Kwa matatizo ya gari

Styvo254

JF-Expert Member
Aug 5, 2015
246
226
Habari za masiku wanaJF,

Kwa mda flani sasa nimekua nikifatilia swala la matatizo ya magari, na vyombo vya moto kwa jumla hapa, kwa sababu za kutoa ushauri - sio kw malipo, na pia huduma - kw mapatano.

Hapa naanzia uzi wa kutoa msaada wa mawaidha, utakavyofanya au fatilia tatizo ili uelewe utakavyotatua na kujibu maswali yoyote kuhusu ufundi wa magari na vyombo vya moto.

Napendekeza kuweka issue/tatizo hapa kwa forum ili wengine waeze kusaidika ILA kuna mambo yatabidi tuyagange nyuma ya pazia.
So, karibuni nyote.
 
Ingekuwa vyema ukawa na eneo moja la kueleza issues za magari. Mfano ule uzi wa nissan xtrail shida na ufumbuzi wake ulikuwa poa sana. Unaweza ukaongeza matatizo na ufumbuzi wa magari mengine pia mkuu
 
Ingekuwa vyema ukawa na eneo moja la kueleza issues za magari. Mfano ule uzi wa nissan xtrail shida na ufumbuzi wake ulikuwa poa sana. Unaweza ukaongeza matatizo na ufumbuzi wa magari mengine pia mkuu
Asante Bw, Galindas
Uzi wa Xtrail bado utaendelea. Huu hapa ni kw matatizo ya magari na vyombo kw jumla.
 
Habari, naomba ushauri wa kiufundi juu ya Toyota Brevis. Nakusudia kununua siku chache zijazo lakini sijui common merchanical problems of this car.
 
Habari, naomba ushauri wa kiufundi juu ya Toyota Brevis. Nakusudia kununua siku chache zijazo lakini sijui common merchanical problems of this car.
Mambo vp,
Naam, Toyota brevis ni gari nzuri sana ya high class sedan, yaani gari ndogo ila ya ngazi ya juu. Ukiangalia ukubwa wa gari lenyewe na engine yake pia utaona ni ya ngazi moja na Mercedes E class, BMW 5 series ingawa kwa bei nafuu kidogo.

Humu kwetu brevis ziko kibao na pia spare ni tele. Mafundi ni swala tofauti kwa kua gari hili linatumia mifumo ya umeme sana na phobia waluonayo mafundi wetu ni ile ya umeme! BUT, issue kubwa ni diagnosis ambayo nina uhakika ni jambo linalotizamwa na mafundi wetu kwa makini sasa.

Lingine la kuweka maanani ni ule ukubwa wa engine! Ukubwa wa lita mbili unusu sio mdogo hasa kwa matumizi ya mjini! Uzito wa ile gari ni mkubwa kwa hiyo ufaidi kwenye highway cruising/driving yaani masafa marefu. Kwa matumizi ya ndani ya jiji, itakua ya show tu sio ya faida!
 
Mambo vp,
Naam, Toyota brevis ni gari nzuri sana ya high class sedan, yaani gari ndogo ila ya ngazi ya juu. Ukiangalia ukubwa wa gari lenyewe na engine yake pia utaona ni ya ngazi moja na Mercedes E class, BMW 5 series ingawa kwa bei nafuu kidogo...
Asante kwa maelezo.
 
Habari mkuu.. kuna rav 4 kili time inakula sana mafuta... Ni 1790cc ukiiwasha mshale wa accelerator unafika hadi kwenye 2 bila kukanyaga padel... tatizo ni nn apo?
 
Habari mkuu.. kuna rav 4 kili time inakula sana mafuta... Ni 1790cc ukiiwasha mshale wa accelerator unafika hadi kwenye 2 bila kukanyaga padel... tatizo ni nn apo?
Asante kw swali! Nadhania wamaanisha hata engine ikiwa imeshapata joto bado idle speed iko juu?

Hapo itabidi inlet manifold na throttle ziangaliwe baada ya service hadi plugs? Uenda ikawa kuna hewa inaingia na sehemu baada ya throttle butterfly, au pia ni fuel system.

PROPER SERVICE, DIAGNOSIS kisha SOLUTION!
 
Nipe darasa kuhusu Toyota cresta GX 100 kuna rafiki angu anataka kuniuzia
Asante kw swali! Toyota GX100 ni chassis iliyotumika kwa muundo wa Toyota Chaser ambayo ina matoleo mawili; Avante - muundo wa kifahari na Tourer - 'sport'/muundo wa kasi. Licha ya ukubwa wa body, gari hili ni la daraja ya wastan/kati na kwa hiyo tunapata engine zisizozidi lita tatu ukubwa, ya chini ni lita mbili unusu.

