Kwa Mara ya Kwanza nimeona Mafanikio ya Serikali kwenye suala la Machinga, Hongera Serikali ya Awamu ya Sita

Hatutaona aibu kukiri kuwa JPM aliwatendea mema wamachinga, na wenyewe wataendelea kumshukuru na kumkumbuka daima!

Huo muonekano unaoufurahia hauwapi shibe watu maskini watanzania
Kwa nini hamkukaribishwa Ikulu?
Kuna biashara nzuri kule, hela yoote inatoka kule, ukipanga meza mlangoni faida tupu.
 
Kwenye suala la Machinga subiri kutoa pongezi baada ya miaka miwili au mitatu. Sasa hivi kwa mfano hapa Jijini Mwanza, RC, RAS, RPC, DC, DAS, DED, Mayor, OCD, Mbunge, Watendaji Kata wote na maafisa wao WOTE wako mabarabarani ETI wanawapanga Machinga. Hakuna ofisi inayofanya kazi. Swali la kujiuliza, hawa maafisa wakirudi ofisini kwao, Machinga watabaki "site"?
Watoto mliozaliwa juzi hamjui kwamba miji ina sheria zinazoongoza namna ya kuishi mjini.
Sheria za uzururaji zipo
Sheria za biashara zipo
Sheria za mazingira zipo
Sheria za usafi zipo

Tatizo kubwa la ninyi wenye mawazo kama yako ni kufikiri unapanda treni toka Uvinza na unajenga banda la mbao pale Posta , unakaanga chips na kuuza vipodozi, na maisha yanaenda!

Mwendazake aliwahadaa kwa malengo ya kisiasa.
 
Wameshindwa kuwatoa machangudoa na wala shisha ambao ni wahalifu wataweza kuwatoa machinga ambao hawamwibii mtu yoyote?

Tatizo viongozi wetu huwa hawajifunzi kutokana na historia ni suala la muda tu ngoja hela ziwaishie.
Machangu wapo mitandaoni uliona wp wamejenga juu ya mtaro wa maji
 
tatizo huwa halishi kwa kuacha tatizo liendelee.

Nimatumaini kuwa tatizo jipya unalolitabiri lipatapata utatuzi

Tatizo la njaa linatatuliwa na kulima

Ukilima unapata tatizo la sugu viganjani

Kuna namna ya kutatua tatizo la sugu na si kwa kuacha kulima.

Maisha ni matatizo yanayotafutiwa utatuzi kila siku.
Kufukuza na kubomoa vitega uchumi vya muwekezaji machinga ni tofauti na kuhamisha uwekezaji .
Unapoteza mtaji na wateja.
Unakuwa desperately doomed
Stressed and frustrated .
How do you cub this phenomenon?
 
  • Thanks
Reactions: Tsh
Muda sio mrefu atakuja kiongozi atasema machinga warudi kwenye maeneo yao Kama zamani ni suala la muda tu
Huko walipopelekwa kama mauzo hamna nawaona wakirudi tena mjini na hapo ndio kamatakamata na fujo zitaanza, tena huwa wanategea uchaguzi unapokarbia, hapo wanajua hawaguswi maana watanu
 
Watoto mliozaliwa juzi hamjui kwamba miji ina sheria zinazoongoza namna ya kuishi mjini.
Sheria za uzururaji zipo
Sheria za biashara zipo
Sheria za mazingira zipo
Sheria za usafi zipo

Tatizo kubwa la ninyi wenye mawazo kama yako ni kufikiri unapanda treni toka Uvinza na unajenga banda la mbao pale Posta , unakaanga chips na kuuza vipodozi, na maisha yanaenda!

Mwendazake aliwahadaa kwa malengo ya kisiasa.
Mi natolea mifano Mwanza, wewe unazungumzia Posta! Watu washamba mnafikiri maisha yako Dar tu! Pumbavu! Halafu, unavyoshadidia Machinga utafikiri wewe hiyo fremu ya duka unalo!

Eti JPM aliwatumia kisiasa. Sawa. Nakupa changamoto. Kama wewe ni mwanasiasa nenda kwenye kampeni za 2025 ukiwaambia wananchi kuwa ukichaguliwa utahakikisha unawashughulikia Machinga uone kama utashinda. Hata huyo Mama ni mnafiki tu.
 
Unadhani watanzania wote ni matahira Kama wewe?

Fuatilia maoni ya watu! Wengi wanaunga mkono juhudi za serikali kuwapanga vizuri ili wafanye biashara Kwa mpangilio na kistaarabu
 
Amani iwe nanyi wanabodi!

Wakati Mama Samia anatangaza mkakati wake wa kuwapanga upya machinga kwenye maeneo mbalimbali, nilibarikiwa kuwa mmoja wa watu wa mwanzo kabisa kutoa ushauri wangu humu!

