Yoyo Zhou
Member
- Jun 16, 2020
- 71
- 110
Jarida la Fortune ambalo limekuwa likitoa orodha ya kampuni yenye nguvu zaidi duniani, limetoa orodha ya mwaka huu ya makampuni 500 yanayoongoza duniani. Kwa mara ya kwanza kwenye orodha hiyo idadi ya makampuni ya China, ikiwa ni yale ya China Bara na Hong Kong imefikia 124, ikiwa imezidi idadi ya makampuni ya Marekani ambayo ni 121.
Tangu China ilipoanza kutekeleza sera ya mageuzi na kufungua mlango, idadi ya makampuni nchini China yenye nguvu imekuwa ikiendelea kuongezeka kutokana maendeleo ya uchumi wake. Mwaka 1997 kulikuwa na kampuni nne za China bara zilizoingia katika orodha hiyo. Mwaka 2001 China ilipojiunga na Shirika la biashara duniani WTO, idadi ya hiyo iliongezeka hadi 12.
Mwaka 2008, kasi ya ongezeko hilo ilikuwa ya kasi zaidi, na kufanya idadi ya makampuni ya China kuizidi ya Ujerumani, Ufaransa, Uingereza na Japan. Jarida la Fortune limesema, tangu mwaka 1995 orodha ya kampuni 500 bora duniani ilipoanza kutolewa, hakuna nchi yoyote iliyoweza kukua kwa kasi kama China.
Kutolewa kwa orodha hii kumekuja wakati kuna migongano wa kiuchumi kati ya China na Marekani, na kutoa mwanga zaidi kuwa kinachoendelea kati ya China na Marekani ni kuwa Marekani haipendi kuona nafasi yake ya kuwa mbele inachukuliwa na nchi nyingine duniani, hasa katika wakati huu ambao China inaonekana kuwa na uwezo mkubwa zaidi, wasiwasi wa Marekani unazidi kuongezeka.
Hata tukiangalia makampuni yanayolengwa na Marekani kwa njia mbalimbali, badala ya kuporomoka inaonekana kuwa yanazidi kuwa imara. Mfano mzuri ni kampuni ya Huawei ambayo inaandamwa sana na Marekani ambayo sasa imekuwa moja ya makampuni 50 yanayoongoza kwenye orodha hiyo.
Katika upande wa kampuni za mtandao wa Internet, kampuni saba duniani zimeingia kwenye orodha hiyo, ambazo ni Amazon, Alphabet, Facebook za Marekani, na JD.com, Alibaba, Tencent na Xiaomi za China.
Katika hali nyingine ya kufurahisha ni kuwa, makampuni ya China yanayofanya shughuli zake barani Afrika hasa yale yanayojihusisha kwenye miradi mikubwa ya ujenzi miundo mbinu yako kwenye orodha ya makampuni hayo. Uwepo wa makampuni hayo unaonyesha kuwa licha ya ushirikiano kati ya China na Afrika umehimiza makampuni hayo kupata maendeleo, bali pia unaonyesha kuwa makampuni ya China yanayoshiriki kwenye shughuli za maendeleo ya Afrika ni makampuni yenye uwezo mkubwa.