the horticulturist
JF-Expert Member
- Aug 24, 2012
- 1,959
- 1,894
Kwa maswali na majibu kwa masuala ya kilimo cha mboga, matunda, maua, viungo na dawa.
Wataalam na wakulima tukutane hapa.
==============================================
Kwa kuanza niongelee live barrier, Kiswahili tutasema uzio hai huu huwa ni mtama au ngano inayopandwa kuzunguka shamba kwa mistari miwili (double row). Nafasi ya mtama au ngano moja hadi nyingine hutegemea aina ya mtama au ngano ila unaweza tumia nafasi ya 30 sm kati ya mstari na kati ya mtama au ngano moja na nyingine,hupandwa kwa mfumo wa zigzag.
Faida yake:
Hupunguza magonjwa shambani kwa kupunguza magonjwa kuingia toka mashamba mengine.
HOW: Mdudu muambikiza magonjwa akitoka shamba jiran atakula kwenye kwenye live barrier hivyo kuacha vidudu vya magonjwa pale.
Hasara:
Kila lenye faida lina hasara, kubwa ni gharama ya ziada na lingine ukiacha ikazalisha mtama au ngano itavutia ndege wengi kama zao lako linashambuliwa na ndege basi watashambuliwa na mazao pia,kuepuka toa vikonyo vya kuzaa mtama au ngano ubaki na mmea wenye majani tu.
Karibuni kwa maswali na maoni