Kwa masikitiko makubwa naomba wana JF tuangalie kwa makini video hii.......!! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kwa masikitiko makubwa naomba wana JF tuangalie kwa makini video hii.......!!

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by DON KILLUMINATI, Oct 14, 2012.

 1. DON KILLUMINATI

  DON KILLUMINATI Senior Member

  #1
  Oct 14, 2012
  Joined: Jan 2, 2011
  Messages: 190
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Hebu tujikumbushe walivyofanywa Waumini wa dini ya kikristo wanaosali Efatha, halafu tulinganishe suala hili lingeweza kufanyika kwa namna hii iwapo waumini hawa wangekuwa ni Waislam????

  Ifike wakati na sisi Wakristo tuamke sasa, maana huu ni uonevu wa wazi wazi kabisa kwenye Nchi yetu sote, ni kwa nini Serikali na Jeshi la polisi wanawapendelea Waislam??? Ni kwa nini Wakristo wanaonewa kiasi hiki??


   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 2. PhD

  PhD JF-Expert Member

  #2
  Oct 14, 2012
  Joined: Jul 15, 2009
  Messages: 3,819
  Likes Received: 818
  Trophy Points: 280
  Sitokaa nimpende polisi wa aina yeyote Tanzania kwa ukatili wanaoufanya kwa masikini wa TANZANIA, to hell siwezi kuwa mnafiki na upuuzi kama huu
   
 3. Mwanaukweli

  Mwanaukweli JF-Expert Member

  #3
  Oct 14, 2012
  Joined: May 18, 2007
  Messages: 4,451
  Likes Received: 288
  Trophy Points: 180
  Kwanza tujulishe:

  Ni kweli watu wa Mwingira walibomoa na kuchoma nyumba za Afroplus?

  Viongozi wa Dini kama Mwingira wanapaswa kujifunza kutatua matatizo yao kwa kufuata sheria, na si kujichukulia sheria mkononi.

  So far, Mwingira na Efatha si mfano mzuri!
   
 4. DON KILLUMINATI

  DON KILLUMINATI Senior Member

  #4
  Oct 14, 2012
  Joined: Jan 2, 2011
  Messages: 190
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  To Hell!!!!
  Wawe wamebomoa au hawajabomoa, hii ilikuwa kesi ya kisheria (Kimahakamani) We umeona unyama waliofanya hawa polisi na kupiga mabomu kanisani, tena unawapiga watu ambao hata hawapambani na mtu yoyote, kulikuwa na haja gani kuwafanyia unyama huu watu ambao hawana silaha wala hawajaonesha kupambana kwa namna yoyote ile??
   
 5. Mwanaukweli

  Mwanaukweli JF-Expert Member

  #5
  Oct 14, 2012
  Joined: May 18, 2007
  Messages: 4,451
  Likes Received: 288
  Trophy Points: 180

  Mkuu, hata jinsi ulivyoanza jibu lako tu, "To hell!"

  Kama ndio namna mlivyo, na mnategemea mko juu ya sheria, huo si ukristo.

  Ni uhalifu.

  Unathibitisha kuwa Polisi walifanya vizuri kushughulikia wahalifu.

  Mimi ni mkristo pia lakini kamwe sitatetea wakristo wa namna yenu.
   
 6. DON KILLUMINATI

  DON KILLUMINATI Senior Member

  #6
  Oct 14, 2012
  Joined: Jan 2, 2011
  Messages: 190
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Kaa kimya kama huelewi ninachozungumzia, wewe una draw conclusion kwa neno langu (to hell) au ulichokiona kwenye video?? Mi nazungumzia uhalisia wa kilichofanywa na polisi, wangekuwa ni waumini wa Kiislam hao polisi wangethubutu??
   
 7. PhD

  PhD JF-Expert Member

  #7
  Oct 14, 2012
  Joined: Jul 15, 2009
  Messages: 3,819
  Likes Received: 818
  Trophy Points: 280
  wewe ni muhalifu kama kamuhanda, ni sheria ipi inamruhusu ofisa wa polisi kumrukia raia mateke na kumtoa damu eti kwa sababu amevunja sheria ( mtuhumiwa), unachotakiwa kama polisi ni kumkamata mtuhumiwa sio kumpiga na mambomu, huu ni wehu tupu.
   
