Mwiba
JF-Expert Member
- Oct 23, 2007
- 7,607
- 1,745
Kila mmoja ana fikra na muono kwa jinsi hisia za siasa miongoni mwa wananchi wa Tanzania zinavyopanda chati,tuweke tofauti na jazba pembeni,ili kila mmoja wetu aweze kutoa maoni yake ,unafikiria CCM inaweza kukaa madarakani kwa muda gani(Mungu anajua zaidi)Lakini na sisi binadamu tunaweza kukisia kutokana na hali inavyokwenda.
Kwa upande wangu sioni ukaribu wa kuiondoa CCM madarakani kipimo nilichokitumia ni chaguzi zilizopita zinaonyesha vigogo hawawezi kuondolewa kwa kura za upinzani hata siku moja ,CCM imejikita kila sehemu na uchaguzi unapochanganyika na upinzani kuwania madaraka ya kiserikali(Ubunge) huwepo mipango maalumu ambayo upinzani hawana ubavu nayo na kuifanya CCM iondoke na ubingwa ,na CCM wanapokuwa katika ugombeaji huo hupima nguvu zao na huongezwa za ziada pale wanapoona pana shaka na ushindi.
Ninachotaka kukisema ni hizi nguvu za ziada ambazo huwapeperusha wapinzani na wasijue la kufanya,kwa kutoa mfano hai ambao umetumika mara zaidi ya Tatu ni Uchaguzi wa wapemba huko CCM inatumia nguvu hizi kwa dhahiri kabisa(Polisi,jeshi,usalama wa Taifa) na ndio mpaka leo inaendelea kuwepo ,sasa kwa hali inavyokwenda hapa Bongo imefikia wakati nguvu hizo nazo kutumika kikamilifu kama kule visiwani au zaidi ,ndipo nikasema sitegemei ukaribu wa kuing'oa CCMmadarakani kwa sera hizi za kutaja ufisadi na kuwataja mafisadi ,hizi sera hazina mshiko wa kuiondoa CCM madarakani.
Napenda wapinzani mulielewe hili wala halina mabadala,mtasomba wapiga kura wengi.au kwa lugha sanifu mtawateka wengi tu,lakini CCM haishughuliki kwa kuona wamepoteza wapiga kura na kuwasababishia kupoteza kiti,wana uhakika wa kujinyakulia kwa kutumia vyombo vilivyodhibitiwa na serikali yao,CCM haitakuwa tayari kuona wanaipoteza serikali wakati kila kitu wancho na sababu wanazo,hivyo mtasubiri sana.