Engine zake (1JZ/2JZ) zaweza kua na turbo ( moja au mbili), VVTI au teknolojia zingine za kuboresha. Mfumo wa umeme unatumika sana katika gari hili na ni muhimu sana kuzingatia diagnosis, service na spares genuine ili kuepuka matatizo. Spare parts ziko tele na kw bei nafuu.

Kulingana na ukubwa wa mashine na pia gari lenyewe, gari hili sio nafuu sana kw matumizi ya kati ya mji na foleni zake.
 
Nipe uzoefu wa kichocheo cha nano enagizer kuwa unaweza kukitumia bila kufanya overhaul katika engine?
 
Nipe uzoefu wa kichocheo cha nano enagizer kuwa unaweza kukitumia bila kufanya overhaul katika engine?
Asante kw swali!

Hiyo bidhaa na zinginezo zinazonadiwa kama 'overhaul in a pack/bottle', zimekua sokoni kw mda. Kuna teknolojia kadhaa wanatumia kama vile Teflon, nano-technology na pia kemikali. Ili kuelewa utendakazi wake, ni muhimu kuelewa hali na udhoofu wa mashine, yaani 'engine state and condition'.

Engine inayohitaji overhaul hua vyuma vyake muhimu vimepungua. Utapata kw sababu ya friction piston rings na cylinder wall zitakua zimeadhirika na kua zinavujisha mskumo wa hewa (combustion pressure) na pia kupitisha oili kw michirizi midogo midogo iliochimbika mle kw cylinder wall. Hapa basi ndipo utapata ile science ikitumika kuweka 'coating/layer' ya ile bidhaa pale. Hii ufanyika pale bidhaa inapoyeyuka-joto (melt) na kupata kwa ile cylinder na pia kwa rings na piston.

Vyuma sio vitu pekee vinavyoisha katika mashine! Utapata pia oil seals na gaskets zitakua zimekauka kwa sababu ya 'heat-cycles' na pia oil contamination. Kuna bidhaa zinazotumia kemikali (conditioners) kutatua hili kwa kulainisha ile rubber au plastic ikaweza kunenepa na kuziba vizuri.

Mashine inatumia vitu kama timing chain, gears/wheels, tappets na vyuma vingine ambavyo kuisha kwake hakuwezi finikwa kw kupakwa unga au dawa. Kuna pia issue ya aina na usafi wa oili inayotumika kw ile mashine. Uchafu na kemikali geni zaweza hitilafiana na ile dawa na aitha kuzidisha ile 'conditioning' na kuyeyusha mipira.

Pia engine miundo ingine kama 'flat' kama vile kw Subaru, haziwezi faidi kwa matumizi ya bidhaa hii labda iwe liquid form na pia pale yaweza kolea kwa upande wa chini wa piston due to gravity!

Ukweli mzuri, suluhu ya uhakika ni complete and thorough overhaul! Na hili halifanyiki kama hakuna MDA, HELA (UJUZI NA SPARE) NA PIA NIA!
 
Asante kwa uzi huu mkuu. Nahitaji kununua gari dogo kwa matumizi ya kawaida/mizunguko ya mjini na masafa ya mkoa kwa mkoa. Vipi kuhusu "Aud"?
Asante kw swali, ingawa gumu kweli; sio kw kujibu ila kwa kujibiwa!
Kwa hilo swali lako kuna contradicting factors mbili ambazo kuafikiana ni mbinde! 'Gari dogo' la matumizi ya mjini haliwezi kua nafuu kwa 'masafa ya mikoani' ILA kwa miundo chache kama "AUDI" (ulivyotaja) Benz na magari/miundo michache ilyo na 'the right mix' ya 'Sport- Touring' (GT) na economy. Magari haya yanahitaji matunzo ya hali ya juu na pia uangalifu flani; SIO KUSEMA GHALI! Linalotatiza zaidi ni uelewa - kwanza wa mwenye gari, THEN ujuzi wa fundi - nasema hivi sababu ukipata gari la kifahari linakarabatiwa kichochoroni, kwanza kaamua mwenyewe kisha kampa fundi PERIOD

La kuzingatiwa kimsingi (kando na magari tulioangalia hapo juu), ni kua matumizi ya mjini yanahitaji engine ndogo, na kw hivyo uzito mdogo wa gari ilhali kwa safari za mikoani inafaidi kua na gari kubwa ili kua na inertia/momentum ya kuwezesha cruising - mzunguko mdogo wa engine kw kudumisha kasi ya gari!

