Kwa mara ya mwisho Rais Kibaki alienda wapi na lini ?

Lunyungu

JF-Expert Member
Aug 7, 2006
8,873
1,898
Baada ya kukaa na kujiuliza ni kitu gani kinamfanya JK atumie mapesa yetu namna hii kwa fujo kubwa kwa jina la kwenda kuomba mara kuleta Sullivan nk , nimejiuliza kuhusu Kibaki wa Kenya mara ya mwisho alienda wapi .Maana tangia achukue Nchi ilikuwa na hali mbaya sana yeye katulia ana inyoosha kesha hadi hapo ilipo lakini JK hata sijui. Hebu naombeni mnipe rekodi ya Kibaki na baadaye Museveni tujue inakuwaje hapa .
 
Lunyungu aka - UWT:
Alikwenda Kampala, Uganda; mkutano wa CHOGM, na hakulala shauri ya kampeni.

Kibaki kaifanyia Kenya kazi nzuri kiuchumi; lakini ameangushwa na washikaji/walarushwa na ukabila alioshindwa kuuonea hata aibu.

Mambo haya ya uongozi na kuwepo kwa uchumi mzuri naona bahati nayo inahitajika! Kwani ni kitu gani mhimu na cha kipekee sana alichokifanya katika hii miaka mitano, hadi uchumi wa Kenya uwe ni tofauti kabisa na ule aliouacha Moi? Structures zilizokuwepo ni zile zile alizoziacha Moi; isipokuwa hilo la watoto wa primary kutolipia karo! nini lingine?.....labda kuanza kufunguliwa kwa misaada?
 
Nina ndugu zangu huko Kenya wanamtania Kibaki, badala ya kutamka jina lake uzuri Mwai Kibaki, wao wanasema "Moi Kabaki". Na sikushangaa "profesa" Moi alipoamua kukigeuka chama chake cha KANU kilichomtunza madarakani miaka mingi, na kuamua majuzi kumfanyia kampeni Kibaki. Moi anataka iendelee kuwa "Moi Kabaki".
 
wewe MOI ni undisputable STRATEGIST leader in east africa...ana makusudi kumshauri uhuru asigombee ..anajua kuwa kwa kuwa kura za kenya zinapigwa kikanda na kwa kuwa kikuyu ndio jamii kubwa ..hakutaka wagawe kura kwa kibaki na kenyatta...akijua kwamba mwaka 2012 hakuna mwanasiasa atakayekuwa amekomaa na kuwa fresh kimawazo kumshinda kenyatta..

amemuunga kibaki mkono sasa ili kenyatta awe rais wa kenya mwaka 2012.
 
Na strategy hii je, inayosemwa kuwepo:
1.Kibaki rais, hadi 2012
2. Uhuru Kenyatta - Makamu wa Kibaki hadi 2012, kupitia PNU, ambayo Kanu ni coalision memba wake. Na kumbuka Kibaki kaweka siri, hakutaka kumtangaza mgombea mwenza hadi sasa.
3. Uhuru Kenyatta - Rais 2012 na kuendelea
4. Gedion Moi, au Jonathan Moi, au yule mwingine (wote wanagombea ubunge sasa hivi) Makamu wa Rais wa Kenyatta

Hapo itakuwa ni Dynasty tosha.
 
wewe MOI ni undisputable STRATEGIST leader in east africa...ana makusudi kumshauri uhuru asigombee ..anajua kuwa kwa kuwa kura za kenya zinapigwa kikanda na kwa kuwa kikuyu ndio jamii kubwa ..hakutaka wagawe kura kwa kibaki na kenyatta...akijua kwamba mwaka 2012 hakuna mwanasiasa atakayekuwa amekomaa na kuwa fresh kimawazo kumshinda kenyatta..

amemuunga kibaki mkono sasa ili kenyatta awe rais wa kenya mwaka 2012.

