Kwa mara ya kwanza nchini Taasisi ya moyo ya Kikwete imefanya upasuaji wa mshipa mkubwa kwenye moyo

Miss Zomboko

JF-Expert Member
May 18, 2014
4,479
9,234
DOQZt-pW0AApQE1.jpg

Kwa mara ya kwanza hapa nchini Taasisi ya moyo ya Jakaya Kikwete imefanya upasuaji wa kurekebisha mshipa mkubwa unaotoa damu kwenye moyo kwenda sehemu zingine za mwili katika kambi maalum ya upasuaji ya siku sita.

======

Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete kwa mara ya kwanza hapa nchini imefanya upasuaji wa kurekebisha mshipa mkubwa unaotoa damu kwenye moyo kwenda sehemu zingine za mwili katika kambi maalum ya upasuaji ya siku sita katika mkutano na waandishi wa habari hospitalini hapo jijini Dar es salaam.

Daktari wa moyo kutoka katika taasisi hiyo Dkt. Bashir Nyangasa amesema katika kambi hiyo ya siku sita kwa kushirikiana na hospitali ya Saifee ya mjini Mumbai nchini India wamefanikiwa kuwafanyia upasuaji mkubwa wa moyo wagonjwa 15 ambao wote afya zao zinaimarika Dkt. Nyangasa amesema upasuaji huo umesaidia serikali kuokoa kiasi kikubwa cha fedha kwani endapo wagonjwa hao wangekwenda kutibiwa nje ya nchi ingetumia zaidi ya milioni 405,gharama ya mgonjwa mmoja ikiwa Milioni 25 ukilinganisha na gharama waliyotumia katika taasisi hiyo sh Milioni 225 tu kwa wagonjwa wote 15.

Taasisi hiyo imeendelea kusisitiza wananchi kufika katika hispitali hiyo kujitolea kuchangia damu kutokana na kuhitajika kwa wingi kwani mgonjwa anayefanyiwa upasuaji huhitaji damu kati ya chupa 5 hadi 6.

Chanzo: ITV
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom