Kwa mara ya kwanza natoa pongezi kwa Lukuvi

Lord denning

JF-Expert Member
Jun 3, 2015
13,214
26,003
Amani iwe nanyi wadau

Leo nimeona taarifa Azam Tv, waziri wa Ardhi akiongelea suala la watendaji wa kata/ serikali za mitaa kupewa mamlaka ya kusimamia ardhi/ makazi.

Suala hili wana JF humu tuliwai kutoa ushauri kwa serikali hii Kama hatua wanayopaswa kuchukua katika kukabiliana na tatizo la makazi holela na ujenzi mbovu unaoharibu mipango miji.

Uzi mmoja wapo ni huu👇

Kwa taarifa hii niliyoiona Leo, napenda kwa Mara ya kwanza kumpongeza ndugu William Lukuvi kwa kuchukua ushauri huu murua ambao kwa hakika ninaamini tukiusimamia vizuri ndo itakuwa dawa kuu na ya kudumu wa makazi holela na ujenzi mbovu usiozingatia mipango miji hapa Tanzania.

Napenda kusisitiza kwa Lukuvi, hili alilolianzisha wala asirudi nyuma maana ndo Litaondoa ujenzi holela na makazi holela hapa Tanzania.

====
WATENDAJI WA MITAA KUPEWA RUNGU KUSIMAMIA ARDHI:

Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi amewaagiza wakurugenzi wa halmashauri nchini kuwapatia mamlaka maafisa watendaji wa mtaa ili wawe na uwezo wa kusimamia masuala yote ya uendelezaji ardhi na kuwachukulia hatua watu wanaokiuka taratibu za ujenzi kwenye mitaa yao.
 
Siungi mkono ,japo wenda wazo lake likawa siri,

Watendaji wa kata tangu mwanzo ipo sheria ya kuwaruhusu simamia huuzwaji wa ardhi Kuna eka wanastahili simamia ,sikumbuki vizuri
Ila Hawa watendaji ata Kama ni mmoja wapo au la, wamegeuka kua madalali wa ardhi za watu.

KWA lugha nyingine wamekua wezi, so kuwaongezea hili watakua wezi Mara mia, so KWA nia ya Lukuvi basi bora itafutwe namna nyingine ya kubeba Jambo hili ,watendaji ni wezi, KWA kushirikiana na wengine, wengine wanafanya wizi hata karibu ya chamwino ikulu, KWA kudhulum ardhi ya wananchi na tena ukizingatia waliitwa ikulu kwa mwaliko kila mmoja hujifanya kipenyo.

wezi Sana hao mh Lukuvi,japo nilisha muomba mungu hutumbuliwe KWA kutaka nyanganya viwanja vya wazalendo wa nchi yao kisa hawajaendeleza.
 
Topic yako na hio uliyoiweka Naona Kama mnaongelea vitu tofauti..

, sijui utendaji wao, Ina maana kutakua na mkandarasi kila kata? Maanake hao viongozi sijui kama wana uwezo huo wa kujua wapi pasijengwe au ndio mimi sielewi, ufafanuzi plz
 
Hao wanaopenda rushwa za elfu tano ndio wasimamie matumizi ya ardhi?
Hawa watakuwa wasimamizi tu wa sheria na taratibu, pamoja na miongozo itskayokuwa inawekwa na maofisa ardhi wa wilaya pamoja na wizarani.

Hakuna linaloshidikana panapokuwa na nia dhabiti na usimamizi mzuri kwenye utekelezaji.

Kwa hali nchi hii ilipofikia sasa ni lazima kuwe na mfumo wa kuwajibishana utakaohakikisha kila mtu anaheshimu ujenzi bora unaozingatia mipango miji. Watu wasimamiwe kujenga kwa mpangilio na wazingatie kuacha barabara kubwa kwenye mitaa ili kila nyumba iwe inafikika kirahisi hata na magari makubwa Kama ya Takataka na hata fire.