 8. Mwanaukweli

  Mwanaukweli JF-Expert Member

  #8
  Oct 14, 2012
  Joined: May 18, 2007
  Messages: 4,451
  Likes Received: 288
  Trophy Points: 180
  Nacheka hapo pekundu!!!

  Mkristo hawi na jazba kama wewe.

  Nimeona kwenye video. Wamewahoji na upande wa pili wale walinzi wa Afroplus na wameelezea upande wao kilichotokea.

  Hao waliochoma moto na kubomoa hata kama walikuwa kanisani, ilikuwa ni sawa wafuatwe huko na kukamatwa kwani ni wahalifu.
   
 9. DON KILLUMINATI

  DON KILLUMINATI Senior Member

  #9
  Oct 14, 2012
  Joined: Jan 2, 2011
  Messages: 190
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  You got no heart brother.

  Umewezaje ku prove kuwa waliokuwa humo kanisani ndo waliobomoa wakati ubomoaji ulifanyika usiku na hii ilikuwa alfajiri ?? That is church, kuna waumini ambao wanaenda kwenye maombi asubuhi? Waliwezaje tofautisha kwamba hawa ni waharifu na hawa wamekuja kuabudu?
   
 10. Mwanaukweli

  Mwanaukweli JF-Expert Member

  #10
  Oct 14, 2012
  Joined: May 18, 2007
  Messages: 4,451
  Likes Received: 288
  Trophy Points: 180
  Our Divine Master, Jesus Christ, who is not exacting, reminds all His would-be followers, without distinction, that they must learn the lesson of Humility, get it well by heart, and into the heart; for Humility is the alphabet out of which every other virtue is formed and built up.

  It is the soil of the garden of the soul, "the good ground" on which the Divine Sower goes forth to sow His seed. It is in the school of Christ, and from the lips of Christ Himself that we must learn Humility. "Learn of Me, because I am meek and humble of heart. Mt. 11:29 "

  By following the Master Himself, by studying His Own Heart, we have to acquire, to appreciate and to practice this first, this vital, this vitalizing, energizing virtue, without which no man can hope to make any progress at all on the way to heaven.
   
 11. Mwanaukweli

  Mwanaukweli JF-Expert Member

  #11
  Oct 14, 2012
  Joined: May 18, 2007
  Messages: 4,451
  Likes Received: 288
  Trophy Points: 180
  Tangu mwanzo unaonesha kiburi kikubwa ambacho ni kinyume na Mt. 11:29.

  Kuna matendo mengi tu ya kihalifu yamefanywa na waumini wa Efatha, na Mtume Mwingira ikiwemo Mwingira kuiba wake za watu eti anawafanyia uponyaji.

  Efatha ni mfano mbaya wa ukristo.
   
 12. Mwanaukweli

  Mwanaukweli JF-Expert Member

  #12
  Oct 14, 2012
  Joined: May 18, 2007
  Messages: 4,451
  Likes Received: 288
  Trophy Points: 180
  Unanihukumu mimi na Kamuhanda, lakini unawafumbia macho waliobomoa Afroplus!

  Watetezi wa Efatha bado mnaendelea na tabia ya kupingana na mafundisho ya Bwana Yesu. Kumbuka Yesu anasema "Msihukumu, nanyi hamtahukumiwa; msilaumu, nanyi hamtalaumiwa; achilieni, nanyi mtaachiliwa" Lk. 6:37
   
 13. PhD

  PhD JF-Expert Member

  #13
  Oct 14, 2012
  Joined: Jul 15, 2009
  Messages: 3,819
  Likes Received: 818
  Trophy Points: 280
  mimi sio mkristo wala muislam, na siongozwi na vifungo vya kimadhehebu, naongozwa na natural justice ambayo haimfungi mtu zaidi ya kutoa mwito wa kuetendewa sawa kwa watu wote kama ambavyo wewe ungependa kutendewa, mnajifunga na vifungo vya kimadhehebu ndio sababu mnawatendea wenzenu isivyo, karl marx aliwahi kuisema dini ni kama bangi ( opium of mind), sina muda na nunukuu zako , imani bila matendo ni uchwara tu, matendo ni kutenda haki kwa wote, wewe na kamuhanda kwa sababu ya tabia zenu kinachowafaa ni kama cha huyo mwenzenu tu.
   
