Kwa mara ya kwanza natoa pongezi kwa Lukuvi

Amani iwe nanyi wadau!

Leo nimeona taarifa Azam Tv, waziri wa Ardhi akiongelea suala la watendaji wa kata/ serikali za mitaa kupewa mamlaka ya kusimamia ardhi/ makazi.

Suala hili wana JF humu tuliwai kutoa ushauri kwa serikali hii Kama hatua wanayopaswa kuchukua katika kukabiliana na tatizo la makazi holela na ujenzi mbovu unaoharibu mipango miji.

Uzi mmoja wapo ni huu👇

Kwa taarifa hii niliyoiona Leo, napenda kwa Mara ya kwanza kumpongeza ndugu William Lukuvi kwa kuchukua ushauri huu murua ambao kwa hakika ninaamini tukiusimamia vizuri ndo itakuwa dawa kuu na ya kudumu wa makazi holela na ujenzi mbovu usiozingatia mipango miji hapa Tanzania.

Napenda kusisitiza kwa Lukuvi, hili alilolianzisha wala asirudi nyuma maana ndo Litaondoa ujenzi holela na makazi holela hapa Tanzania.

====
WATENDAJI WA MITAA KUPEWA RUNGU KUSIMAMIA ARDHI:

Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi amewaagiza wakurugenzi wa halmashauri nchini kuwapatia mamlaka maafisa watendaji wa mtaa ili wawe na uwezo wa kusimamia masuala yote ya uendelezaji ardhi na kuwachukulia hatua watu wanaokiuka taratibu za ujenzi kwenye mitaa yao.
Mkuu hiyo ipo tangu kitambo sn, watendaji wanatakiwa kusimamia tatizo linakuja kwenye urasimu wa utaoaji vibali vya ujenzi, pia gharama za michoro kwa mtu ambaye anajenga kwa kuunga unga chumba kimoja au viwili hawezi kwenda kuomba kibali + ramani zaidi ya laki 1 ambayo ataitumia kununua material
 
Lukuvi huyu jamaa anapiga kazi, basi tu kwangu ni presidential material.
Acha ujinga. Lukuvi ni Mwalimu wa UPE baada ya kumaliza STD VII, hana elimu yeyote.

Ukada wa CCM, unafiki na u-snitch ndiyo umemfikisha hapo kuwa Waziri.
 
Lukuvi kapwaya kwenye kitu kimoja tu kutatua migogoro ya ardhi bado kuna baadhi ya mikoa kuna migogoro ya chini chini baina ya wakulima na wafugaji yani imefikia hatua wanauwana kwasababu ya ardhi maeneo bado hayatengwa ipasavyo ili hawa mabwana wakae kwa amani
 
Ni adui yako?
Mimi nilitarajia ungesema unampongeza kwa mara nyingine tena. Nasema hivi kwa sababu huyu mtu ana mambo mengi mno na hayahesabiki ambayo kwayo anasthaili kupongezwa. Wewe ndiyo umeona hili tu katika yote ambayo ameshawahi kufanya Lukuvi kiasi kwamba unasema bila aibu kabisa kwamba unampongeza mara ya kwanza?
Kwangu mimi hili alilolifanya ndo jambo analostahili pongezi.

Kama hujui kuwa Tatizo kuu la Tanzania kwa sasa ni makazi holela basi wewe utakuwa una shida kwenye Ubongo wako.
 
Viongozi wa vijiji wanapenda rushwa hasa pale unapotazamia kununua ardhi, yani wanatumia vibaya sana madaraka yao, wengine wanakwamisha kabisa zoezi la ununuzi ardhi
 
Mkuu hiyo ipo tangu kitambo sn, watendaji wanatakiwa kusimamia tatizo linakuja kwenye urasimu wa utaoaji vibali vya ujenzi, pia gharama za michoro kwa mtu ambaye anajenga kwa kuunga unga chumba kimoja au viwili hawezi kwenda kuomba kibali + ramani zaidi ya laki 1 ambayo ataitumia kununua material
Lilikuwepo lakini halikuwekwa kwenye utaratibu wa enforcement. Tena lilikuwepo katika kuwaweka kushuhudia mauziano tu. Hawakuweko kwenye kusimamia mipango miji na kusimamia ujenzi ili kuepusha ujenzi holela
 
Acha ujinga. Lukuvi ni Mwalimu wa UPE baada ya kumaliza STD VII, hana elimu yeyote.