Ni mawazo potofu ya Moi yaliyosambatarisha KANU kwenye uchaguzi wa 2002. Yaani unataka kuniambia akina Saitoti, Murungi, Murungaru, Mwiraria, Karua, Kibwana, Mukhisa na wengineo watakubali kumpisha Kenyatta agombee? Walioondoka KANU mwaka 2002 na kumwachia Moi KANU yake kisa ilikuwa ni kumteua Kenyatta agombee na hoja ilikuwa ni kwamba he was too junior kwao, ina maana hoja hiyo itakuwa imekwisha ifikapo 2012???

Swala la kugawana kura liko pale pale. Kama Kenyatta angekuwa na akili wala asingekubaliana na Moi. Moi anachofanya ni kutetea maslahi yake na wanae. Maana anajua kwamba Raila akiingia madarakani hawatapona lazima ufisadi walioufanya miaka ya nyuma utafufuliwa na kufanyiwa kazi. Kwa hiyo agenda ya Moi ni kulinda maslahi yake binfasi na ameingia rasmi kwenye kampeni kwa ajili ya kummaliza Raila ili Kibaki apate kura nyingi. Kama Kenyatta angeingia kwenye kinyang'anyiro ina maana kwamba kura za Central wangezigawana na hivyo kuongeza chances za Raila kushinda.

Kwa kifupi kama Kenyatta ameahidiwa kupewa ugombea 2012 na akakubali yatakuwa ni yale yale ya NARC ambapo Kibaki aliahidi kukaa ofisini kwa term moja na aliponogewa akaona aongeze term ya pili. Hapo ndipo Kenyatta anapotumika kama ride ya kumrudisha Kibaki Ikulu huku akiwa na matumaini ya kupewa nafasi come 2012.

Wanasiasa wa PNU wengi wao wana kiu ya kugombea urais na ndiyo maana Kibaki aliyumbishwa sana na hakujua angegombea kupitia chama gani. PNU si chama, ila vehicle ya kumrudisha Kibaki ofisini na baada ya hapo itasambaratika na kila chama kitaanza kuwa na mikakati yake ya kuweka mgombea urais ifikapo 2012. Angalia uteuzi wa wagombea ubunge jinsi ilivyokuwa tatizo, kila chama kinataka kuweka mgombea wake kwa mwavuli wa PNU, hiyo ni dalili tosha kwamba vyama vina nguvu, na ninajua baadhi ya vyama vimeshindwa kuweka wagombea kwa kuwa vilikuwa kwenye coalition government na hivyo wamemuonea aibu rais aliyewapatia ulaji katika kipindi cha miaka 5. Lakini kama Kibaki angekuwa anamaliza term ya pili basi mwaka huu ingekuwa balaa kubwa sana na Raila angeingia Ikulu kiulaini sana, maana kungekuwa na wagombea wengi sana ambao wangegawana kura na kumfanya Raila ashinde kirahisi.

Tusubiri 27/12 tuone mwisho wake!
 
MOI ni undisputable STRATEGIST leader in east africa...

I believe you bro, Moi aliwanyima KANU uongozi kwa makusudi kabisa wakati anaondoka, ndio wameanza kumshitukia sasa na bado anaendelea kuwaongoza kwa pembeni, what a political genius,

Mimi ninazimia na huyu mkuu, toka ile siku pale Arusha, uso kwa uso alipowaita Buyoya na Kagame, kuwa ni thugs! That was bold.
 
Ni mawazo potofu ya Moi yaliyosambatarisha KANU kwenye uchaguzi wa 2002.

Mkuu kweli unaaamini Moi, alitaka kuwaachia KANU uongozi? Ili the West waendelee kumsakama kuhusu hela zao? Wewe huoni kuwa ilikuwa ni strategy ya kuwaondoa the West mgongoni kwake na it worked, kwa kuwapa the so called "Upinzani", wewe kweli unaamini kuwa Saitoti anaweza kwenda against Moi!

Kwa nini Kibaki mpaka leo hajamfikisha Moi, kwenye sheria na wakatio ushahidi wote upo clear? Hivi unajua Moi bado anatesa tena hata kuliko Kibaki mwenyewe rais wa Kenya?, na hawezi fanya kitu chochote!

Mkuu Moi, ni sungura mjanja huyo, na ni wachache sana Afrika!
 
