Kwa maswali na majibu kwa masuala ya kilimo tu

the horticulturist

JF-Expert Member
Aug 24, 2012
1,959
1,894
Kwa maswali na majibu kwa masuala ya kilimo cha mboga, matunda, maua, viungo na dawa.

Wataalam na wakulima tukutane hapa.

==============================================

Kwa kuanza niongelee live barrier, Kiswahili tutasema uzio hai huu huwa ni mtama au ngano inayopandwa kuzunguka shamba kwa mistari miwili (double row). Nafasi ya mtama au ngano moja hadi nyingine hutegemea aina ya mtama au ngano ila unaweza tumia nafasi ya 30 sm kati ya mstari na kati ya mtama au ngano moja na nyingine,hupandwa kwa mfumo wa zigzag.

Faida yake:
Hupunguza magonjwa shambani kwa kupunguza magonjwa kuingia toka mashamba mengine.

HOW: Mdudu muambikiza magonjwa akitoka shamba jiran atakula kwenye kwenye live barrier hivyo kuacha vidudu vya magonjwa pale.

Hasara:
Kila lenye faida lina hasara, kubwa ni gharama ya ziada na lingine ukiacha ikazalisha mtama au ngano itavutia ndege wengi kama zao lako linashambuliwa na ndege basi watashambuliwa na mazao pia,kuepuka toa vikonyo vya kuzaa mtama au ngano ubaki na mmea wenye majani tu.

Karibuni kwa maswali na maoni
 
Nimependa thead yako, unaweza saidia comon spacing za nyanya, tikiti kabeji vitunguu karoti na bamia (okra)

Nyanya 50-60x75
Tikiti 100-150x150
Kabeji 40-50x40
Vitungu 7-10x15x(30 njia)

Karoti 5x15(x30 njia)
Bamia 45x45

Hizi ni kwa kilimo cha umwagiliaj wa kawaida,kwa drip nyingne zinachange kama nyanya ya drip n 40x40x150 kwa determinate type na 30x30x150 kwa indeterminate type.
Vipimo vyote ni kwa sentimita
 
Asante mkuu umenisaidia, mi nilikua najua tikiti ni 60*60cm leo nimepata ukweli, vipi hapo kwenye nyanya 40*40*150. 150 ni nini?
 
Karibu sana,hapo kwa nyanya ni kwamb tunapanda mistari miwili kwenye tuta moja,inakua nyanya hadi nyanya ndani ya mstari mmoja ni 40sm,nyanya mstari mmoja hadi mwingine kwenye tuta moja nayo ni 40 halafu 150 ni mstari wa tuta hadi tuta ndugu
 
nimekupata mkuu shukrani
 
Spacing ya 150 ni kubwa sana. Kwa hybrid nyanya recommended spacing ni 60 kwa 90 hapa ikiwa na maana mche mpaka mche 60 ma mstari mpaka mstari 90. Kwa nyanya za OPV tumia spacing ya 50 kwa 70.
 
Hapana hujamuelewa muelimishaji. Soma vizuri ufafanuzi wake hapo juu.
 
Baba hizi spacing sio za nyanya ni za mahindi sijawahi ziona bustanini

Sawa boss wangu hapa kwetu Mlali na Mgeta twatumia hizi ili plant population iwe sawa. Siko hapa kupinga
Na katika uzi huu niliona spacing ya 150 toka tuta mpaka tuta ni kubwa pia 40 kwa 40 hizi sio kwa bush nyanya sie hata hoho twatumia 45
 
Spacing ya 150 ni kubwa sana. Kwa hybrid nyanya recommended spacing ni 60 kwa 90 hapa ikiwa na maana mche mpaka mche 60 ma mstari mpaka mstari 90. Kwa nyanya za OPV tumia spacing ya 50 kwa 70.

Ndugu inategemea method gan unatumia kwa umwagiliaji plant population kwa ekari ni nyanya 13 elfu je ni kidogo??tuta la sm 40 tuta hadi tuta ni mfereji huo si tuta height ya tuta Arusha na ninayoitumia ni 45 cm to 60cm from the ground level na kwa flat beds na raise 15 to 25 cm high.unapata picha ya hizo tuta??mpaka hoho za njano na nyekundu ndani ya green house natumia spacing ya 150 cm tuta hadi tuta,kitaalam spacing chache kwa tuta ni 100 cm.Hizo zako ukiweka stakings si unakosa pa kupita ndugu?utapaliliaje,utavunaje?utapgaje dawa??
 
Sawa boss wangu hapa kwetu Mlali na Mgeta twatumia hizi ili plant population iwe sawa. Siko hapa kupinga
Na katika uzi huu niliona spacing ya 150 toka tuta mpaka tuta ni kubwa pia 40 kwa 40 hizi sio kwa bush nyanya sie hata hoho twatumia 45

Hybrid gani mnatumia huko?mnazipata wapi maana wengi wanatumia za maduka ya mbegu ambazo n opv zote
 
Sawa boss wangu hapa kwetu Mlali na Mgeta twatumia hizi ili plant population iwe sawa. Siko hapa kupinga
Na katika uzi huu niliona spacing ya 150 toka tuta mpaka tuta ni kubwa pia 40 kwa 40 hizi sio kwa bush nyanya sie hata hoho twatumia 45

Ndugu ndio maana ya hii sehemu kuelekezana ndugu
 
Sawa boss wangu hapa kwetu Mlali na Mgeta twatumia hizi ili plant population iwe sawa. Siko hapa kupinga
Na katika uzi huu niliona spacing ya 150 toka tuta mpaka tuta ni kubwa pia 40 kwa 40 hizi sio kwa bush nyanya sie hata hoho twatumia 45

Hakika mnatumia opv ndugu wanawadanganya ni hybrid mfano tengeru 97 ni opv ila wauza duka la pembejeo watakueleza n hybrid,nimelima anna f1 na shanti ,anna f1 mbegu ya eka ina cost tsh 270,000 na hupati maduka ya kawaida ndugu.pili pili hoho qsem mche wanauza tsh 300 hoho za njano na nyekundu(ilanga na parsilela),mnatumia hizo ndugu au mnauziwa tu za opvs?
 
Back
Top Bottom