria (majaji) huteuliwa na mwenyekiti wa ccm
Sasa kwa hali hii chadema unashindaje?
 
Hakika binafsi tangu jana usiku nimeshikwa na bumbuazi la hatari sana. Magufuli analipeleka taifa kusiko julikana. Kikwete na Mkapa nchi itabaki kuwalaani milele.
 
Tutarajie kurudi nyuma zaidi ya hapa tulipo.Uhuru na Haki ya watu kujichagulia viongozi ni muhimu zaidi ya kitu chochote ktk ulimwengu wa Sasa.
 
Sanduku la kura need kwa ajili ya kuwadanganya wazungu ili watupe hela.Ila kazi tunayo kuondoa ukoloni huu wa weusii
 
Ukishinda uchaguzi kwa Haki hata isoni kwako kunaonekana ushindi waziwazi lkn watazame CCM Kama ww ni mdadisi wa Mambo utaelewa kitu kikubwa sana.
 
Back
Top Bottom