kwa mawakala wa m-pesa,tigo pesa

Kuku wa Kabanga

JF-Expert Member
Oct 28, 2009
807
366
Habari zenu wadau
Mimi ni mgeni kwenye hii biashara,naomba ushauri wa uzoefu kuhusu jambo moja,utachukua hatua gani endapo unapata mteja anataka kutoa hela kwenye akaunti yake,lakini anapokurushia wewe ili umpe cash,yeye anapata confirmation sms kutoka mtandao husika lakini wewe wakala hupati,utampa pesa au utamwambia asubiri upate sms hiyo?
 
ww huruhisiwi kutoa pesa mpaka upate sms,..wengine wanachofanya ni kuchukua cmu ya mteja na kunakili namba ya muamala..then anampa helaa
 
Kunakili namba ya muamala inakusaidia nini,unaitumia vipi hiyo namba?
 
Just in case mambo yakienda sivyo unakuwa na sehemu ya kuanzia kufanya follow up kwa service provider wako kwa kuwa namba ya muamala inatolewa na service provider i.e vodacom or tiGO
 
Asante kiongozi kwa mchango wako.
 
Kawaida unachukua simub ya mteja na kisha unanakili namba ya muamala, then unawapigia tigo au mpesa ku- confirm transaction. Wakikuthibitishia imepita then unampatia fedha. Lakini mara zote unashauriwa kuweka kumbukumbu ya floating balance kila wakati.
 
Ahsante mkuu,imenisaidia.
 
Mpesa ni 15366 huwa wanakata kama sh.mia ukiwapigia wadau nahitaji lain ya tigo pesa msaada tafadhali.
 
Habari zenu wadau
Mimi ni mgeni kwenye hii biashara,naomba ushauri wa uzoefu kuhusu jambo moja,utachukua hatua gani endapo unapata mteja anataka kutoa hela kwenye akaunti yake,lakini anapokurushia wewe ili umpe cash,yeye anapata confirmation sms kutoka mtandao husika lakini wewe wakala hupati,utampa pesa au utamwambia asubiri upate sms hiyo?

Kwenye Mpesa hata siku moja usitoe hela bila wote kupata msg. Labda mkiruhusiwa na customer care au kama una mtandao wa mpesa kwenye computer uangalie kama transaction ni completed kabla ya kutoa hela.

Tigo siku zote ina tabia ya mwenye kutoa hela kupata msg na wakala kutopata. Inabidi kutumia msg ya mteja na kuangalia kwamba salio lako limeongezeka kwenye till ya kazi. Jifunze vizuri kuielewa msg ya tigo ili kuakikisha sio feki. Sasa hivi kuna watu wenye uwezo wa kutuma msg kama za mtandao, tofauti ni kwamba salio haliongezeki kwenye simu ya kazi.
 
Hapo nimekusoma mkuu,hilo la tigopesa limetokea mara kadhaa.

Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums
 
Back
Top Bottom