Kikubwa hawa watu wawekewe miongozo ya kusimamia makazi bora na mipango miji na wasimamiwe ipasavyo
 
Topic yako na hio uliyoiweka Naona Kama mnaongelea vitu tofauti..

, sijui utendaji wao, Ina maana kutakua na mkandarasi kila kata? Maanake hao viongozi sijui kama wana uwezo huo wa kujua wapi pasijengwe au ndio mimi sielewi, ufafanuzi plz
Mapendekezo ni kuwa hawa ndo wawe wasimamizi kuhakikisha ujenzi wa mitaani unazingatia mipango miji na makazi bora. Wawe na mamlaka ya kusimamisha na kurepoti juu kwa maofisa ardhi juu ya mtu yeyote anayeuza eneo lake bila kuweka njia za kuhakikisha magari makubwa yanapishana, wawe na mamlaka pia ya kusimamisha ujenzi wowote usiozingatia mipango miji Mf. Mtu anajenga na kuzuia barabara au anawazibia majirani wake njia.

Lazima tukubali kuwa kuongezeka kwa makazi holela Tanzania kumechangiwa sana na kutokuwepo kwa mfumo thabiti wa usimamizi wa mipango miji.

Lukuvi akifanikiwa kuliweka sawa hili. Tutakuja kumkumbuka na kumpa nishani huko mbeleni kwa sababu tatizo kuu la Tanzania kwa sasa ni makazi holela na hili jambo lisipofanyiwa kazi sasa huko mbeleni watu tutaikana Tanzania kwa aibu
 
Siungi mkono ,japo wenda wazo lake likawa siri,

Watendaji wa kata tangu mwanzo ipo sheria ya kuwaruhusu simamia huuzwaji wa ardhi Kuna eka wanastahili simamia ,sikumbuki vizuri
Ila Hawa watendaji ata Kama ni mmoja wapo au la, wamegeuka kua madalali wa ardhi za watu.

KWA lugha nyingine wamekua wezi, so kuwaongezea hili watakua wezi Mara mia, so KWA nia ya Lukuvi basi bora itafutwe namna nyingine ya kubeba Jambo hili ,watendaji ni wezi, KWA kushirikiana na wengine, wengine wanafanya wizi hata karibu ya chamwino ikulu, KWA kudhulum ardhi ya wananchi na tena ukizingatia waliitwa ikulu kwa mwaliko kila mmoja hujifanya kipenyo.

wezi Sana hao mh Lukuvi,japo nilisha muomba mungu hutumbuliwe KWA kutaka nyanganya viwanja vya wazalendo wa nchi yao kisa hawajaendeleza.
Unapokuwa na sheria bila muongozo lazima siku ya mwisho utafeli tu. Unampa mtu mamlaka ya kusimamia uuzwaji alafu huweki muongozo au mamlaka kwake katika kusimamia au kuhakikisha mipango miji inazingatiwa hapo Kwa nini usifeli??

Mpe mamlaka ya mtungie sheria ya kusimamia mipango miji then akifeli ndo uje kumlaumu
 
Ni adui yako?
Mimi nilitarajia ungesema unampongeza kwa mara nyingine tena. Nasema hivi kwa sababu huyu mtu ana mambo mengi mno na hayahesabiki ambayo kwayo anasthaili kupongezwa. Wewe ndiyo umeona hili tu katika yote ambayo ameshawahi kufanya Lukuvi kiasi kwamba unasema bila aibu kabisa kwamba unampongeza mara ya kwanza?
 
Tufwile.... Kuna demu wangu ni mtendaji wa Kijiji ambapo nilinunua ardhi sasa tulizinguana ameweka bifu. Sijui kama ardhi yangu itapona kwa rungu hili
 
Waziri pekee aliyeibadilisha Wizara ya Ardhi. Yaani unapata hati yako bila hongo tena kwa muda mfupi. Hakika ninatamani uwe lifetime Minister wa hiyo Wizara.
 
Back
Top Bottom