Moi.... his strategic days are numbered. Raila is taking over this year. Kibaki is out and KANU is out.....l
 
Funny,
Watu wanasifia Moi mwizi. LOL. Ila mafisadi wabongo wanasakamwa. Waafrika bana. We need to make up our minds.
Kiongozi akiondoka madarakani bila kuiba, tunamkandya. Akiiba, tunamsifia.
Haya.
 
Watu wanasifia Moi mwizi. LOL. Ila mafisadi wabongo wanasakamwa. Waafrika bana. We need to make up our minds.

Mkuu tunasifia uwezo wake kisisasa, ambao hauhusini kabisa na wizi wake, Mrema naye at one time alikuwa na uwezo mkubwa kisiasa na tulimsifia, sio kwamba hatukujua kuwa na yeye ni FISADI au mwizi, no tulikuwa kama sasa tunasifia kipaji chake kisiasa, tatizo ni kwamba kina Karamagi hata vipaji vya siasa hawana,

labda hapo ndipo unahitaji ku-make up your mind mkuu, betweeen kuhusu kuheshimu kipaji cha binadamu na kukemea ufisadi wake, maana kila kimoja kina season na time yake.

Ahsante Mkuu.
 
Watu wanasifia Moi mwizi. LOL. Ila mafisadi wabongo wanasakamwa. Waafrika bana. We need to make up our minds.

Mkuu tunasifia uwezo wake kisisasa, ambao hauhusini kabisa na wizi wake, Mrema naye at one time alikuwa na uwezo mkubwa kisiasa na tulimsifia, sio kwamba hatukujua kuwa na yeye ni FISADI au mwizi, no tulikuwa kama sasa tunasifia kipaji chake kisiasa, tatizo ni kwamba kina Karamagi hata vipaji vya siasa hawana, labda hapo ndipo unahitaji ku-make up your mind betweeen kipaji na ufisadi.

Ahsante Mkuu.

Mkuu, with all due respect. Huwezi kuongelea siasa ya Moi bila kuongelea ufisadi wake. Na siwezi nikamsifia mwizi wa kiafrika. Mobutu alikuwa mjanja pia ku-survive miaka yote hiyo...pia alikuwa fisadi. So was Kamuzu Banda. Siwezi kuwasifia hao.
Nyerere alikuwa mzuri kisiasa lakini sio fisadi.
As kuhusu siasa na ufisadi, sijaona mwanasisa wa kiafrika wa sasa hivi wa kumsifia. So, sihitaji kumake-up mind mkuu.
 
Siwezi kuwasifia hao.
Nyerere alikuwa mzuri kisiasa lakini sio fisadi.
As kuhusu siasa na ufisadi, sijaona mwanasisa wa kiafrika wa sasa hivi wa kumsifia. So, sihitaji kumake-up mind mkuu.

Mkuu heshima mbele, naona tunahitaji kukubali kutokubaliana, maana sio yote unayoaamini wewe na sisi wote ni lazima tuamini hivyo hivyo, inaonekana kuwa ndio tatizo hapa, anyways mimi ninaendelea kuheshimu vipaji vya viongozi wetu, maana kuna kina Sengor, waliokuwa wezi lakini walileta maendeleao kwa wananchi wao pia, Mwalimu hakuwa fisadi, lakini nafikiri unajua aliyotuachia!
 
I think is not fair kucompare kati ya kibaki na JK. Both this presidents are facing different turmoil in their leaderships. JK anaface big corruption, lack of leadership, wrong strategic planners and many other problems. Wakati mwai anaangushwa na mawaziri wake kwa corruptions.

So, hawa marahisi wawili wameonyesha weakness katika different parts of leaderships, but we cant compare the leadership plan.
 
Siwezi kuwasifia hao.
Nyerere alikuwa mzuri kisiasa lakini sio fisadi.
As kuhusu siasa na ufisadi, sijaona mwanasisa wa kiafrika wa sasa hivi wa kumsifia. So, sihitaji kumake-up mind mkuu.