 14. Mwanaukweli

  Mwanaukweli JF-Expert Member

  #14
  Oct 14, 2012
  Joined: May 18, 2007
  Messages: 4,451
  Likes Received: 288
  Trophy Points: 180
  Ungeongozwa na natural justice ungetambua kuwa hata kanisa linapaswa kutatua migogoro yake kwa kufuata sheria. Sheria gani iliyotumiwa kubomoa na kuchoma kama Efatha walivyofanya pale Afroplus?

  Natural justice hiyohiyo unayosimamia ingekupeleka kuangalia na haki ya Afroplus, lakini tayari una jazba la upande mmoja, hiyo si dalili ya natural justice.
   
 15. Mwanaukweli

  Mwanaukweli JF-Expert Member

  #15
  Oct 14, 2012
  Joined: May 18, 2007
  Messages: 4,451
  Likes Received: 288
  Trophy Points: 180
  Hivi mnasemaje kuhusu na haya yanayohusu Efatha na Mtume na Nabii Mwingira?

  Na Elvan Stambuli
  Tuhuma nzito ya ubakaji imemwangukia Nabii na Mtume wa Kanisa la Efatha la Jijini Dar es Salaam, Josephat Elias Mwingira (pichani) ambapo Wakili Eliya Hubert Mbuya amedai katika Mahakama Kuu Kitengo cha Ardhi kuwa, kati ya mwaka 2005 na 2009, mtumishi huyo wa Mungu alimbaka mkewe.

  KESI YA MSINGI
  Kesi ya msingi yenye namba 226/2010 ilifunguliwa mwaka jana na Nabii Mwingira ikimtaka Wakili Mbuya ambaye ni mlalamikiwa awe amefika mahakamani hapo Novemba 10, 2011 mbele ya Jaji Nchimbi ili ajibu madai ya mlalamikaji anayemshitaki kwa suala lenye utata wa umiliki wa kiwanja nambari 548 (a) kilichopo Kawe, Dar es Salaam.

  Mwingira anamlalamikia Mbuya kwa kuvunja mkataba wa kumpa sehemu ya kiwanja hicho ambacho tayari nabii huyo amejenga nyumba na kuboresha miundombinu kwa thamani ya shilingi 1,000,000,000.
  Katika majibu ya Mbuya yayowasilishwa mahakamani hapo na Kampuni ya Mawakili ya Ngalo (Ngalo and Advocates), Mbuya amedai kuwa mke wake alibakwa na Mwingira, hivyo akaghairi kutoa kipande cha ardhi kwa mlalamikaji kama alivyofanya awali.

  MWANZO WA SAFARI
  Akieleza kwa urefu sakata hilo, Wakili Ngalo alidai kuwa, Julai 2003, Mbuya akiwa na mkewe Betha alihudhuria semina iliyoendeshwa na Mwingira katika Kanisa la Efatha, Mwenge Jijini Dar es Salaam ambapo kutokana na mahubiri yake, waliamua kuokoka na kuwa wanachama wa kanisa hilo. Wakili Ngalo akaongeza kuwa, Mbuya alidai kwamba Oktoba 2003, katika kanisa hilohilo, iliendeshwa semina nyingine iliyokuwa chini ya Ibrahim Mlay na mlalamikiwa (Mbuya) alichangia basi dogo aina ya Toyota Coaster.

  Alisema kuwa baada ya muda Mlay aliendesha semina tena katika kanisa hilo ambapo Mbuya na mkewe walihudhuria na walichangia kipande cha ardhi kilichopo Ploti Namba 548, Kawe Beach. Sehemu ya majibu hayo ya kinga ikasema kuwa mwaka 2005, Mwingira alimtaka mlalamikiwa kutafuta mnunuzi wa kiwanja hicho ambapo fedha ambazo zingepatikana, zingejenga makanisa ya Efatha sehemu nyingine.
  Ikadaiwa kuwa, alijitokeza mnunuzi aliyekuwa tayari kulipa shilingi 176,000,000, mwingine akiwa tayari kwa kulipa shilingi 450,000,000 kwa lengo la kujenga hoteli. Ikasemekana kwamba, Novemba 2006, mlalamikaji alimwambia mlalamikiwa kuwa Mungu alimwonesha maono yakimtaka mlalamikiwa asikiuze kiwanja hicho, bali amkabidhi mlalamikaji hivyo amwandalie ‘dokumenti' za makabidhiano ya kiwanja hicho, naye akatii.

