Kwa mara nyingine tena Masele amedhihirisha udhaifu wa Spika

Nilijaribu kufuatilia mazungumzo ya mbunge Masele alipopewa nafasi ya kuomba radhi kule Bungeni. Kwanza kabisa hili jambo limetia aibu nchi yetu. Picha iliyopo ni ubabe tu usio na ulazima.

Masele analalamika kutiwa hatiani na Spika kwa kumuandikia Mwenyekiti wa PAP kuwa amesitishwa uwakilishi wa Bunge bila ya Masele Kusikilizwa na huyo mwenyekiti kutaka kuitumia barua hio kumfukuza na kumsimamisha. Huyu Ndugai kaonesha udhaifu mkubwa mno hapa.

Bila ya ujasiri wa Masele kusema haitambui barua ya Spika na kwamba ana baraka zote za Serikali ni wazi Masele angekwisha simamishwa. Asilolojiua Ndugai ni kuwa Masele kule anaiwakilisha nchi ya Tanzania Kutaka kufukuzwa Masele kwa njia hiyo ya Barua ya Ndugai ni usaliti wa wazi.

Jiulize kwa nini Masele amelazimika kuweka mambo hadharani pale Bungeni? Udhaifu wa Ndugai umeleta taharuki ya wazi kwa Mihimili iliyosababishwa na ndugai Mwenyewe na si Masele.

Kulikosekanaje mawasiliano ya ndani baina ya Ndugai na Masele kiasi cha kumfanya Spika aje hadharani pale Bungeni kumtuhumu masele, kumuhukumu na kumfrastrate aje kuhojiwa ? kipi kilipaswa kutangulia?

Naamini hili hata Waziri Mkuu na Mh Rais wameuona udhaifu wa Spika. Hakukuwa na haja kutumia nguvu kubwa kumshughulikia Masele wakati kukiwa na mgogoro kule Bunge la Afrika baina ya Mwenyekiti na wabunge na Ndugai kujiingiza hadharani kwenye kumfrastrate Masele kama si udhaifu wa kutumia Madaraka vibaya, usaliti au kiburi. Huyu Spika ni Dhaifu.

Hata jana alitaka kutumia madaraka yake kumuonesha Masele kuwa ni Mkosa ukweli umeeleweka.

Kwa mara nyengine tena Masele amedhihirisha udhaifu wa Spika.

Kishada
Mimi naona pia Masele anamadhaifu vile vile kumbuka ndugai hawezi kua mdhaifu kila siku ambacho sijaelewa ugonvi hasa nini?kwa maelezo ya spika Masele anataka apatiwe hadhi kama rais wa binge la Africa moja mabodigad ,nyumba kitu ambacho ndugai anadai mamlaka hayo hana.
 
Katika vitu ambavyo Tanzania imekosa toka 2015 ni viongozi wa mihimili miwili ,hakuna kabisa ni milembe type .
 
hapo kuna jambo sirini hivi hakuna ga utaratibu wa hansad ya mahojiano kuwekwa hazarani ili wabunge wote waone maana ripoti ya mwenyekiti wa mahojiano kaikataa maanayake yaliyohojiwa na aliyoyajibu siyo hayo
CAG pia alitaka hansard ya mahojiano kati yake na kamati kuwekwa hadharani ili wabunge waone alichoulizwa na alivyojibu. Hii kamati inaonekana inadanganya, haiwezekani CAG adai mahojiano yawekwe hadharani na Masele naye adai hivyo hivyo kama hakuna mambo yanayofichwa na ambayo kamati haitaki wabunge na watu wote wajue.
Inavyoonekana hukumu ya CAG na Stephano ilishatolewa hata kabla ya kamati kukaa na kuwahoji. Mengine ni maigizo tu.
 
Masele Akili nyingi sana...................

Na kashajua Spika akili ndogo............

Akakuza mgogoro kijanja, akatapanya vita.........................

Na kwenye hii issue amejijenga kisiasa.............

Kiboko ya Ndugai Kapatikana...........
 
Nilijaribu kufuatilia mazungumzo ya mbunge Masele alipopewa nafasi ya kuomba radhi kule Bungeni. Kwanza kabisa hili jambo limetia aibu nchi yetu. Picha iliyopo ni ubabe tu usio na ulazima.

Masele analalamika kutiwa hatiani na Spika kwa kumuandikia Mwenyekiti wa PAP kuwa amesitishwa uwakilishi wa Bunge bila ya Masele Kusikilizwa na huyo mwenyekiti kutaka kuitumia barua hio kumfukuza na kumsimamisha. Huyu Ndugai kaonesha udhaifu mkubwa mno hapa.

Bila ya ujasiri wa Masele kusema haitambui barua ya Spika na kwamba ana baraka zote za Serikali ni wazi Masele angekwisha simamishwa. Asilolojiua Ndugai ni kuwa Masele kule anaiwakilisha nchi ya Tanzania Kutaka kufukuzwa Masele kwa njia hiyo ya Barua ya Ndugai ni usaliti wa wazi.

Jiulize kwa nini Masele amelazimika kuweka mambo hadharani pale Bungeni? Udhaifu wa Ndugai umeleta taharuki ya wazi kwa Mihimili iliyosababishwa na ndugai Mwenyewe na si Masele.

Kulikosekanaje mawasiliano ya ndani baina ya Ndugai na Masele kiasi cha kumfanya Spika aje hadharani pale Bungeni kumtuhumu masele, kumuhukumu na kumfrastrate aje kuhojiwa ? kipi kilipaswa kutangulia?

Naamini hili hata Waziri Mkuu na Mh Rais wameuona udhaifu wa Spika. Hakukuwa na haja kutumia nguvu kubwa kumshughulikia Masele wakati kukiwa na mgogoro kule Bunge la Afrika baina ya Mwenyekiti na wabunge na Ndugai kujiingiza hadharani kwenye kumfrastrate Masele kama si udhaifu wa kutumia Madaraka vibaya, usaliti au kiburi. Huyu Spika ni Dhaifu.

Hata jana alitaka kutumia madaraka yake kumuonesha Masele kuwa ni Mkosa ukweli umeeleweka.

Kwa mara nyengine tena Masele amedhihirisha udhaifu wa Spika.

Kishada

Ugomvi wa wanaCCM huwa inaishia kusiko eleweka, Malima vs Marehemu Mengi, Masele Vs Spika nk wanasameheana ila angekuwa mbunge wa upinzani angepigwa burn vikao vyote vilivyosalia vya bunge la 9
 
Masele Akili nyingi sana...................

Na kashajua Spika akili ndogo............

Akakuza mgogoro kijanja, akatapanya vita.........................

Na kwenye hii issue amejijenga kisiasa.............

Kiboko ya Ndugai Kapatikana...........
angekuwa na akili asingekuwa CCM...
 
11 Reactions
Reply
Back
Top Bottom