Ukada wa CCM, unafiki na u-snitch ndiyo umemfikisha hapo kuwa Waziri.
Hakuna binadamu ambaye Hana sifa hzo ulizozitaja , na pia hakuna mahali ufaulu wa darasan ndo umekuwa kigezo cha kupata kiongozi Bora , Diamond anaendesha Wasafi Media lakn kaishia form four, Steve Jobs alipata GPA ya 2 lakn ndo mwanzilishi wa Apple technology , Jack ma mwanzilishi wa Alibaba nafkri unajua background yake ..... Mambo anayoyafanya Lukuvi yamewashinda magenius wa darasan kama Pro Mhongo nk...

Jamaa yupo Baraza la mawazir tangu enzi za Mwinyi sjui Mkapa mpak leo ,siyo kaz rahs kama unavyofkria
 
Amani iwe nanyi wadau!

Leo nimeona taarifa Azam Tv, waziri wa Ardhi akiongelea suala la watendaji wa kata/ serikali za mitaa kupewa mamlaka ya kusimamia ardhi/ makazi.

Suala hili wana JF humu tuliwai kutoa ushauri kwa serikali hii Kama hatua wanayopaswa kuchukua katika kukabiliana na tatizo la makazi holela na ujenzi mbovu unaoharibu mipango miji.

Uzi mmoja wapo ni huu

Kwa taarifa hii niliyoiona Leo, napenda kwa Mara ya kwanza kumpongeza ndugu William Lukuvi kwa kuchukua ushauri huu murua ambao kwa hakika ninaamini tukiusimamia vizuri ndo itakuwa dawa kuu na ya kudumu wa makazi holela na ujenzi mbovu usiozingatia mipango miji hapa Tanzania.

Napenda kusisitiza kwa Lukuvi, hili alilolianzisha wala asirudi nyuma maana ndo Litaondoa ujenzi holela na makazi holela hapa Tanzania.

====
WATENDAJI WA MITAA KUPEWA RUNGU KUSIMAMIA ARDHI:

Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi amewaagiza wakurugenzi wa halmashauri nchini kuwapatia mamlaka maafisa watendaji wa mtaa ili wawe na uwezo wa kusimamia masuala yote ya uendelezaji ardhi na kuwachukulia hatua watu wanaokiuka taratibu za ujenzi kwenye mitaa yao.
Wengine wanatumia vibaya madaraka yao watakuja na hoja utasikia vunja hujazingatia kuacha nafasi ya barabara wakati huo huo mkononi una kibali cha ujenzi
 
Kwa hiyo unategemea hao watendaji wa mitaa ndiyo watakuwa mwarobaini wa mipango miji?
 
Wengine wanatumia vibaya madaraka yao watakuja na hoja utasikia vunja hujazingatia kuacha nafasi ya barabara wakati huo huo mkononi una kibali cha ujenzi
Hawawezi kutumia madaraka vibaya kwa sababu watakuwa wanasimamia miongozo na michoro wanayopewa na maofisa ardhi wa wilaya na mikoa.
 
Kwangu mimi hili alilolifanya ndo jambo analostahili pongezi.

Kama hujui kuwa Tatizo kuu la Tanzania kwa sasa ni makazi holela basi wewe utakuwa una shida kwenye Ubongo wako.
Kwa hiyo uwepo wa makazi holela unamfanya apoteze credits zote za mambo yote aliyowahi kufanya na kumpelekea abakize hiyo moja ya kwako, si ndiyo?
 
Hawawezi kutumia madaraka vibaya kwa sababu watakuwa wanasimamia miongozo na michoro wanayopewa na maofisa ardhi wa wilaya na mikoa.
Naongea hilo from experience, nina eneo langu nimejenga uzio tangu naanza kujenga mpaka namaliza hakuna aliekuja kuongelea chochote baadae nakuta barua ya serikali ya kijiji ikinitaka kubomoa uzio kosa sikuacha road reserve wakati nimeacha 10mitas toka kwenye uzio na ni barabara za mitaani, wewe usisemi kitu banah nilisumbuana nao sana mpaka nikaita tarura ndiyo wakasema nipo sawa, je ningevunja kwa kupaniki bila kuwa mbishi na ni juzi tu,
 
Jamaa kwenye ardhi kafight sio kitoto
Tz utamsifia mwanasiasa kama hayajakufika, amefight kitu gani? Kwa wakazi wa msalato waliopisha ujenzi wa airport kuna wengine mwaka wa 6 sasa hawajalipwa chochote na wengine makadirio ni ya hovyo nyumba ya 30M unalipwa 8M.
 
mnyonge mnyongeni haki yake mpeni, kwa kweli huyu mzee ni mchapa kazi kweli kweli na hana mihemuko na papala kama walivyo mawaziri wengi wa awamu hizi, kwa kiasi kikubwa amefanikiwa kupunguza sana migogoro ya Ardhi, big up Lukuvi
 
Amani iwe nanyi wadau!

