Kwa matamshi haya kuhusiana na uchaguzi mdogo huko Zanzibar, Makamu wa Raisi Zanzibar kutoka ACT-Wazalenido kujiuzulu wakati wowote?

Pslmp

JF-Expert Member
Mar 18, 2021
1,624
2,000
Ulaya kulikuwa kuna nchi inaitwa Czechoslovakia. Sehemu moja ilipoona kuwa hairidhiki na hali ilivyo ikafanywa referendum kuhusu ushirika huo. Sharti likikuwa nchi itabaki ilivyo kama tu pande zote zitaridhia. Pande moja ikakataa, wakaheshimu maamuzi, wakapeana talaka. Matokeo ni nchi ya Czech na Slovakia. Mpaka sasa wanaishi kwa amani.

Huko huko kulikuwa na Yugoslavia. Slovenia na Croatia wakalalamika kuwa Serbia inawanyima haki zao na inajifanya yenyewe ndio Yugoslavia. Serbia wakakataa kuwasikiliza. Slovenia na Croatia zikajitangaza kuwa ni nchi huru. Serbia wakashambulia Croatia kupinga uamuzi huo. Matokeo ni vita ambamo raia wengi walipoteza maisha na unyama mkubwa ulifanyika. Hatimaye Yugoslavia ikasambaratika na sasa kuna Slovenia, Croatia, Serbia, Bosnia na Herzegovina, Macedonia ambazo kila moja ni nchi huru.

Uingereza mpaka leo kuna wa Scot wanaotaka waondokane na uUK . Spain hivyo hivyo.

Hauwezi kulazimisha umoja. Mmoja akichoka ni heri kutengana kwa amani kuliko kulazimishana.

Amandla...
Tukiwaachia tu na wao hawaaminiani, Pemba itakuwa nchi huru pia Unguja nayo, sasa hayo yoote ya nini?
 

white wizard

JF-Expert Member
May 18, 2011
6,325
2,000
Kitu ambacho sipendi ni muungano kuvunjika. Utawasikia baadhi wanaomba msaada na kulalamika kwa nchi za Ulaya ambazo nazo zimeungana. Ujerumani, Uingereza, Marekani bila kuungana zingekuwa na uwezo mdogo kuliko sasa
Muungano wao utaulinganisha na huu wa kwetu?, ambayo kiongozi wa huko lazima achaguliwe toka bara, usilinganishe muungano wa huko, na muungano huu wa ajabu ajabu tu.
 

Fundi Mchundo

JF-Expert Member
Nov 9, 2007
7,029
2,000
Tukiwaachia tu na wao hawaaminiani, Pemba itakuwa nchi huru pia Unguja nayo, sasa hayo yoote ya nini?
Neno "tukiwaachia" halipendezi maana lina maanisha kuwa ni matakwa yetu ndio yenye umuhimu kuliko ya raia wa Unguja na Pemba.
Kwani kuna ubaya gani kama hicho ndicho wanachokitaka? Hiyo ni heri kuliko Tanganyikakuweka majeshi yake huko kuwalazimisha wakae pamoja.


Amandla...
 

Huihui2

JF-Expert Member
Jan 5, 2012
1,604
2,000
Muungano wa Tanzania hauna tija kwa pande zote 2.
Pande zote 2 hazitaki Muungano. ZNZ wanasema tunawakalia kimabavu na tunawachelewesha kupata maendeleo yao wakati Tanganyika wanadai wanabeba gharama za kuiendesha Serikali ya ZNZ.

Muungano umefeli upigwe chini tu kama miungano mingine tu duniani mfano USSR, Yugoslavia
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom