Kwa matokeo haya ya waliounga juhudi kuangukia pua, mmeamini kuwa CCM ina wenyewe na wenyewe ndio hao?

Aliyewapa wazo la kununua watu ili kuuwa upinzani yafaa wamkamate arudishe pesa alizopiga aliwapa wazo na shauri la kijinga kabisa la Karne hii,limeshindwa kuwaletea tija.Huwezi uuwa upinzani kwa kununua wanaopigiwa kura Hali upinzani ndio chuo pekee cha kupika chipukizi wa siasa baada ya chuo cha ccm cha siasa kufa.
Njia pekee ya kuuwa upinzani ni kuboresha maisha ya watz, upinzani utajifia wenyewe Kama ilivofanya chama cha ukombozi cha watu wa China.Muondolee mtu njaa ashibe atakupenda.Na sio kumfanya awe masikini kwa kumsomesha namba ili umtawale hapa umejitengeneza bomu
Che Nkapa katika wasia wake (My life; My Purpose) nae kawaeleza.
Wa Ibo (Nigeria) wanasema "..........Nzi mbishi huishia kuzikwa pamoja na mzoga.........."
 
.
Alafu damu za puani zinakuwa nyingi Sana na zinachelewa kukata
20200722_113520.jpg
 
Tanga kuna diwani wa kata ya mng'aro lushoto anaitwa jambia jumaaa amepita alikuwa chadema 2015-2020 akaunga juhudi

Tanga kuna diwani wa kata ya mng'aro lushoto anaitwa jambia jumaaa amepita alikuwa chadema 2015-2020 akaunga juhudi
Huyo amemuiga Ndugai mtaalamu wa kutembeza rungu kuwatwanga wapinzani wake safari hii amepita kwa kishindo wa Tanga ametumia jambia kuwakatakata mikia wapinzani wake kuinuka kidedea. Wasukuma wa Simiyu si wabunifu wanategemea kushinda kwa kuunga mkono juhudi, warithike na dau walilopewa kuhama Chama, wajaribu Tena miaka 5 ijayo wakitumia mishale au mikuki watashinda.
 
Kwa utafititi nilioufanya kwa mikoa 3 tu yaani Mwanza,Mara na Simiyu ,madiwani waliounga Juhudi kisa mh Rais na baadhi kununuliwa na kupewa nafasi ya kugombea kwenye chama cha CCM wote wameangukia pua

Mpaka sasa sijapata Diwani aliyeunga juhudi aliyependekezwa na ccm kupeperusha bendera

Wengi wa madiwani waliounga juhudi matokeo yao yamechezea 0 hadi 3 tu kati ya wapinzani wao ccm asili waliochezea 78 kwa 105

Asanteni CCM
 
Kwa utafititi nilioufanya kwa mikoa 3 tu yaani Mwanza,Mara na Simiyu ,madiwani waliounga Juhudi kisa mh Rais na baadhi kununuliwa na kupewa nafasi ya kugombea kwenye chama cha CCM wote wameangukia pua

Mpaka sasa sijapata Diwani aliyeunga juhudi aliyependekezwa na ccm kupeperusha bendera

Wengi wa madiwani waliounga juhudi matokeo yao yamechezea 0 hadi 3 tu kati ya wapinzani wao ccm asili waliochezea 78 kwa 105

Asanteni CCM
Wajumbe wa chama tawala si wa mchezo, wamekwisha kufanya mambo yao. Ni wakati wa ng'ombe waliokatwa mikia kurudi ktk mazizi ya asili yao. Wasione aibu, mbona hata Lowassa na Sumaye walijisalimisha.
 
ukiona hivyo ujue hao ni fungu la kukosa,tunaaomba waendelee kuunga juhudi mkono
 
wanachama wa ccm hawakushiriki kwa ujinga wa kudhoofisha misingi ya uongozi wa Taifa kwa misingi ya kidemocrasia, kama walishiriki, kipindi hicho hao malaya wa chadema wananunulia wangepitia kwenye mchakato wa namna hii ndani ya ccm wakashinda alafu wakaingia kwenye uchaguzi wa ushindani sawa na vyama vingine washinde pia.

Ukumbuke, hao malaya walishinda baada ya kupigiwa kura nyingi na wananchi katika maeneo yao, kama walikuwa wanataka kuunga mkono juhudi wangeziunga kwa hoja bila kuliingiza Taifa Hasara za kurudia uchaguzi huku wakipokea hongo kutoka account za serikali pale Ikulu.

aliyekuwa na lengo la kudhoofisha upinzani ni Magufuri, ujinga kabisa, Magufuri hajawahi jitambua kama ni kiongozi wa Taifa na hivyo ni kiongozi si tu wa wananchi bali wa vyama vyote vya upinzani, Kama kiongozi wa Taifa hajui kama anawajibu wa kuona Taifa linasheheni siasa safi na mfumo wa kidemocrasia unaokua.

hata huko kuudhoofisha upinzani kwenyewe akikufanya kishamba, alivunja hata taratibu za chaguzi ndani ya ccm. ndio maana sasa wana ccm wamempa majibu. CCM ni chama kikongwe, kina katiba na kanuni zake na zinafahamika kwa wanachama wake, na hawavumilii ujinga wa ulevi wa madaraka.
Wameshiriki kwa kumuunga mkono mwenyekiti wao na viongozi wao (wa chama na serikali) walio ongoza kwenye kuwanunua au kuwapa ahadi hao unaowaita malaya. Tumeona wakishiriki kwa mbwembwe kwenye kuwakaribisha hao watu na hata kwenye chaguzi kuwapigia kura na kushinda tena viti vyao.
 
Hakuna kitu kinauma kama kuunga mkono halafu mwisho wa mchezo unakuja kukatwa.Unaweza ukajinyonga kabisa, maana unaunga juhudi za mwenyekiti ukiwa na kinyongo.
 
Kwa hili wana CCM wenzangu mmetisha sana! Tuwafundishe kuwa wakijiunga kwetu wajenge chama kwanza ndipo wagombee. Walifikiri kura zitapigwa na mwenyekiti?
 
Silinde kajidhalilisha sana
Alikuwa na Jimbo kupitia Chadema bila mpinzani. Masikini kaamua kuunga juhudi dakika za mwisho yaani apate posho za siku 10 Chadema walizokaa nje kwasababu ya covid
Mh Silinde kaishia kupiga magoti juu ya ngawasuma, picha inayomdhalilisha na itakayomdhalilisha maishani mwake na watoto wake. Kwamba Baba hakuwa na namna, watu wakipiga magoti miskitini na makanisani yeye alipiga magoti mbele ya wajumbe. Yaani hiyo picha tu inatosha kueleza kiwango cha uelewa wake hataka kama ana madigrii

Mkewe naye anaiona na anaona jinsi mume anavyotafuta mkate! Hii ni dhalili ya kiwango cha kimataifa
 
Back
Top Bottom