Mkuu heshima mbele, naona tunahitaji kukubali kutokubaliana, maana sio yote unayoaamini wewe na sisi wote ni lazima tuamini hivyo hivyo, inaonekana kuwa ndio tatizo hapa, anyways mimi ninaendelea kuheshimu vipaji vya viongozi wetu, maana kuna kina Sengor, waliokuwa wezi lakini walileta maendeleao kwa wananchi wao pia, Mwalimu hakuwa fisadi, lakini nafikiri unajua aliyotuachia!

Fair enough. Ila usiseme 'sisi wote'. Ila nakubali kutokubaliana. Heshima.
 
Mkuu kweli unaaamini Moi, alitaka kuwaachia KANU uongozi? Ili the West waendelee kumsakama kuhusu hela zao? Wewe huoni kuwa ilikuwa ni strategy ya kuwaondoa the West mgongoni kwake na it worked, kwa kuwapa the so called "Upinzani", wewe kweli unaamini kuwa Saitoti anaweza kwenda against Moi!

Kwa nini Kibaki mpaka leo hajamfikisha Moi, kwenye sheria na wakatio ushahidi wote upo clear? Hivi unajua Moi bado anatesa tena hata kuliko Kibaki mwenyewe rais wa Kenya?, na hawezi fanya kitu chochote!

Mkuu Moi, ni sungura mjanja huyo, na ni wachache sana Afrika!

Mkuu FMES,

Kwanza, sikuwa na habari kuhusu huo mkakati wa Moi wa kuwapa wapinzani uongozi. Lakini nina uhakika na kitu kimoja kwamba baada ya kuisambaratisha KANU alijuta kwanini alifanya hivyo maana inawezekana kabisa kwamba hakutarajia baadhi ya wana KANU wangeenda kujiunga na upinzani na kuongeza nguvu ya upinzani. Inawezekana ni kweli kabisa kwamba watu waliokuwa wanatarajia kuchukua mikoba yake walihisi wamesalitiwa na hivyo kuamua kuingia upinzani na wakafanya kweli. Ili kuthibitisha kwamba ushindi wa NARC ulimchanganya MOI ni kwamba hata handing over ya urais haikufuata proper channel. Walio hudhuria shughuli hiyo waliondoka na maswali mengi sana, kama kungekuwa na mahusiano mazuri kati ya MOI na serikali mpya ya KIBAKI. Nina uhakika MOI alichanganyikiwa na hakujua ni nini kingefuata na hasa ukizingatia kwamba Raila (adui yake mkubwa) alikuwa NARC na alikuwa likely kuteuliwa kuwa Waziri Mkuu wa nchi.

Chambo alichomeza KIBAKI ndiyo kimemfanya mpaka leo hii ashindwe kumshughulikia MOI na mafisadi wengine wa enzi za MOI. Kosa kubwa la KIBAKI ilikuwa ni kurithi Anglo Leasing Scandal na kuamua kutafuna hela. Dhambi hiyo bado inamfanya KIBAKI mpaka leo hii asiwe na nguvu ya kuwashughulikia mafisadi. Archtect wa Anglo Leasing alikuwa MOI na serikali yake, waliacha wametega mabomu na KIBAKI alipoingia alifakamia ulaji bila kujiuliza kama huo ulaji ulikuwa ni chambo au la. Baada ya kumeza chambo hakuwa na ujanja tena maana inabidi ukubaliane na aliyekulisha chambo kwa kufanya yale anayoyataka yeye. Kuanzia hapo ndipo mahusiano ya KIBAKI na MOI yalipokomaa, mara wakutane Ikulu au Kabarak (nyumbani kwa Moi). Hapo hapo kukawa na joto la katiba na hasa kilicholeta mgogoro mkubwa ilikuwa ni post ya Waziri Mkuu ambayo LDP walikuwa wanaitaka kwa nguvu zote kama walivyoahidiana na KIBAKI wakati wa makubaliano ya KIBAKI TOSHA!

