Kwa masikitiko nauona mwisho wa chama changu CCM

mngony

JF-Expert Member
Jul 27, 2012
5,188
6,351
Jambo hili linaloumiza nililiona tangu kuanza kukataliwa kwa mikutano ya siasa na kuletwa kwa sheria mbalimbali kama za takwimu, habari n.k ambazo kiuhalisia lengo ilikuwa kudhibiti ukosoaji na Upinzani na kuongeza kuungwa mkono kwa chama na serikali kwa sababu watu watakuwa wanasikia mambo mazuri yaliyofanyika peke na kujenga mawazo chanya kwa serikali.

Hii ilikuwa kama kucheza kamari kwa sababu inaweza kulipa kisiasa au ikarudi kukuumiza. Kichama mwanzoni haya yalikuwa maamuzi mazuri kwani lile vuguvugu la 2015 na watu wangeachwa waongee muda wowote basi ingehatarisha kupungua kuungwa mkono na wananchi kwa chama na Serikali kwa ujumla.

Lakini sheria hizo na katazo halijakisaidia kuungwa mkono zaidi Chama na serikali kwa ujumla bali limeghairisha tu kwa muda, Chama kimebweteka kikitegemea dola kunyamazisha mawazo tofauti na wakosoaji. Kimeshindwa kujitathmini sera zake na uungwaji wake mkono na wananchi. Matokeo yake kimekuwa 'surprised' muitikio wa watu kwa upinzani kipindi hiki.

Hatujui tuseme nini, maana tulishasema kwa miaka bila kupewa changamoto. Kama tuliwaambia yale yale lakini sasa hivi tunaona kumbe hawajelewa je sasa hivi tutaambia nini cha tofauti? Mtumishi hajapanda daraja tunamwambia tunajenga bwawa, mpinzani anamwambia ni haki yako umeikosa kwa miaka minne . Mwananchi kijijini tutamtajia kuwa mafaniko tumenunua shirika la ndege, mpinzani atamwambia maji hujaletewa miaka miaka minne. Hakuna uchawi hapo.

Upinzani wana kazi rahisi sana,wanazungumza na kufanya yale ambayo watu walizuiwa kwa miaka minne , wananchi wanaona faraja wamepata wa kuyazungunza na kuamsha ari zao. Watu hawakutegemea kuwa wapinzani wangevuta watu na husia zao kiasi hiki. kamari ya kuzuia mikutano na kutofanya siasa ime 'backfire' inatuumiza sisi.

Tungewaacha waongee miaka yote watu wangeona hawana jipya wangezoea tu kama miaka yote. Ni wazi wananchi wana mengi sana wameweka moyoni, wana matatizo wana manung'uniko mengi, si waalimu, si wanafunzi, si wafanyabiashara wala si wakulima. Sote tunajua hali halisi. Watu wanavinyongo moyoni ila pakusema hakuna.

Lakini lingine, ikatokea chama kikaendelea kushika dola baada ya uchaguzi 2020. Na aliyepo akaondoka 2025, uwezako mkubwa ni hizi sheria makatazo na hatua za kuzuia mawazo mabadala mengi yataondolewa, hapo sasa ndipo itakapokuwa rasmi chama kimemalizika.

Hebu fikiria miaka hii minne walimu, wafanyabiashara, wanafunzi vyuo vikuu wakulima na watumishi kwa ujumla wangekuwa huru kutoa madukuduku yao, fikiria vyombo vya habari vinatoa fursa sawa kwa wapinzani kusikika, fikiria press comference hazizuiwi n.k nadhani tunapata picha halisi kuwa chama kipo katika hali mbaya ya uungwaji mkono kisiasa. Tukitoboa 2020 basi 2025 napata mashaka sana.

Lissu tumtengeneza wenyewe, Lissu alishamkosoa sana JK kama Rais mwenyekiti wa Chama na kama mtu binafasi lakini tuliomuoma kama tu mpinzani anayeongea sana kama wengine tu , ikulu aliitwa na chai anakaribishwa. Ila sasa hivi Lissu anaonekana shujaa mbele ya wananchi, kwanza ame survive assasinationa attempt na mbili anazungumza yale madukuku yaliyojaa moyoni. Lissu wa sasa sio yule ana nguvu kubwa ya ushawishi, ni kwa sababu tu anazungumza yanayowagusa wananchi. Lissu anatisha.

