kuna madhara gani kama mwembe mmoja nikau graft aina tofauti za miembe kwenye matawi yake, mf kipande cha chini kiwe embe sindano matawini niunge embe mwaka, bolibo, na mingineyo.
Mkuu naomba utuelezee jinsi ya kuchoma udongo na faida zake
Mkuu naomba kujuzwa, ni mbegu kiasi gani ya vitunguui inaweza tosha eka moja kwa mavuno ya gunia 50-70 kwa eka.
Natanguliza shukrani kwa masaada wako.
Mbegu kiasi cha kg 2.5 za vitunguu zinatosha kwa ekari,tumia nafasi ya kitunguu hadi kitunguu ni 8 sm na mstari na mstari ni 15 sm na baada ya mistari sita unaacha nafasi ya sm 30 ambayo kama utapanda kwa matuta itakua ndio nafasi ya tuta hadi tuta,hii itakua njia yako wakati wa kuhudumia shamba.karibu ndugu
Mtaalamu nashukuru sana kwa majibu mazuri sana,nimekupata barabara kabisa.
Mkuu mbegu wakati wa kusia natakiwa kutawanya random au kwene mstari na natakiwa kuhamisha baada ya muda gani kutoka kitalu kwenda shambani?.
Standard size ya tuta la kitalu na shamba(lakuhamishia) ni kiasi gani?
Natanguliza shukrani, samahani kwa usumbufu mkuu.
the horticulturist;
Naomba unisaidie, hivi drip lines(pipes)huwa wanauza moja ndefu na unakata ww kwa vipimo vyako au inakua ktk vipande? kama iko ktk vipande vina urefu gan? natanguliza shukran
Umenichanganya maana umeongelea drip line na pipes,pipes ni pvc pipes zina urefu wa mita 10 na kwa drip line inauzwa kwa roller ndugu
Hakika mnatumia opv ndugu wanawadanganya ni hybrid mfano tengeru 97 ni opv ila wauza duka la pembejeo watakueleza n hybrid,nimelima anna f1 na shanti ,anna f1 mbegu ya eka ina cost tsh 270,000 na hupati maduka ya kawaida ndugu.pili pili hoho qsem mche wanauza tsh 300 hoho za njano na nyekundu(ilanga na parsilela),mnatumia hizo ndugu au mnauziwa tu za opvs?
unaposema Opv, unamaanisha nini? mtaalamu.
Open pollinated varieties,ni mbegu ambazo si hybrid na zinahitaji pollination(uchavushaji)ili kutoa mazao mara nying hupandwa nnje si kwenye green house,kuna hybrid ambazo huzaa hata bila ya uchavushaji
Nimekupata, nilimaanisha hasa drip lines. ohoo kumbe unanunua roller unakuja kukata mwenyewe kutegemea na shamba lako. hapo sawa. pia tank la lita 1000 litafaa kutumia kwa kilimo cha kabeji kwenye eneo la 500mita za eneo?
asante mtaalamu mimi mwezi wa pili nilipanda nyanya, na niliuziwa mbegu ambayo muuzaji alidai ni Ana f1, lakini cha ajabu ile nyanya ilikua ikishambuliwa sana na magonjwa pamoja na kufuata masharti yote ya upigaji madawa, kwa maelezo yako, napata picha kuwa Ile mbegu huenda ilikua hiyo Opv uliyosema, mwaka huu mwezi wa kumi na plan nifanye tena mradi huu, hivyo ntaomba unielekeze sehemu ntakayo pata hiyo genuine hybrid. mimi niko morogoro. asante
Nunua product yoyote ya kilimo toka kwa muuzaji mwenyewe au authorised dealer,kama ni product ya kibo,balton,syngenta hakikisha umenunua kwa wakala wao au kampuni branch zao mbali na hivyo utakumbana na zilizochakachuliwa ndugu,watanzania ujanja umezidi,pia ukinunua kwao au wakala bei ni rahisi pia