  DALILI ZA UBAKAJI
  Akizungumzia madai ya mkewe kubakwa, Wakili Ngalo alisema kuwa mwaka 2009, mke wa Mbuya alitubu kwa mumewe kwamba siku moja mwanaume huyo akiwa kazini, yeye alizini na mtumishi huyo wa Mungu kwenye ndani ya nyumba yao.
  Sehemu ya waraka huo ikasema kuwa, mke huyo aliamua kuchukua uamuzi huo baada ya kupata ugonjwa mbaya (tunausitiri) uliomsumbua kwa muda wa miaka mitatu ambapo katika kumwomba Mungu, aliisikia sauti ikimwambia ili apone lazima atubu dhambi ya uzinzi kwa mumewe.

  MUME NA MKEWE WANAMKABILI MWANGIRA
  Baada ya kusikia hayo, mlalamikiwa akiwa na mkewe walikwenda kumkabili mlalamikaji ofisini kwake ambapo walimkuta akiwa na mkewe. Kwa mujibu wa wakili huyo, mke wa mlalamikiwa aliweka wazi uhusiano wake wa mapenzi na mtumishi huyo wa Mungu ambapo mke wa mlalamikaji naye akasema amewahi kusikia tetesi za kuwepo kwa uhusiano huo.
  "Mke wa mlalamikiwa alimuomba radhi mke wa mlalamikaji ambapo alimsamehe lakini mlalamikaji hakujibu chochote," ilisema sehemu ya nyaraka ya Wakili Ngalo iliyopo mahakamani.

  NINI KIINI CHA TATIZO?
  Aidha, Mbuya alinukuliwa na wakili wake akidai kwamba kwa sababu walikuwa wakihudhuria hafla mbalimbali za maombi kanisani hapo na kutoa michango hiyo ndiyo ilikuwa kivutio cha Mwingira kumtembelea nyumbani kwake mara kwa mara na kutenda hayo.

  KWANINI MUME ALIGHAIRI KUTOA KIWANJA?
  Nyaraka hizo zimesema kuwa kutokana na Mbuya kugundua uhusiano huo usiofaa ambao mke wa mlalamikaji alikiri kuusikia, aliamua kufuta uamuzi wake wa awali wa kugawa ardhi aliyokusudia kumpa Mwingira na akaifahamisha Wizara ya Ardhi, mlalamikaji pamoja na mkewe (Mbuya). Wakili Ngalo amesema Mbuya aliiomba mahakama hiyo kuitupilia mbali kesi hiyo na mlalamikaji aamuriwe kulipa fidia.

  ANACHOTAKA NABII MWINGIRA
  Kwa mujibu wa nyaraka mbalimbali za kimahakama (nakala tunazo), Mwingira alifungua kesi Mahakama Kuu Kitengo cha Ardhi Agosti 23, 2010 akiitaka itoe amri ya utekelezwaji wa kile alichokiita ‘mkataba wa ugawaji eneo.'
   
 16. PhD

  PhD JF-Expert Member

  #16
  Oct 14, 2012
  Joined: Jul 15, 2009
  Messages: 3,819
  Likes Received: 818
  Trophy Points: 280
  unaweza kuthibitisha kuwa hao wanaopigwa na polisi ndio waliobomoa hapo afro Plus, polisi sio mahakama, kama ishu ni kubomoa wakamatwekwa utaratibu waepeleke mahakamani , mahakama ifanye kazi yake ndio natural justice hiyo, vipigo vinavyofanywa na polisi kwa watuhumiwa sio haki, naona wewe na mmiliki wa afro plus mliwahonga polisi ili kufanya udhalimu, sioni mantiki ya wewe kujificha kwenye kivuli kuwa una dini, UNAFIKI. sijui unakunywa bia gani nikuagizie wengine tunajifariji kwa yanayoanza kuwapata polisi pia.
   