Ushauri huu niliutoa kwenye Thread hii hapa chini

Wakati naandika hii thread nilitoa haya Mawazo nikiamini kuwa yakifanyiwa kazi yataleta matokeo!

Baadae Waziri Mkuu wa JMT Ndug Kassim Majaliwa alifanya kikao na Wakuu wa Mikoa na akatoa maagizo ambayo nashukuru Mungu Kwa sehemu fulani yalitoka kwenye thread niliyoiandika hapa JF

Nirudi kwenye mada!
Watu wengi walipoona Rais Samia anatoa yale maagizo walifikiri kuwa kamwe hayatofanikiwa, Kuna wengine walidhani kuwa ndo Kama maagizo ya siku zote ya wanasiasa wa Tanzania ambayo hayazingatiwi, Kuna wengine walidhani as long as ni mwanamke basi ni dhaifu hivyo maagizo yake hayawezi kufanyiwa kazi, Kuna kundi lingine ni kwa chuki zao tu walimkatisha tamaa Mama samia na kuongea maneno ya kejeli kumdhihaki ili kumfanya aone tu hatoweza!

Nimekuwa jijini Dar es Salaam kwa wiki sasa na nimetembea sana Jiji la posta na hata maeneo ya Ubungo na mwenge, napenda kusema kwa sauti kuu na moja
HONGERA MAMA SAMIA, ZOEZI LINAKWENDA VIZURI NA SURA YA MJI WETU WA DAR UNAOJENGWA KWA GHARAMA KUBWA NA SERIKALI IMEANZA RASMI KUONEKANA.

Nilisema humu na ninasema tena, suala la machinga kamwe, haliwezi kuwa mfupa mgumu kwa serikali, kilichokuwa kunasababisha kutokea yale tuliyokuwa tunayaona awamu ya tano kurudi nyuma ni

1. Viongozi kukosa commitment ya kushughulikia mambo ya msingi

2. Siasa ya kijinga, uvivu na uzembe kwa viongozi hasa Wakuu wa Mikoa, Wilaya na Wakurugenzi wa Majiji na Halmashauri

3. Ushamba na kukosa exposure

Kwa mwezi sasa tumeona viongozi wakikomaa kushughulikia suala la machinga na sasa imeanza kuonekana kuwa kumbe inawezekana Kwa machinga kupangwa na kufanya biashara kistaarabu

Kwa Mafanikio haya niliyoanza kuyaona sasa napenda kuishauri Serikali ya Awamu ya Sita kuzingatia haya

1. Msibweteke kwa mafanikio mliyoanza kuyapata hasa baada ya machinga wenyewe kukubali kupangwa baada ya serikali kuweka msisitizo! Maeneo Yaliyokuwa wazi sasa yawekewe ulinzi na utaratibu maalum ili kutoruhusu hali ya huko nyuma kujirudia tena

2. Kuwe na by laws za faini na hata kufanya kazi za kijamii kwa watu wanaokiuka taratibu na kurudi kwenye maeneo waliyoondolewa

3. Ziundwe kamati za wafanyabiashara wenyewe kusimamiana wenyewe ili kutoruhusu sheria kuvunjwa tena na hali kurudi Kama ilivyokuwa.
Mf. Kwa kariakoo Wafanyabiashara wa pale waunde kamati zao na vikundi vyao vya kusimamia usafi na ufanyaji biashara kwa kuzingatia taratibu . Kamati hizi sipewe meno na mamlaka ya kuadhibiana wenyewe kwa wenyewe pale taratibu zilizowekwa zinapokiukwa

4. Kwa maeneo wanayopelekwa machinga! Naomba sasa mkazo uwekwe huko, miundombinu Bora na ya kisiasa ijengwe huko. Wafanyabiashara hawa wapangwe na kusimamiwa vizuri chini ya kamati za wao wenyewe watakaoziunda. Wapangwe kisasa na kistaarabu kwa kuzingatia aina ya biashara wanayofanya

Wafanyabiashara hawa wawekewe utaratibu mzuri wa kulipa kodi kidogo kidogo na jamii ielekezwe kwenye kununua bidhaa kwenye maeneo hayo walikopangiwa wafanyabiashara hao. Vijengwe vituo vya mabasi kwenye maeneo hayo ili ununuzi wa bidhaa uwe rahisi

Naomba niishie hapa Kwa leo
Naunga mkono hoja zako lakini punguza kumsifia Sifia bila sababu,
 
Unadhani watanzania wote ni matahira Kama wewe?

Fuatilia maoni ya watu! Wengi wanaunga mkono juhudi za serikali kuwapanga vizuri ili wafanye biashara Kwa mpangilio na kistaarabu
Watu wengi unamaaninisha walioipigia kura CCM iongoze Serikali? Hapo sawa. Nakuunga mkono!!!
 
Amani iwe nanyi wanabodi!

