Kwa mara ya kwanza katika maisha yangu, video hii yaniliza! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kwa mara ya kwanza katika maisha yangu, video hii yaniliza!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mag3, Feb 8, 2012.

 1. Mag3

  Mag3 JF-Expert Member

  #1
  Feb 8, 2012
  Joined: May 31, 2008
  Messages: 9,094
  Likes Received: 6,187
  Trophy Points: 280
  Kwa hisani ya Legal and Human Rights Centre kupitia kwa mwanajamvi EMT.  Nimejikuta natoa machozi kitu ambacho hakikuwezekana katika maisha yangu yote hata pale nilipowapoteza ndugu zangu wa karibu. Nimejiuliza ni kwa nini hali imekuwa hivi kwani huzuni peke yake haijawahi kunitoa machozi! Ukweli ni kwamba hii ni zaidi ya huzuni, ni uchungu uliojaa hasira! Kwamba vifo vingi vya wapendwa wetu vingeweza kuepukika kama si upumbavu, uovu, ulafi, ufisadi, ubadhirifu na udhaifu wa viongozi walioko madarakani, ni ukweli mchungu na usiovumilika... hakika nalia...

  Nawalilia watu kama FaizaFoxy, Rejao, Ritz, Barubaru, Raia Mwema, Raisi wa Migomo, Topical, Malaria Sugu na wengineo ambao bila shaka watakuwa wanatabasamu kwa utendaji uliotukuka wa Jakaya Mrisho Kikwete uliotufikisha hapa.
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 2. Puppy

  Puppy JF-Expert Member

  #2
  Feb 8, 2012
  Joined: Oct 6, 2011
  Messages: 2,268
  Likes Received: 653
  Trophy Points: 280
  Kesho naandamana hata mwenyewe
   
 3. T

  Topical JF-Expert Member

  #3
  Feb 8, 2012
  Joined: Dec 3, 2010
  Messages: 5,176
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  mag3;

  first; Unaonaje tukichukua zile Bil.90 tunazowapa kanisa through MoU tukawapa madaktari utakubali?? najua hutakubali uache unafiki wako wewe ungelia na Richmond ya kanisa i.e. MoU ambayo hata hivyo wameshindwa kuboresha mazingira KCMC na Bugando..

  Pili; nawa challenge hawa madaktari wajenge hospitali yao waendeshe na walipane kama wanavyotaka (kama wanafikiri ni rahisi let them try) waache wale madaktari wanaotosheka na mshahara wa serikali wachape kazi ..otherwise hii ni siasa na kukosa utu na inachochewa na wanasiasa kama wewe..na mwanakijiji et al. after all this is free market


  tatu; madakatari Tanzania wanasoma bila kulipa mikopo, hizo hela zinatoka kwa wananchi wanaowatesa kwa sasa; simply hawana hoja isipokuwa harakati za kisiasa..
   
 4. A

  August JF-Expert Member

  #4
  Feb 8, 2012
  Joined: Jun 18, 2007
  Messages: 4,505
  Likes Received: 723
  Trophy Points: 280
  wana subiri shida za jangwani na majipandwe
   
 5. m

  mtolewa Senior Member

  #5
  Feb 8, 2012
  Joined: Jan 18, 2011
  Messages: 197
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  tatizo lako ni kwamba hauko objective na una roho ya korosho,angalia chuki binafsi zitakuua siku si zako
   
 6. Mchaka Mchaka

  Mchaka Mchaka JF Bronze Member

  #6
  Feb 8, 2012
  Joined: Jul 20, 2010
  Messages: 4,530
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 0
  Na ukiona mtu mzima analia ujue kuna jambo!
   
 7. BelindaJacob

  BelindaJacob JF-Expert Member

  #7
  Feb 8, 2012
  Joined: Nov 24, 2008
  Messages: 6,060
  Likes Received: 475
  Trophy Points: 180
  Kweli hali ni mbaya sana! Eeh Mola saidia nchi yetu tumalizane na hili janga. Inasikitisha!
   
 8. T

  Topical JF-Expert Member

  #8
  Feb 8, 2012
  Joined: Dec 3, 2010
  Messages: 5,176
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Nimetoa hoja tatu very objectives jibu basi hata moja; mwenye roho na chuki na ubinafsi nani sasa..yule anayevuta bil.90 halafu haboreshi huduma mbona hueleweki??
   
 9. Noti mpya tz

  Noti mpya tz JF-Expert Member

  #9
  Feb 8, 2012
  Joined: Mar 23, 2011
  Messages: 936
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Wewe kweli hata aibu utadhan ulizaliwa mtini.
  Wananch wanalipa kodi inaenda serikalin na serikal inatakiwa iwalipe wananch kwa huduma.
   
 10. T

  Topical JF-Expert Member

  #10
  Feb 8, 2012
  Joined: Dec 3, 2010
  Messages: 5,176
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Usitukane wewe jibu hoja tatu nilizoweka hapo one after another nitakuelewa..