Baada ya referandum na kubwagwa kwa KIBAKI na serikali yake, Kibaki alikosa mahali pa kukimbilia maana NARC ilishaonyesha dalili zote za kusambaratika. LDP ambaye alikuwa mshirika mkubwa alikuwa kajitoa serikalini kwa kwenda kinyume na serikali na ndipo mawaziri saba wakapigwa chini. Since then KIBAKI hakuwa na option na ndipo uswahiba ulipokuwa mkubwa sana kati ya KIBAKI na MOI kiasi cha kutia mashaka. MOI ndiye aliyefanya kazi ya kumhamisha Kenyatta kutoka ODM na kumrudisha KANU, na hiyo ilifanyika kwa makusudi ili kupunguza makali ya ODM. Lakini pamoja na hayo KIbaki bado ana kibarua kipevu kwani ushindani uliopo kati ya Kibaki na Raila ni mkubwa sana, lolote linaweza kutokea.

Kibaki akishinda basi itakuwa ni kutokana na mchango mkubwa sana wa MOI hasa baada ya MOI kufanikiwa kumhamisha Kenyatta kutoka kwenye kambi ya ODM. Wazo la kwamba Kenyatta atakuwa mgombea wa 2012 bado ninaliona ni kama ndoto kutokana na politics za Kenya zilivyo za ajabu sana. Kama Kenyatta kaahidiwa kupewa mikoba basi tusubiri 2012 kama tutakuwa hai ili tuone. Swala la kupewa u-makamu wa Rais it is easy, kwa kuwa ni maamuzi ya Rais personally. Japo hilo nalo linaweza kuleta msuguano mkubwa sana kati vyama vishiriki kwenye huo umoja wao. Kibaki hata kama akishinda bado atakuwa weak sana kwenye uongozi wake. Kinachomsaidia huyo jamaa huwa ni mtu wa kukaa kimya na kuacha mambo yaende jinsi yanavyokwenda na wala huwezi ukamsikia akijibu tuhuma labda kama Lucy Kibaki akimkomalia ndipo anaweza kutoa statement. But as long as hiyo ni term ya mwisho kwake basi wala hana haja ya hiyo PNU maana hata ikifa haihitaji tena kwa kuwa atakuwa alishaitumia kama ride ya kurudi Ikulu kumalizia miaka 10 ya utawala wa katiba!
 
I think is not fair kucompare kati ya kibaki na JK. Both this presidents are facing different turmoil in their leaderships. JK anaface big corruption, lack of leadership, wrong strategic planners and many other problems. Wakati Mwai anaangushwa na mawaziri wake kwa corruptions.

So, hawa marais wawili wameonyesha weakness katika different parts of leaderships, but we cant compare the leadership plan.

Kibaki ana watu wake na wote alikuwa amewaweka kwenye post za ulaji na wamefanya kufuru ya kula. Same applies to JK, angalia akina Karamagi, EL na wengineo ambao amewaweka kwenye position za kula. Kibaki alijitahidi kwa kuwaondoa akina Mwiraria, Murungi, na Murungaru. Tena mwanzoni walikuwa wabishi kweli ku-resign, lakini baadaye walijiuzulu. Pamoja na hayo mbona juzi aliwarudisha tena kazini na hakuna lolote la maana ambalo walifanyiwa kuhusu tuhuma zao. It pains unapoona UK wanampa waziri wako ban ya kuingia nchini kwao wakati wewe Rais wa nchi bado umemkumbatia tu kwamba anafaa. Watu wamepiga sana kelele kuhusu akina EL na Karamagi, hivi umeishasikia JK akihangaika na hizo kelele? Yuko kimya as if hakuna kinachoendelea. Kwa hiyo JK nae kazungukwa na akina Mwiraria wengine (EL, NK, and the likes).

Wote wawili wana sifa ya kuacha mambo yajiendee tu na hivyo system itaji-check yenyewe. Ndo maana akina EL wanakuwa na kiburi na jeuri ya kujifanyia mambo kwa jinsi wanavyoona wenyewe na hata ikibidi wanaweza kuteua mtu na kupewa ulaji na Rais akirejea anakuta changes na hawezi kuuliza.
 
Back
Top Bottom