Tabutupu
JF-Expert Member
- Nov 26, 2010
- 13,185
- 18,513
Matokeo yameonyesha wazi, shule zilizofanya vizuri ni zile za gharama, ambazo wananchi wa kawaiada hawaendi huko.
Shule kama Mzumbe, Ilboru, Msalato, Tabora boys zote hazimo top 10 kitu ambacho nahisi kimechangiwa na ukosefu wa walimu pamoja na ukosefu wa fedha za vitendea kazi.
Serikali kujinasibu kuwa inatoa elimu bure wakati inatoa fedha zisizo kidhi mahitaji ya shule ni kuua elimu na kuwaonea wanyonge ambao hawana fedha za kupeleka watoto wao shule za private.
Tunaomba serikali ituache tuchangie, kunusuru elimu ya walala hoi kwa kuwa serikali imeshindwa kutimiza majukumu yake.
Pia haya ni matokeo ya kubana matumizi wakati walimu mashuleni hawapo. Walimu wamejaa mitaani, shule zimejaa madawati bila walimu, ajabu sana.
Kwa mwendo huu tusitegemee kuona hata ndani ya top 50 shule yoyote ya serikali kama tutaendelea kukimbizana na miradi isiyo na tija kwa mtanzania kama ndege, airport vijijini, maamuzi yasiyo pitiwa na bunge etc.