Wakati Mama Samia anatangaza mkakati wake wa kuwapanga upya machinga kwenye maeneo mbalimbali, nilibarikiwa kuwa mmoja wa watu wa mwanzo kabisa kutoa ushauri wangu humu!

Ushauri huu niliutoa kwenye Thread hii hapa chini

Wakati naandika hii thread nilitoa haya Mawazo nikiamini kuwa yakifanyiwa kazi yataleta matokeo!

Baadae Waziri Mkuu wa JMT Ndug Kassim Majaliwa alifanya kikao na Wakuu wa Mikoa na akatoa maagizo ambayo nashukuru Mungu Kwa sehemu fulani yalitoka kwenye thread niliyoiandika hapa JF

Nirudi kwenye mada!
Watu wengi walipoona Rais Samia anatoa yale maagizo walifikiri kuwa kamwe hayatofanikiwa, Kuna wengine walidhani kuwa ndo Kama maagizo ya siku zote ya wanasiasa wa Tanzania ambayo hayazingatiwi, Kuna wengine walidhani as long as ni mwanamke basi ni dhaifu hivyo maagizo yake hayawezi kufanyiwa kazi, Kuna kundi lingine ni kwa chuki zao tu walimkatisha tamaa Mama samia na kuongea maneno ya kejeli kumdhihaki ili kumfanya aone tu hatoweza!

Nimekuwa jijini Dar es Salaam kwa wiki sasa na nimetembea sana Jiji la posta na hata maeneo ya Ubungo na mwenge, napenda kusema kwa sauti kuu na moja
HONGERA MAMA SAMIA, ZOEZI LINAKWENDA VIZURI NA SURA YA MJI WETU WA DAR UNAOJENGWA KWA GHARAMA KUBWA NA SERIKALI IMEANZA RASMI KUONEKANA.

Nilisema humu na ninasema tena, suala la machinga kamwe, haliwezi kuwa mfupa mgumu kwa serikali, kilichokuwa kunasababisha kutokea yale tuliyokuwa tunayaona awamu ya tano kurudi nyuma ni

1. Viongozi kukosa commitment ya kushughulikia mambo ya msingi

2. Siasa ya kijinga, uvivu na uzembe kwa viongozi hasa Wakuu wa Mikoa, Wilaya na Wakurugenzi wa Majiji na Halmashauri

3. Ushamba na kukosa exposure

Kwa mwezi sasa tumeona viongozi wakikomaa kushughulikia suala la machinga na sasa imeanza kuonekana kuwa kumbe inawezekana Kwa machinga kupangwa na kufanya biashara kistaarabu

Kwa Mafanikio haya niliyoanza kuyaona sasa napenda kuishauri Serikali ya Awamu ya Sita kuzingatia haya

1. Msibweteke kwa mafanikio mliyoanza kuyapata hasa baada ya machinga wenyewe kukubali kupangwa baada ya serikali kuweka msisitizo! Maeneo Yaliyokuwa wazi sasa yawekewe ulinzi na utaratibu maalum ili kutoruhusu hali ya huko nyuma kujirudia tena

2. Kuwe na by laws za faini na hata kufanya kazi za kijamii kwa watu wanaokiuka taratibu na kurudi kwenye maeneo waliyoondolewa

3. Ziundwe kamati za wafanyabiashara wenyewe kusimamiana wenyewe ili kutoruhusu sheria kuvunjwa tena na hali kurudi Kama ilivyokuwa.
Mf. Kwa kariakoo Wafanyabiashara wa pale waunde kamati zao na vikundi vyao vya kusimamia usafi na ufanyaji biashara kwa kuzingatia taratibu . Kamati hizi sipewe meno na mamlaka ya kuadhibiana wenyewe kwa wenyewe pale taratibu zilizowekwa zinapokiukwa

4. Kwa maeneo wanayopelekwa machinga! Naomba sasa mkazo uwekwe huko, miundombinu Bora na ya kisiasa ijengwe huko. Wafanyabiashara hawa wapangwe na kusimamiwa vizuri chini ya kamati za wao wenyewe watakaoziunda. Wapangwe kisasa na kistaarabu kwa kuzingatia aina ya biashara wanayofanya

Wafanyabiashara hawa wawekewe utaratibu mzuri wa kulipa kodi kidogo kidogo na jamii ielekezwe kwenye kununua bidhaa kwenye maeneo hayo walikopangiwa wafanyabiashara hao. Vijengwe vituo vya mabasi kwenye maeneo hayo ili ununuzi wa bidhaa uwe rahisi

Naomba niishie hapa Kwa leo
Huu utakuwa waraka kwa wakuu wa mikoa usomwe na Wakuu wote wa mikoa.
 
Ukweli ni kwamba hata barabara sasa zinaonekana vizuri baada ya kuondoa hao wanaoitwa wajasiriamali aka wapiga kura , sijui walikua wanaona tabu gani kuwaondoa hao maana waliwaruhusu wenyewe kuwa mtaani
 
Back
Top Bottom