 17. Mwanaukweli

  Mwanaukweli JF-Expert Member

  #17
  Oct 14, 2012
  Joined: May 18, 2007
  Messages: 4,451
  Likes Received: 288
  Trophy Points: 180
  Wala mimi sina uhusiano na Afroplus.

  Video imewekwa, tumeiona.

  Video inaongea kuhusu Polisi kupiga waumini wakiwa kanisani, lakini pia inaongelea kuhusu ubomoaji na uchomaji wa Afroplus.

  Mimi nimetaka kukuwekea na hoja za upande wa pili. Hapa si lazima wote wawe upande wako.

  Inanisikitisha kuwa unafurahia kifo cha Kamanda wa Polisi wa Mwanza. Kama ni mkristo wewe ungejua hupaswi kumhukumu Marehemu Barlow kwa kosa la Kamuhanda, wala kosa la watu wawili kulifanya kosa la wote na kuhukumu wote. Natural justice unayoiongelea ndio hiyo?
   
 18. Mwanaukweli

  Mwanaukweli JF-Expert Member

  #18
  Oct 14, 2012
  Joined: May 18, 2007
  Messages: 4,451
  Likes Received: 288
  Trophy Points: 180
  Jesus Christ calls us all into His school to learn, not to work miracles nor to astonish the world by marvelous enterprises, but to be humble of heart. "Learn of Me, because I am meek and humble of heart." [Matt. 11, 29]

  He has not called everyone to be apostles, preachers, prophets or pastors, nor has He bestowed on all the gift of restoring sight to the blind, healing the sick, raising the dead or casting out devils, but to all He has said: "Learn of Me to be humble of heart," and to all He has given the power to learn humility of Him.

  Innumerable things are worthy of imitation in the Incarnate Son of God, but He only asks us to imitate His humility.

  What then? Must we suppose that all the treasures of Divine Wisdom which were in Christ are to be reduced to the virtue of humility?

  Absolutely Yes! Humility contains all things because in this virtue is truth; therefore God must also dwell therein, since He is the truth.
   
 19. PhD

  PhD JF-Expert Member

  #19
  Oct 14, 2012
  Joined: Jul 15, 2009
  Messages: 3,819
  Likes Received: 818
  Trophy Points: 280
  shauri yao POLISI, Tanzanians are tired, naongelea natural justice kwa wote ambayo polisi wameivunja hivyo sina muda wa kumpenda polisi yeyote hata wakiondoka wote leo kwangu sawa tu, nilikuwa Dar es Salaam wakati wa SENSA nikawakuta polisi maeneo ya kijitonyama wameingia kwenye nyumba moja wamembeba kama mzigo wa kuni mzee mmoja mwenye zaidi ya miaka 70 eti kisa anahamasisha waislam kugomea SENSA, nilimwambia dereva wangu asimame nikamwambia yule askari kiongozi anatoka Oystrebay, nilimuuliza kwa wanayotenda ni kama vile mzee yule ana silaha, nikawambia huu sio utaratibu ndio akaamrisha askari wake wawachukue watuhumiwa kwa utaratibu. Pengine angeuwawa yule mzee na tungeambiwa alikuwa na vitu vyenye Ncha kali, hiyo mass protest unayoiona ya wananchi wengi kufurahia kifo cha RPC mwanza ndio message yenyewe kuwa wananchi wanonyesha hisia zao, ni vile tu nao hawana silaha, keep thinking within the context,Vijana wa mjini wanasema KIFO ni mwisho wa mbwembwe POLISI hawalijui hilo.
   
 20. Ukwaju

  Ukwaju JF Bronze Member

  #20
  Oct 14, 2012
  Joined: Oct 19, 2010
  Messages: 8,287
  Likes Received: 810
  Trophy Points: 280
  Hawa Ephata na Mwingira siwaamini na tulishachangia sana humu JF kuhusu hicho kiwanja na kipigo cha Polisi
  Muulizeni Mchungaji Mtikila alipopapaswa Makalio hivi bila ya Polisi na Mahakama hawa Maaskofu uchwara wangemaliza wake zetu na viwanja
   
Loading...