Kwa mara ya kwanza, 2018 Tanzania inapata madaktari bingwa wanawake wa upasuaji wa Ubongo, Mgongo na Mishipa ya fahamu

tatum

JF-Expert Member
Jan 16, 2018
5,788
4,490
DtuuXM8WoAA-vFl.jpg

Tanzania imepata madaktari bingwa wanawake (Dr Aingaya Kaale na Dr Happiness Rabiel) wa upasuaji wa Ubongo, Mgongo na Mishipa ya fahamu kwa Mara ya kwanza. Madaktari hawa wamesoma Katika chuo kikuu cha Muhimbili MUHAS, na kufanya mafunzo kwa Vitendo hapa MOI.
 
Hivi daktari bingwa ndio kwa kimombo anaitwa specialist?

Sijui ni mimi tu ama na wengine, huwa nahisi kama jina "daktari bingwa" linapotosha hivi? Si kama nadharau taaluma, nawaheshimu sana. Ni kama ilivyo kwa "wakili msomi" kwa taaluma ya sheria.

Hongera kwa hao kina dada kwa ubobevu.
 
Madaktari bobezi katika upasuaji wa ubongo, mgongo na mishipa ya fahamu.
Bingwa ni mshindi aliyeshindana na wengine na kuwashinda wote.
 
Hivi daktari bingwa ndio kwa kimombo anaitwa specialist?

Sijui ni mimi tu ama na wengine, huwa nahisi kama jina "daktari bingwa" linapotosha hivi? Si kama nadharau taaluma, nawaheshimu sana. Ni kama ilivyo kwa "wakili msomi" kwa taaluma ya sheria.

Hongera kwa hao kina dada kwa ubobevu.
Daktari bingwa inaashiria kuwa amebobea kwenye eneo analotibu, jina ni la kitambo kidogo. Hii ya wakili msomi ni mbwembwe zisizo na maana hata kidogo. Hili jina limezuka siku za karibuni tu kutokana na vyuo kuzalisha wanasheria uchwara hivyo inferiority complex ikafanya wajiite hivyo.
 
Yap ni kweli kabisa hao wanaitwa Neurosurgeon sasa wanatimia 9 tu nchi nzima
 
Hivi daktari bingwa ndio kwa kimombo anaitwa specialist?

Sijui ni mimi tu ama na wengine, huwa nahisi kama jina "daktari bingwa" linapotosha hivi? Si kama nadharau taaluma, nawaheshimu sana. Ni kama ilivyo kwa "wakili msomi" kwa taaluma ya sheria.

Hongera kwa hao kina dada kwa ubobevu.
wakili msomi ni jina tu la utani kwa taaluma ya sheria lakini ikifika mwanasheria amesoma mpaka kufikia level ya degree tatu kwa maana ya kuwa na Ph D ya sheria basi huyo atakuwa ni Bingwa wa sheria katika eneo fulani hapo kama Family Law ya Prof Kabudi au Constitutional law ya marehemu Dr Mvungi
 
Yap ni kweli kabisa hao wanaitwa Neurosurgeon sasa wanatimia 9 tu nchi nzima
Afadhali kivumbi walimu wa hilo eneo kulikuwa na professor mmoja tu.mtanzania tena mzee sana wa hilo eneo .Hawa akina mama wakiweza waendelee kusoma wawe walimu hilo eneo bado Lina uhaba wa maprofessor watanzania
 
Watasoma tu naimani kuwa Prof Kahamba ni mzuri katika hilo eneo na pia tuna Dr Shabaan na wenzakeni wazuri sana pale MOI watawasaidia tu katika ujuzi wao.
 
Wamekuaje mabingwa?
Fani ya udaktari mwanafunzi wa fani ya udaktari akisoma masters ya fani ya udaktari kwa mfano internal medicine ataitwa daktari bingwa wa magonjwa ya ndani,akisoma masters ya ngozi ataitwa daktari bingwa wa magonjwa ya ngozi,akisoma masters ya upasuaji mwanadamu ataitwa daktari bingwa wa upasuaji na akisoma masters ya magonjwa ya wanawake ataitwa daktari bingwa wa magonjwa ya wanawake.....sijui hasa swali lako kama kuna tofauti na haya niliyoeleza kama unataka kujua zaidi.
 
Hivi daktari bingwa ndio kwa kimombo anaitwa specialist?

Sijui ni mimi tu ama na wengine, huwa nahisi kama jina "daktari bingwa" linapotosha hivi? Si kama nadharau taaluma, nawaheshimu sana. Ni kama ilivyo kwa "wakili msomi" kwa taaluma ya sheria.

Hongera kwa hao kina dada kwa ubobevu.
Uko sahihi, bingwa ndio specialist. Kwa madaktari ni sahihi, ila kwa wanasheria au wahandisi, imekaa kisiasa, na hiyo ni Tz tu kutokana na ulimbukeni.
 
Fani ya udaktari mwanafunzi wa fani ya udaktari akisoma masters ya fani ya udaktari kwa mfano internal medicine ataitwa daktari bingwa wa magonjwa ya ndani,akisoma masters ya ngozi ataitwa daktari bingwa wa magonjwa ya ngozi,akisoma masters ya upasuaji mwanadamu ataitwa daktari bingwa wa upasuaji na akisoma masters ya magonjwa ya wanawake ataitwa daktari bingwa wa magonjwa ya wanawake.....sijui hasa swali lako kama kuna tofauti na haya niliyoeleza kama unataka kujua zaidi.
Basi hilo neno bingwa litakuwa halina maana sasa , Kama zaidi ya operation moja Dr anatokea mlango Wa nyuma.. Kuna jamaa mmoja Dr kwenye TV aliongea vizuri Sana ubingwa unakuja pale umetoka TR. au DR na Ushindi... Kama umenielewa
 
Uko sahihi, bingwa ndio specialist. Kwa madaktari ni sahihi, ila kwa wanasheria au wahandisi, imekaa kisiasa, na hiyo ni Tz tu kutokana na ulimbukeni.
mambo mengine si ya kulaumiana kuna historia huko nyuma kwa mfano mwanafunzi wa uchumi akimaliza shahada yake ya kwanzaataitwa mchumi akiwa na shahada ya uzamili ataitwa mchumi na akiwa na shahada ya tatu ya uchumi bado ataitwa mchumi kama Prof Lipumba huwa anaitwa mchumi tu.hiyo inatokana na historia ya namna gani wasomi wetu walianzwa kuitwa huko nyuma.lakini haizuii huwa mchumi wa PhD kuitwa Mchumi Bingwa wa kodi au Mchumi Bingwa wa kitu fulani.Hata mainjinia haizui kumuita Injia Bingwa wa Rejeta au Injia Bingwa wa Gearbox au Injinia Bingwa wa zege au Injinia Bingwa wa soft wire.
 
13 Reactions
Reply
Back
Top Bottom