Kwa mara ya kwanza, 2018 Tanzania inapata madaktari bingwa wanawake wa upasuaji wa Ubongo, Mgongo na Mishipa ya fahamu

mambo mengine si ya kulaumiana kuna historia huko nyuma kwa mfano mwanafunzi wa uchumi akimaliza shahada yake ya kwanzaataitwa mchumi akiwa na shahada ya uzamili ataitwa mchumi na akiwa na shahada ya tatu ya uchumi bado ataitwa mchumi kama Prof Lipumba huwa anaitwa mchumi tu.hiyo inatokana na historia ya namna gani wasomi wetu walianzwa kuitwa huko nyuma.lakini haizuii huwa mchumi wa PhD kuitwa Mchumi Bingwa wa kodi au Mchumi Bingwa wa kitu fulani.Hata mainjinia haizui kumuita Injia Bingwa wa Rejeta au Injia Bingwa wa Gearbox au Injinia Bingwa wa zege au Injinia Bingwa wa soft wire.
Ni Tz tu. Watu wataka waitwe majina makubwa, utendaji sifuri. Unakuta sijui mhandisi msomi fulani, lakini ni mkuu wa mkoa, au waziri, wapi na wapi!
 
Naona hao wadada wameamua kujipiga promo dk bingwa kwa kuhitimu tu ?
Wamekuaje mabingwa?
Hivi daktari bingwa ndio kwa kimombo anaitwa specialist?

Sijui ni mimi tu ama na wengine, huwa nahisi kama jina "daktari bingwa" linapotosha hivi? Si kama nadharau taaluma, nawaheshimu sana. Ni kama ilivyo kwa "wakili msomi" kwa taaluma ya sheria.

Hongera kwa hao kina dada kwa ubobevu.
Daktari bingwa ni "super specialist" ambae kitaaluma ana masters ya kwanza ya MMed na baada ya hapo akasoma post masters nyengine ya eneo jengine kama hao wa ubongo....
Wakati huo wote huwa anaitwa resident doctor na huwa anafanya kazi chini ya uangalizi kwa hiyo mpaka anapatiwa usuper specialist ame prove uwezo wake kwenye eneo hilo
 
  • Thanks
Reactions: SMU
Tangu uanze hii course mpk uhitimu inachukua muda gani kuanzia Bachelor degree
Shahada ya kwanza huwa ni miaka 5 na mwaka 1 wa internship hivyo ni miaka 6 baada ya hapo daktari anatakiwa kufanya kazi miaka 3 kabla ya kwenda kuchukua kozi ya shahada ya pili na kwa kozi hii inaweza hata kuchukua miaka 7 kumaliza neurosurgery hivyo ukichanganya 5 na 7 unapata miaka 12

Hapo chini ni namna ambavyo hao mabingwa wanalipwa huko USA kama kazi ikitangazwa ya fani yao.

The salary range for a neurosurgeon averages $103,279‒$789,182, depending on experience. With bonuses, profit-sharing and commissions, top neurosurgeons can earn more than $800,000 annually.

How Many Years Does it Take to Become a Neurosurgeon?
 
Hii avatar yako nasikia huyo jamaa Valentine karudi kwa mama yake analelewa na amekuwa mnywa pombe za kienyeji utadhani hakuwahi kuwa rais wa nchi
1544183088560.png
1544183088560.png
 
mambo mengine si ya kulaumiana kuna historia huko nyuma kwa mfano mwanafunzi wa uchumi akimaliza shahada yake ya kwanzaataitwa mchumi akiwa na shahada ya uzamili ataitwa mchumi na akiwa na shahada ya tatu ya uchumi bado ataitwa mchumi kama Prof Lipumba huwa anaitwa mchumi tu.hiyo inatokana na historia ya namna gani wasomi wetu walianzwa kuitwa huko nyuma.lakini haizuii huwa mchumi wa PhD kuitwa Mchumi Bingwa wa kodi au Mchumi Bingwa wa kitu fulani.Hata mainjinia haizui kumuita Injia Bingwa wa Rejeta au Injia Bingwa wa Gearbox au Injinia Bingwa wa zege au Injinia Bingwa wa soft wire.
Injinia bingwa wa kupiga deki
 
View attachment 958027
Tanzania imepata madaktari bingwa wanawake (Dr Aingaya Kaale na Dr Happiness Rabiel) wa upasuaji wa Ubongo, Mgongo na Mishipa ya fahamu kwa Mara ya kwanza. Madaktari hawa wamesoma Katika chuo kikuu cha Muhimbili MUHAS, na kufanya mafunzo kwa Vitendo hapa MOI.
Baada ya miaka 50+ ya uhuru? Ivi na hili ni la kujivunia? Mbona naona kama ni kichekesho na aibu kwa taifa?
 
Neno 'bingwa' hapo limetumiwa vibaya.
Ilitakiwa litumike neno "bobezi'

Neno lingine ambalo hutumiwa vibaya ni 'utawala'. Kwenye ofisi za umma hakuna anayetawaliwa bali watu wanaongozwa. Hivyo neno sahihi ni uongozi.
 
Kiswahili ni kigumu na hata maksi zake darasani huwa si za kuridhisha sana ukilinganisha na masomo mengine kama kiingereza
 
  • Thanks
Reactions: SMU
Neno 'bingwa' hapo limetumiwa vibaya.
Ilitakiwa litumike neno "bobezi'

Neno lingine ambalo hutumiwa vibaya ni 'utawala'. Kwenye ofisi za umma hakuna anayetawaliwa bali watu wanaongozwa. Hivyo neno sahihi ni uongozi.
exactly! Bingwa ina connote mashindano. So, Dr bingwa ameshindana na nani? "Bobezi" ingefaa zaidi.
 
Back
Top Bottom