Kwa mara ya kwanza.... | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kwa mara ya kwanza....

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by MJINI CHAI, May 28, 2011.

 1. MJINI CHAI

  MJINI CHAI JF-Expert Member

  #1
  May 28, 2011
  Joined: Dec 12, 2010
  Messages: 1,804
  Likes Received: 587
  Trophy Points: 280
  Heshima Wakuu....kwa mara ya kwanza tangu nizaliwe nimesikia maneno ya Faraja na ya kizalendo kutoka kwa kiongozi wa ngazi ya juu wa Wilaya, Huyo si mwingine ni DC wa wilaya ya KISARAWE mama KARAMAGE bila kujali kuwa leo 28.05.2011 ni siku ya Jumamosi ambapo alitakiwa apumzike lakini aliamua kufanya ziara katika kijiji cha KAZIMZUMBWI majira ya saa 14:26 akaaza mkutano na wanakijiji na kumtaka mwenyekiti wa kijiji kusoma ripoti ya mapato na matumizi ya kijiji ili wanakijiji wafahamu, vilevile alimtaka mwenyekiti kutoa vipaumbele vya kijiji. cha kushangaza uongozi wa kijiji walimweleza DC kuwa wataiandaa ripoti.......
  Ndipo mhe DC aliwaeleza wananchi ya kuwa Wilaya ya KISARAWE ni kongwe tangu enzi za mkoloni na ina takribani zaidi ya miaka 100 lakini ipo nyuma kimaendeleo, yeye akiwa kama DC wa 13 baada ya uhuru hatakubali wilaya hiyo ambayo ilianzishwa wakati mmoja na jiji la NAIROBI kenya iwe nyuma kimaendeleo..........
  Aliwataka wanakijiji kuwa na moyo wa kupenda maendeleo.....kwani yeye kama DC WAMEKAMILISHA MCHAKATO wa kuishanya wilya kuwa Mji Mdogo sambamba na kupima viwanja vya makazi na viwanda na tayari kiwanda cha cement kinaendelea kujengwa nakuwataka wanakijiji kujitokeza kuomba kazi mara kitakapoanza kufanya kazi......
  Aliwataka uongozi wa kijiji kumpa taarifa za wanafunzi ambao kwa njia moja au nyingine wameshindwa kwenda shule ili kuona anawasaidia vipi na aliwapa rai wazazi ya kuwa wasiwaachie wanafunzi kuendesha BODABODA wakaacha kwenda shule...........
  Kwa vile mji unapanuka aliwaasa watendaji wa wilaya ya kuwa kuna maeneo ambayo yameainishwa kwa kuyaendeleza hivyo ni vizuri wanakijiji wakashirikishwa ili kuondoa migogoro ya aridhi na hatimae wanakijiji watakao chukuliwa maeneo yao watafidiwa.......

  Kwa maoni yangu na baadhi ya wanakijijitumemkubali huyu mama na laiti kama ****** angekuwa na timu kama hii basi miji yetu ingekuwa mbali..licha ya mkutano kwisha saa 16:30 bado DC alichukua kama nusu saa tena kubadilishana mawazo na wanakijiji......it was very interesting........... Je wakuu huko kwenu MaDC wanabadilishana mawazo na wanakijiji?......
   
 2. ABEDNEGO

  ABEDNEGO Senior Member

  #2
  May 28, 2011
  Joined: Aug 20, 2009
  Messages: 109
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Acha kutuhadaa bwana wewe DC ni shemeji yako unapigia chepuo, Siku zote alikuwa wapi?? Hilo gamba tuu mwambie Julai hayupo kwenye list tena ya ma-DC kwani yeye ni gamba la kuvuliwa tu!
   
 3. Timor

  Timor Member

  #3
  May 28, 2011
  Joined: Feb 4, 2009
  Messages: 49
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 15
  Jamani tuache kupigiana madebe humu JF huyu DC amechapa usingizi muda wote leo ndo anagutuka Kisarawe iko nyuma???
   
 4. MJINI CHAI

  MJINI CHAI JF-Expert Member

  #4
  May 29, 2011
  Joined: Dec 12, 2010
  Messages: 1,804
  Likes Received: 587
  Trophy Points: 280
  mnyonge mnyongeni........mimi binafsi ndio kwa mara ya kwanza nauona na kumsikiliza.......nawachukia viongozi wanaowazulumu wananchi kwa mgongo wa kuwatetea wawekezaji lakini si kwa huyu mama ni mchapa kazi kweli kweli na laiti kama una ndugu KISARAWE wewe muulize hataki masihara kwenye Kazi leo amenifurahisha sana kwenye kikao cha wanakijiji cha KAZIMZUMBWI.......
   
 5. MJINI CHAI

  MJINI CHAI JF-Expert Member

  #5
  May 29, 2011
  Joined: Dec 12, 2010
  Messages: 1,804
  Likes Received: 587
  Trophy Points: 280
  ABEDNEGO usemayo si ya kweli kwani hata kabila lake silifahamu......ingawa mimi ni mtu wa KUCHICHA sasa ISOMILE nadhani ndiye Mumewe na KUCHICHA wapi na wapi? tuwe wakweli wakati mungine DC hayupo kwenye Chama chochote Gamba linatoka wapi?.........kwa watu wa KISARAWE wanajua utendaji mzuri wa huyu mama ameibadilisha sana hii wilaya kimaendeleo......................
   
 6. MUREFU

  MUREFU JF-Expert Member

  #6
  May 29, 2011
  Joined: Oct 1, 2010
  Messages: 1,230
  Likes Received: 38
  Trophy Points: 145
  safi sana tatzo litakuja kwny selikar yetu ndo huwa wanatabia ya kumuangusha huyo mana akiipeleka vizur anaweza akaamishwa ili akapatengeneze pengne ndo hapo wanapohalibu mana unakuta watakae mleta ameshndwa kutengeneza kwngne au amehalibu kwngne ndo wanawaletea nyny
   
 7. MJINI CHAI

  MJINI CHAI JF-Expert Member

  #7
  May 30, 2011
  Joined: Dec 12, 2010
  Messages: 1,804
  Likes Received: 587
  Trophy Points: 280
  natamani MaDC wote TZ wangekuwa kama huyu Mama
   
Loading...