  Nasema hivi madai ya madaktari ni illusion hayatekelezeki wakae chini wajadiliane wakiwa hawana jazba na serikali; lakini kama vipi hii ni soko huria

  a. Wajenge hospitali zao walipane wapendavyo (problem solved) serikali itashindana na soko katika la ajira

  b. Kila anayesomea udakatari Tanzania nakusomeshwa na kwa kodi za wananchi aingie bond na serikali kwamba atafanya kazi serikalini for 5-8 kwa mshahara wa serikali uliopo

  c. Tuchukue bil.90 tunazo wapa kanisa tuwalipe madaktari maana kanisa limeshindwa kuboresha hospitali zake japo wanapokea pesa za umma..

  JIBUNI hizo hoja

  c.
   
 11. mshikachuma

  mshikachuma JF-Expert Member

  #11
  Feb 8, 2012
  Joined: Dec 2, 2010
  Messages: 2,853
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0

  Kwanza pole sana mkuu....hauko peke yako,tuko wengi katika kilio hiki,
  Hapo kwenye bold uko sahihi kabisa....yaani hao watu wanaangalia jina la mtu,kabila,dini na chama chake. Yaani hawajali utendaji
  wake wa kazi wala nini....yaani hao watu ni wa kuwaonea huruma na kuwasamehe bure!
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 12. salito

  salito JF-Expert Member

  #12
  Feb 8, 2012
  Joined: Dec 29, 2011
  Messages: 1,365
  Likes Received: 352
  Trophy Points: 180
  wewe nae mwana umbwembwe..
   
 13. salito

  salito JF-Expert Member

  #13
  Feb 8, 2012
  Joined: Dec 29, 2011
  Messages: 1,365
  Likes Received: 352
  Trophy Points: 180
  dah washkaji tusitukanane humu haina haja,tueleweshane taratibu,tutatoana ngeu za bure humu jman wakati tayari nchi ipo kwenye msiba wa kuondokewa na wananchi wake wasio na idadi,tukikaa vibaya hapa kila baada ya nyumba mbili kutakuwa na maturubai ya misiba.
   
 14. QUALITY

  QUALITY JF-Expert Member

  #14
  Feb 8, 2012
  Joined: Sep 27, 2010
  Messages: 854
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Wafanye linalowezekana madaktari walipwe. Tumezoea kudharau taaluma na kutukiza wanasiasa; sasa maji yamefika shingoni. Ngoja kidogo uone hoja ya wabunge wa CCM kuwa hawana imani na Rais hapo ndipo utajua kuwa hata wewe hauna lako. Hapo ni mawili, Bunge lipige kura ya kutokuwa na imani na Rais au Rais avunje Bunge kazi ianze upya. Rais akitoka, tunatafuta Rais anayefaa.

  Uliona wapi Rais ambaye anakaa kimya wakati maisha ya wananchi wake yanateketea?

  Rais anaenda kusherehekea kwa kuchinja ng'ombe 50 huku watu wanakufa, hawana hata wa kucertify kuwa wamekufa wapelekwe chumba cha maiti?
  Rais anacheza ngoma n.k

  Hatuna viongozi Tanzania,

  Great Doctors.
   
 15. Matola

  Matola JF-Expert Member

  #15
  Feb 8, 2012
  Joined: Oct 18, 2010
  Messages: 36,045
  Likes Received: 13,265
  Trophy Points: 280
  Wewe ni pimbi tu. subiri ubwabwa na urojo tu hakuna unalolijuwa hapa.
   
 16. T

  Topical JF-Expert Member

  #16
  Feb 8, 2012
  Joined: Dec 3, 2010
  Messages: 5,176
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Zero thinking capacity, soon nitaku-report
   
 17. T

  Topical JF-Expert Member

  #17
  Feb 8, 2012
  Joined: Dec 3, 2010
  Messages: 5,176
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Zero thinking capacity
   
 18. K

  Kuntakint JF-Expert Member

  #18
  Feb 8, 2012
  Joined: Sep 26, 2011
  Messages: 1,111
  Likes Received: 468
  Trophy Points: 180
  Fikiria kabla ya kuchangia hapa ulipwi posho ata ukichangia mara mia.
   
 19. Kiziza

  Kiziza JF-Expert Member

  #19
  Feb 8, 2012
  Joined: Dec 10, 2011
  Messages: 440
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Ina maana leo ndio mara yako ya kwanza kulia?
   
 20. Superman

  Superman JF-Expert Member

  #20
  Feb 8, 2012
  Joined: Mar 31, 2007
  Messages: 5,702
  Likes Received: 97
  Trophy Points: 145
  Moja ya dalili ya Serikali iliyoshindwa kutekeleza wajibu wake ni kuzembea katika eneo linalohusika na Haki ya Mtu Kuishi.

  Kwa maelezo yoyote yatakayotolewa hali haikupasa kufika hapa ilipofika. Uongozi umekosekana.

  Na ieleweke kuwa binadamu yoyote anapofika katika "Point Of No Return" basi hajali chochote kitakachotokea au kitakachompata.

  Poleni sana wagonjwa na ndugu wa wote waliopoteza maisha katika sakata hili.
   
Loading...