Busara inahitajika kunusuru taifa, tusilazimeshe mambo, Taifa letu litabaki vyama vitakuja na kuondoka. Lazima tukubali ukweli kuwa iko siku chama kitatoka madarakani, sisi wa kwanza kwa vyama vya ukombozi kutolewa kwenye dola. Na tujiandae kisailolojia kuwa siku za kuwa chama dola zimekaribia mwisho, tukijisahaulisha haya ndio tunahamaki badala ya kukabiliana nao kwa hoja tunafanya ya tofauti.

Chondechonde yaliyotokea Hai ni aibu na fedheha kubwa yasijirudie kwa sababu mwisho wake sio mzuri, tujiulize kwa nini anavutia watu wengi, kwa nini wanamsapoti, kwa nni wanamsikiliza. Tufanye propanga na mbinu zingine ila sio ya Hai. Uzalendo ni kusimama na Taifa sio na Chama au Mtu, tusiwe tayari kunyamazisha wapinzani kwa njia ambazo zitagharimu Taifa wala tusiwe tayari kuona Taifa linaangamia kwa sababu tu kulinda chama au mtu.

Sidhani kama kuna tafsiri mpya ya Uzalendo.

Tanzania yetu ni moja.
 
Tatizo kubwa la ccm ni kumruhusu Mwenyekiti wenu kuwa bz na media kwa miaka 4 uku mkiwaziba wapinzani mikopo. Leo hii tunakwenda kuanza kampeni, Mgombea wenu ladha yake machoni na masikioni kwa wapigakura imezoeleka, wakati Tundu Lissu amekuja kama chakula au kinywani kipya chenye kuvutia na kupendeza machoni pa wengi, hapo kila mtu atataka kumwona na kumsikiliza.

Sishangai ccm kuwakusanya wanamuziki zaidi ya 40 na kuwazungusha ili wawavutie watu waje kwenye mikutano yao. Hiyo ni dalili ya chama kilichoishiwa na kufilisika kifikra.

Mchimba kaburi huingia mwenyewe, hii hali ya sasa ya kisiasa mliitengeneza wenyewe na sasa mnapaswa muikabili
 
Mleta mada umeongea maneno mazito sana
Tatizo la Jiwe ni kupenda kupendwa, kutiiwa kwa lazima. Yaani haimuingii akilini kwa nini asipendwe wala kukubaliwa kila anachokitaka yeye!
Kwa hiyo ndiyo maana anabana kila outlet ya kumkosoa.
Anajidanganya
Tujifunze kujenga hoja na kueleza mazuri kuliko kuzuia watu wasiseme
 
Umeongea adi point ya mwisho Mzee Ccm inatakiwa wakubali siasa za vyama vingi mbona Wameongea sana miaka mi nne na wamefanya mengi sana mazuri lakini bado hawajiamini.
 
You can fool some people for some time but you cannot full people all the time.

Time will tell , haya yote yana mwisho!
 
CCM huwa wanaonekana Kama mgonjwa mahututi kabla ya uchaguzi lkn baada ya uchaguzi wanakuwa wezi wa kura.....ni mtazamo wa wapinzani. 🤣
 
CCM mi chama kikongwe.... Na akili za mkongwe au mzee Ni Kama mtoto mdogo... Kifupi akili zimedumaa.

Wanazo mbinu za kizamani za kutoa rushwa na ubabe na sio kushindana kwa hoja za maendeleo..
 
CCM kama imeshindwa miaka yote 59 sasahivi inajipya lipi?

Ni aibu ya Karne tokea Uhuru Hadi leo mtu anataabika khs upatikanaji wa maji Tena anaishi Mwanza mjini au Dar... Je wa huko Kijijini sijui Ana Hali gani..
 
31 Reactions
Reply
Back
Top Bottom