Leo nimeona taarifa Azam Tv, waziri wa Ardhi akiongelea suala la watendaji wa kata/ serikali za mitaa kupewa mamlaka ya kusimamia ardhi/ makazi.

Suala hili wana JF humu tuliwai kutoa ushauri kwa serikali hii Kama hatua wanayopaswa kuchukua katika kukabiliana na tatizo la makazi holela na ujenzi mbovu unaoharibu mipango miji.

Uzi mmoja wapo ni huu👇

Kwa taarifa hii niliyoiona Leo, napenda kwa Mara ya kwanza kumpongeza ndugu William Lukuvi kwa kuchukua ushauri huu murua ambao kwa hakika ninaamini tukiusimamia vizuri ndo itakuwa dawa kuu na ya kudumu wa makazi holela na ujenzi mbovu usiozingatia mipango miji hapa Tanzania.

Napenda kusisitiza kwa Lukuvi, hili alilolianzisha wala asirudi nyuma maana ndo Litaondoa ujenzi holela na makazi holela hapa Tanzania.

====
WATENDAJI WA MITAA KUPEWA RUNGU KUSIMAMIA ARDHI:

Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi amewaagiza wakurugenzi wa halmashauri nchini kuwapatia mamlaka maafisa watendaji wa mtaa ili wawe na uwezo wa kusimamia masuala yote ya uendelezaji ardhi na kuwachukulia hatua watu wanaokiuka taratibu za ujenzi kwenye mitaa yao.
Huyu LUKUVI aliingia kichwa kichwa katika swala hili. Alipoingia alikataa kabisa vikaratasi vyetu vya kumiliki na kuuziana ardhi vyenye baraka ya watendaji wa mitaa. Nashukuru ameona alipokosea, kwani huko hakuna mahakama, polisi wala wataalam wa Ardhi. Hivyo njia nyepesi ya maridhiano ya wananchi ilikuwa kupitia watendaji wa mitaa.

Mpango huu kimsingi ulianzishwa wakati wa Kikwete na karatasi uliweza kuipeleka Ardhi na wakaanza mchakato wa kukupimia Ardhi. Lukuvi nilimsikia akisema hivi vikaratasi vyenu sivitambui mkavitupe tu. Wakati huo nilikuwa na vikaratasi kama hivyo vya viwanja vitatu - Iliniuma roho sana.

Shida haya mambo yanatolewa matamko tu na wala hayapelekwi Bungeni yakawa sheria, hivyo sitashangaa baada ya uchaguzi 2025 waziri wa ardhi wakati huo kuvikataa vikaratasi vitavyotolewa na watendaji. Yaani kuifutilia mbali hiyo kauli ya Lukuvi.

Wizara ya Ardhi ni Bomu ambalo bado halijapatiwa uvumbuzi!
 
Hakuna binadamu ambaye Hana sifa hzo ulizozitaja , na pia hakuna mahali ufaulu wa darasan ndo umekuwa kigezo cha kupata kiongozi Bora , Diamond anaendesha Wasafi Media lakn kaishia form four, Steve Jobs alipata GPA ya 2 lakn ndo mwanzilishi wa Apple technology , Jack ma mwanzilishi wa Alibaba nafkri unajua background yake ..... Mambo anayoyafanya Lukuvi yamewashinda magenius wa darasan kama Pro Mhongo nk...

Jamaa yupo Baraza la mawazir tangu enzi za Mwinyi sjui Mkapa mpak leo ,siyo kaz rahs kama unavyofkria
Kwa akili yako finyu unamuona Lukuvi anaweza? Hivi unajuwa Katiba ya JMT imetaja kiwango cha chini cha elimu ya mgombea u-Rais wa Tanzania kuwa ni nini?
 
Ni
Naongea hilo from experience, nina eneo langu nimejenga uzio tangu naanza kujenga mpaka namaliza hakuna aliekuja kuongelea chochote baadae nakuta barua ya serikali ya kijiji ikinitaka kubomoa uzio kosa sikuacha road reserve wakati nimeacha 10mitas toka kwenye uzio na ni barabara za mitaani, wewe usisemi kitu banah nilisumbuana nao sana mpaka nikaita tarura ndiyo wakasema nipo sawa, je ningevunja kwa kupaniki bila kuwa mbishi na ni juzi tu,
Nimekuelewa, ila kwa sasa hili linaenda kuwekewa msukumo na msisitizo wa kisheria na kuwekewa utaratibu mzuri zaidi. Kwa iyo hiki kinachoenda kufanyika ni kizuri zaidi
 
Back
Top Bottom