Magari ya kisasa yana teknolojia zinazowezesha mashine kubwa kutumia mafuta kidogo kama vile VVTI, CGI, D4/8, VTEC, n.k. na pia mashine mdogo kua na nguvu zaidi kw kutumia turbo za VNT/VG, n.k.

Kuna factors zingine pia za kibinafsi itabidi uangazie kw makini ili kupata suluhu. Mambo kama ukubwa wa familia(idadi ya abiria), mazingira ya matumizi hasaa kw safari (Off au On-tarmac), upatikanaji wa utaalam na spare na pia kimo cha mfuko na/au upana wa mawazo yako!

La kuwaza! Aliye na Patrol 4.2 hulsusan safari za mikoani na pia Isis au Toyota/Nissan nyingine ndogo kw matumizi ya mjini, anatumia hela kidogo kw magari hayo zaidi ya aliye na lake moja na PIA baada ya mda kudhoofika kw body na mashine kutapunguza resale value ya hii asset muhimu!

Na kwa hayo yangu machache, maamuzi ni kwako kaka ila ijapo kuna swali, by all means .....
 
Habari za masiku wanaJF,
Kwa mda flani sasa nimekua nikifatilia swala la matatizo ya magari, na vyombo vya moto kwa jumla hapa, kwa sababu za kutoa ushauri - sio kw malipo, na pia huduma - kw mapatano...
Mkuu naomba nijuzwe matatizo na ufumbuzi wa Nissan Murano tafadhal
 
Mkuu naomba nijuzwe matatizo na ufumbuzi wa Nissan Murano tafadhal
Mkuu ! Naomba unijuze magonjwa common ya Nissan x-trail na ufumbuzi wake
Kw 'Mkulima Big Results' na 'NHS'; asanteni kw maswali yenu. Naomba mniruhusu kuyajibu kw pamoja.
Magari ya Nissan kw ujumla ni magari ya hali ya juu licha ya kua na sifa mbaya ya kudumu kwake na ufundi wake kw jumla. Kwa maoni yangu problem ni kutoeleweka vizuri na mafundi wetu, wengi wakiwa wamegobea kw Toyota. Nissan, kw maoni yangu, hutumia teknolojia ya hali ya juu na isio rahisi kuelewa bila kua makini sana.

Magari ya Nissan hukashifiwa sana kwa upande wa auto transmission. Shtuma hizi hazina misingi yeyote ya kiufundi au matumizi ila ni matunzo mabaya au kutowajibika kuzuri katika service zake. Kampuni ya Jatco inayo milikiwa na Nissan inakandarasi za kuwatengenezea transmission waundaji magari wengine mashuhuri kama Nissan, Jaguar na Landrover; hii ni dhihirisho kua wako stadi sana katika utaalam huu.

Cha msingi kabisa kuzingatiwa katika haya magari, na pia mengine yote, ni diagnosis au udadisi unaofanywa pale wakati wa service au tatizo linapoibuka. Nissan hutumia mfumo wa CONSULT katika kudadisi mitambo ya magari yake, bila huu mfumo ni ngumu sana kulenga tatizo kwa uhakika na haraka. Pia mambo mengine kama programming na module initialization lazima yafanyike kwa mfumo huu unaotumia kompyuta.

Nissan na Renault ni kampuni ndugu, utapata engine na transmission za Nissan kw magari haya ya kiFaransa.
 
Kw 'Mkulima Big Results' na 'NHS'; asanteni kw maswali yenu. Naomba mniruhusu kuyajibu kw pamoja.
Magari ya Nissan kw ujumla ni magari ya hali ya juu licha ya kua na sifa mbaya ya kudumu kwake na ufundi wake kw jumla. Kwa maoni yangu problem ni kutoeleweka vizuri na mafundi wetu, wengi wakiwa wamegobea kw Toyota. Nissan, kw maoni yangu, hutumia teknolojia ya hali ya juu na isio rahisi kuelewa bila kua makini sana...
Nashukuru mkuu kwa maelezo mujarrab..naomba unipe au unielekeze garage ambayo kidogo wana ufaham na hilo jambo tafadhal
 
Gari yangu ni aina ya premio old model inaniwashia alama ya check engine nimepeleka kwa mafundi lkn hiyo alama haitoki na kupelekea gari kuwa na mis msaada
 
Back
Top Bottom