Kwa matamshi aliyotoa akiwa Kilosa na Kilwa, Rais Magufuli anaweza kutoa kauli zitakazoiletea nchi matatizo makubwa wakati wa kampeni

G Sam

JF-Expert Member
Apr 20, 2013
11,555
35,880
Kwa sasa sina shaka kabisa kuwa Rais Magufuli kila akizungumza mara nyingi ni lazima aache upepo mbaya wa kauli za maudhi kwenye jamii. Hilo sasa halina tena mjadala.

Sasa kwa muda huu Rais Magufuli anazungumza hayo akiwa peke yake na hakuna majibizano ya dhahiri kutoka upande wa pili. Anazungumza hayo huku akijua fika kuwa kwa sasa hakuna wa kumjibia. Kwa hilo anajiandalia mazingira hatarishi wakati wa kampeni.

Hakuna mtu atakayekubali kuona mgombea mwenzake akiongea maneno kama ya jana ya Rais Magufuli akiwa Kilwa au kipindi kile alipojichanganya akiwa Kilosa na hatimaye rangi yake halisi ikaonekana, kisha akae kimya bila kujibu. Najua wengi mnaelewa kinachotokea pale Rais Magufuli anapojibiwa.

Ni kweli kuwa Rais Magufuli ana chuki za wazi tena kutoka moyoni dhidi ya wale wapinzani wake wa kweli kisiasa! Chuki hizi zimepelekea matukio kadhaa kutokea ambayo ni mabaya sana na matukio ya aina hii huwa yanakuja kuwa na majibu mabaya siku za usoni.

Ipo hatari kubwa sana ya dhahiri itakayotokea siku za usoni wakati wa kampeni itakayoletwa na Rais Magufuli ikiwa ataendelea kuthubutu kuongea vile. Ni jambo la hatari sana analokuza na sijui kwanini haelewi.

Mimi binafs nachukizwa sana na kauli hizi na huwa nawaza ikiwa zitazungumzwa kwenye uwanja wa kampeni ni nini kitatokea? Nakiona kitakachotokea! Rais aelewe kuwa kipindi cha kampeni ndipo nchi yetu inakumbwa na vitendo vya mauaji na yote yanatokana na sisi kutokuchunga midomo yetu. Rais akiwa kama kiongozi wa nchi ameanza vibaya sana!

Rais aelewe kuwa kauli zake hazitafanya upinzani uyeyuke nchini bali zitafanya wapinzani wa kweli waanze kuwa na chuki moyoni na hapo ndipo ubaya utakapoanza kujitokeza. Rais afundishwe kuwa sasa nchi hii kama ilivyo kwa dini, pia ina watu wenye mtazamo tofauti wa kisiasa hivyo akiwa kama kiongozi mkuu wa nchi, anapaswa kuwa mtu wa kwanza kabisa kulijua hili na kuliweka akilini. Anapandikiza chuki mbaya kutokana na matamshi yake.

Akae chini ajiulize ni kwanini wafuasi wake wote walioonyesha kiburi, dharau na majivuno mbele ya wananchi wameishia kuanguka vibaya? Ajue kuwa watanzania wanachukizwa na watu wa aina hiyo ambapo nathubutu kusema kuwa wameiga kutoka kwake!

Rais Magufuli hana uvumilivu wa kisasa! Hili litapelekea hatari kubwa wakati wa kampeni. Anaenda kufanya kampeni huku akiwa na dola mkononi! Hili ni jambo la hatari kwa kiongozi asiye na uvumilivu wa kisiasa kama Magufuli! Atakutana na kada tofauti huko mitaani, ikiwa hajajifunza kuishi nazo kipindi cha baridi vipi ikifika kipindi cha joto la kisiasa?

Kiongozi aliyeonekana kulia msibani siku moja iliyopita siamini kama ni yule niliyemuona jana! Bado yupo Mtwara anaomboleza!
 
NUKUU:Kiongozi aliyeonekana kulia msibani siku moja iliyopita siamini kama ni yule niliyemuona jana! Bado yupo Mtwara anaomboleza!"". MWISHO.

Huyo mzee ni muigizaji mzuri sana, ni dizain ya akina Joti.

anaweza tamka jambo la kuhuzunisha karibu na kulia, ghafra anaongea jambo jingine muda huo huo na kucheka kwa nguvu kweli.
 
Kuna siku moja mwananchi alimwambia kwamba hali ni ngumu na aachie hela mtaani. Jibu alilopewa aisee ni balaa na jibu la dharau mno.

Yaani hiyo video ikipatikana na ikatumika vilivyo kwenye kampeni panawezekana hata CCM wakapigia kura upinzani.

Inawezekana shoo ya wajumbe ikampata hata yeye.

Mwenye hiyo video aitume humu.
 
Endeleeni kulialia vilaza nyie. Hao si ndio kila siku wanapinga bajeti ya serikali bungeni??? yaani wao ni kupinga tu kila kitu na acha waisome namba.
 
Kuna siku moja mwananchi alimwambia kwamba hali ni ngumu na aachie hela mtaani. Jibu alilopewa aisee ni balaa na jibu la dharau mno. Yaani hiyo video ikipatikana na ikatumika vilivyo kwenye kampeni panawezekana hata CCM wakapigia kura upinzani.
Inawezekana shoo ya wajumbe ikampata hata yeye.
Mwenye hiyo video aitume humu.
Hahah mama mwingine aliomba mh. awaletee huduma ya maji akaambiwa akamwambie mumewe akamletee hayo maji.
 
Endeleeni kulialia vilaza nyie. Hao si ndio kila siku wanapinga bajeti ya serikali bungeni??? yaani wao ni kupinga tu kila kitu na acha waisome namba.

Tuambie ni lini ccm waliunga mkono hoja za wapinzani, ili tujue kuwa ccm haipingi kila kitu. Bajeti ina vifungu vingi, na jibu mwishoni sio la kifungu kwa kifungu, bali ni kwa ujumla wake. Na jibu linapaswa kuwa ndio au hapana. Je unategemea jibu gani kwa bajeti inayobeba vitu vyote kwa pamoja?
 
Hizi kauli hapana, kusema kweli zinaudhi mno mno.

Ni vyema washauri wake wakamwambia ukweli madhara ya hizi lugha.

Wateule wake wamekuwa wakitumia kauli chafu na za kufedhehesha dhidi ya watu hata makabila mengine na hawachuliwi hatua kwani ndio 'mwelekeo' wa aliyewateua.
 
Back
Top Bottom